HATARI NGORONGORO
- Siku za uhai wa Hifadhi ya Taifa hiyo yenye sifa za kipekee Duniuani zinahesabika
- hali ya muingiliano wa shughuli za binaadamu, mifugo, uhifadhi na utalii yazidi kuwa mbaya
- Makundi ya Mifugo mamia kwa maelfu yatanda kila kona ya hifadhi, magari ya watalii yapishana na Ng’ombe na kondoo barabarani badala ya Wanyama pori
- Matajiri wajenga majumba ya kifahari Hifadhini kinyume cha sheria iliyounda hifadhi hiyo huku wakitumia neno umasikini kama kinga
- Mabilioni ya shilingi yatengwa na asasi kutoka nchi jirani kuhakikisha hifadhi hiyo inapoteza umashuhuli wake
Hifadhi ya Taifa ya Ngorongoro ipo hatarini kupotea na kupoteza uhai na umashughuli wake kutokana nna kukithiri kwa shughuli za kibinaadamu ikiwemo ufugaji uliopitiliza kiasi, ujenzi wa nyumba zisizofuata taratibu za kihifadhi na shughuli nyingine za kibiashara
Mwaandishi wa habari hizi ameshuhudia bmakundi makubwa ya mifugo ikiwemo Ng’ombe, mbuzi, kondoo, punda, kuku, na mingineyo ikichukua eneo kubwa kuliko Wanyama wa asili wanaopendwa kufuatiliwa na watalii
Pamoja na kuzingatia ukweli kuwa Ngorongoro ni hifadhi ni hifadhi ya kipekee inayowahusisha Wanyama binaadamu na mifugo kwa pamoja lakini hali ilivyo kwa sasa inatisha kiasi cha kutishia usalama wa hifadhi na wananchi husika wa asili wanaoishi katika eneo hilo
Taarifa za uhakika ambazo gazeti hili imezitafiti ni kuwa mwaka 1959 wakati wakazi walioruhusiwa kuishi katika hifadhi hiyo kwa mchanganyiko wao na Wanyama pori, wakazi hao hawakuzidi watu elfu 9 tofauti na sasa wakazi hao wamefika zaidi ya laki moja na mifugo yao bwanayoimiliki ikikadiriwa kuwa zaidi ya laki6
‘’kwa mujibu wa taarifa wanasema kuna mifugo laki 2 na nusu, nadiriki kusema sio kweli, mifugo hii haipungui haipungui laki saba hadi laki nane…hebu angalia tangu tumeanza kuanza makundi ya ng’ombe, mbuzi na kondoo sasa hivi ni zaidi ya masaa mawili tunazunguka tunawaona tu…hii maana yake kuwa hata kama watu hawa wapo kisheria lakini inahitajika jitihada za makusudi kunusuru tatizo hili…hili ni tatizo kwa kweli’’. Alisema Paul Schenzern Raia wa ujerumani aliyekuwa katika safari za kitalii
Schezern ameongeza kuwa kwao wanavyoifahamu Ngorongoro nin kuwa eneo bora zaidi la kiutalii na kamwe hakuwaza kama angepita barabani akipishana na ng’ombe na mifugo mingine japokuwa alikuwa anaufahamu kuwa Ngorongoro wanaishi binaadamu na Wanyama lakini si kwa kiwango alichokiona
‘’nimetembea hifadhi kadhaa Duniani ambazo Wanyama na binaadamu wanaishi kwa asili, kwa kweli zinavutia n ahata kuishi kwao kunaemndana na uhifadhi wa mazingira, tofauti na hapa Ngorongoro…ntapata shida san akumshawishi mtu atakayeniomba ushauri juu ya kutaka kuja hapa. Nafikiri watetezi wa haki za binaadamu, mifugo, Wanyama na mazingira wanapaswa kupaza sauti ya pamoja kuinusuru hifadhi hii muhimu na bora’’. aliongezq
‘’unajua watu wanaweza kulalamika kwamba wanaishi humu na haipaswi kupangwa vizuri, lakini sio sahihi watetezi makini wa binaadamu wanatakiwa watetee kwanza usalama wa mazingira, usalama wa mazingira ya Ngorongoro ndio usalama wa Arusha, usalama wa Arusha ndio usalama wa Tanzania na ndio maana Dunia nzima kunakuwa na sheria kali zinazolinda mazingira…..kujazana kwa watu na mifugo hifadhini sio haifai tu kwa mifugo bali haifai zaidi kwa binaadamu wanaoishi nhumo kwani kuishi kwao kunategemea zaidi ikolojia nya hifadhi husika’’. Alisema Habibu Mchange, Mratibu wa mtandao wa wanahabari wanarasilimali asilia na taarifa alipoombwa kutoa maoni yake
Mchange alisema kuwa hata yeye alikuwa Ngorongoro mwishoni mwa mwaka jana na ameshuhudia ujenzi uliokithiri na unaovunja kabisa sheria na kanuni za uhifadhi na kuongeza kuwa anaandaa ziara ya wanahabari wanarasilimali asilia na taarifa kwenda kujionea hali ilivyo na kuuhabarisha umma na kuwataka wanaharakati kushirikiana kuokoa kivutio hicho muhimu
‘’hata mimi nilitembbea tembea mwishoni mwa mwaka, niliyoyaona Ngorongoro kwa kweli yanatisha na hayafai kusimuliwa hata kidogo, wadau nwa utalii, uhiofadhi na mazingira tusipochukua hatua na kupaza sauti, Ngorongoro itapotea kama upepo…..kwa kifupi tu nikuambie ndugu mwandishi kuwa NGORONGORO IPO HATARINI KUPOTEA’’. Aliongeza Mratibu Mchange
Taarifa na uchunguzi zaidi kuhusu kuharibika kwa ikolojia Ngorongoro na mitazamo ya wahusika wa pande zote muhimu tutawaletea katika matoleo ya siku zijazo