Ngorongoro hatarini kupoteza uhai na umaarufu wake kutokana na kukithiri kwa shughuli za binadamu

Walikuwa wangapi ?, na walikuwa wanaishi kama part ya ecosystem na viumbe wengine au walikuwa wanaishi kama sasa kwa kuharibu mazingira na kuwafanya hao viumbe wengine watoweke / kupotea ?

Hili sio tatizo la Tanzania tu, ni tatizo la kidunia..., sababu tumeshindwa kuishi kwa kutegemeana na mazingira yetu its just a matter of time kabla hatujapay the price (ingawa tumeshaanza kufanya hivyo)

“When the last tree has been cut down, the last fish caught, the last river poisoned, only then will we realise that one cannot eat money,”

By the way huo ulikuwa ni msemo wa wahenga fulani kabla ya ukoloni....
 
Hakuna kitu kama hicho. Wakiondolewa wamaasai pale basi Ngorongoro itakuwa na hadhi sawa na pori la akiba la Maswa tu basi.
Unadhani umaarufu wa Ngorongoro ni wanyama tu? Mbona Selous, Mikumi, Tarangire na Manyara zina wanyama lkn hazina umaarufu wa Ngorongoro?
 
Mwaka 1959 Wamaasai waliondolewa kwenye plains za Serengeti na serikali ya wakati huo. Na makubaliano mojawapo ni kubaki kwenye mfumo mzima wa Ngorongoro.
Mifugo inayofugwa na Wamaasai haina madhara kwa wanyamapori.
 
Serengeti nayo inawatu!?
 
Mwaka 1959 Wamaasai waliondolewa kwenye plains za Serengeti na serikali ya wakati huo. Na makubaliano mojawapo ni kubaki kwenye mfumo mzima wa Ngorongoro.
Mifugo inayofugwa na Wamaasai haina madhara kwa wanyamapori.
Aidha hujafuatilia au umeamua kuwa biased.
Ile mifugo inapeleka maradhi kutoka kwa mifugo ya kufugwa mpaka kwa wanyapori.
Watu wanaongezeka kila uchao pale Ngorongoro ni kweli hawezi kuishi nje ya Ngorongoro
na maisha yakaendelea!?
 
Aidha hujafuatilia au umeamua kuwa biased.
Ile mifugo inapeleka maradhi kutoka kwa mifugo ya kufugwa mpaka kwa wanyapori.
Watu wanaongezeka kila uchao pale Ngorongoro ni kweli hawezi kuishi nje ya Ngorongoro
na maisha yakaendelea!?
Ndio akili yako ilipoishia? Hayo magonjwa ya wanyama wafugwao yanatoka kwa binadamu? Mbona pointi yako haina maana.
Wanyama pori ndio wanaambukiza magonjwa kwa wanyama wafugwao kwa wingi. Acha ujinga.
Ninyi mnajisikiaje mkiambiwa mhame Same, Makanya na Hedaru, kisa kuna wanyama wa Mkomazi. Hifadhi ndio iliwafuata Wamaasai.
 
Hivi huelewi hata maaradhi yanayo wapata binadamu yanaweza wapata wanyama?
waliposema ukimwi umetokea kwa nyani ulikuwa hujazaliwa?
Hamna namna mtahama tu huko...
Maisha bila ngorongoro hamyawezi ama!?
Uoto wa asili wa kila siku unalalamikiwa kutoweka nyie hamtaki kuhama tu hameni kwa hiari
kabla shuruti haijaanza.
Watu wanahama kupisha migodi, wawekezaji ije kuwa urithi wa dunia?
 
Shame,
Nimeona mtalii Richard Branson billionaire muingereza, akizungukia mlima Kilimanjaro na hot air balloon, IPO kwenye page yake ya Instagram,

Sisi huku Ngorongoro tumeigeuza Machinga na machungaji complex, shaabaashhh!

Watakuja kweli kuangalia full suti za mabati, ng'ombe, mbuzi na kondoo?

TANAPA NGORONGORO CONSERVATION wanakula miposho Tu ya vikao!
 
Tuhame kwenda wapi? Hatuondoki. Hatuhami. Utaendelea kuota hivyo lkn hatuhami. Acheni ujinga bana.
 
Acha wivu, baba ako angekuwa na mifugo humo ungeandika?
 
Acha kutumika na CCM kwa nia ovu
 
Hifadhi yenyewe inatusaidia nini zaidi ya watawala kugawana pesa?
 
Lakini wajue tu kwamba wanatafuta crisis ambayo haijawahi kutokea.
 
Hali ya sasa ni mbaya mbaya mbaya sana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…