NGORONGOJO: Usafiri wa watoto mkoani Kigoma

Kigoma Region Tanzania

JF-Expert Member
Joined
May 25, 2021
Posts
230
Reaction score
611
Ngorongojo ni usafiri uliokuwa ukitumika enzi za nyuma na hadi hivi sasa hapa mkoani Kigoma. Ngorongojo huundwa kwa miti migumu, hivyo mchakato wake wa utengenezaji unaanzia maporini ambapo ni lazima kwenda kutafuta miti migumu kwenye mapori.

Ngorongojo ina mpini "kishikio" ambapo hutegemea kupakwa mafuta ya mawese ili kuwezesha kuteleza na kukimbia kwa kasi zaidi. Mara nyingi huwa hazina breki, na nirahisi kukurusha na kukuacha na makovu kama sio kukutoa meno, (Ukiumia na ngorongojo unatakiwa kuficha makovu usifahamike nyumbani). Kusimama kwake hutegemea muinuko wa mlima, kwani Ngorongojo husaidia kwenye safari za maporomoko na mishuko.

Ngorogojo zingine huwekewa breki kwa kutumia kipande cha gamba la tairi ya gari au baiskeli ambapo ili usimame unabidi kukanyaga mzunguko huo wa tairi. Hivi sasa usafiri huu muhimu umekuwa adimu tofauti na enzi za nyuma.
Usafiri huu unaundwa kwa kutumia miti, na ndio chanzo kikuu cha kamptula za watoto kuchanika makalioni, ngorongojo inaongoza kwa kumaliza kamptula.

Huu ni ubunifu wa watoto wa Kigoma zinaitwa baiskeli za asili au ngorogojo ni katika hatua za makuzi ya kijana, gharama za kununua ngorongojo kwa asiyeweza kutengeneza ilikuwa ni kati ya Tsh 150 hadi 250 kipindi hicho. Kuikodisha ilikuwa ni kati ya Tsh 5 hadi Tsh 50.

196758009_3872428969477950_6670767037646725073_n.jpg
 
Umenikumbusha maisha ya kasulu enzi hizo...miaka ya 2000,watoto walikuwa wanazipenda sana hizi bike,pia watu wazima niliwashuhudia wakizitumia kubebea mizigo yao hasa mazao kupeleka sokoni...wengi walikuwa wakitoa mazao vijijini wanapeleka kasulu mjini pale sokoni sofya..kipindi hicho yaani nakumbuka mbali sana..natamani maisha yale yarudi vyakula ilikuwa bei rahisi sana ukienda sokoni sofya pale bakuli la maharage linauzwa 200-300..Dah ngorongojo tumezidandia sana sema zilikuwa za washkaji unaazima.

Kuna jamaa alikuwa mlemav, alikuwa anaitwa Paulo yeye alikuwa fundi makoroboi maeneo ya karibu na kwa Onesmo huyu alikuwa mfanyabiashara mkubwa enzi hizo...paulo aliimodify Ngorongojo yake akaiwekea jembe la baiskeli lenye mnyororo na pedali akawa anaichochea ngorongojo yake kwa mikono...nakuipanda kwake alikuwa anaipanda kama amelala vile,jamaa alikuwa mbunifu sana...ila baadae alitengenezewa baiskeli ya walemavu na waarabu waliokuwa na gereji maeneo kama unaelekea shule ya murubona.

Nakumbuka maeneo ya kagunga,msufini,kumsenga,sofya,mudyanda.mjini pale sokoni jirani ya kwa marehemu mzee Hasunu wa mabasi ya Fazili mawese na wale wasomali wa Embasy.
 
Duuuh! Kwa Mahsen Hapo ukiwa unaenda Shule ya Murubona.
 
Back
Top Bottom