Ngorongoro huenda kuna "crime against humanity" ya kutisha

Mchango wa kijinga kabisa. Kwa upumbavu wa fikra hizi, nyumbu wakizaliana sana, itabidi Watanganyika wote wahamishiwe Zanzibar ili wanyama wajinafasi?

Facts gani mjinga anazitaka zinazoweza kumwondolea ujinga wake wa kudumu? Ushahidi upo wazi kuwa Serikali inawazuia watu huru kutoka taasisi mbalimbali wanaotaka kwenda kuupata ukweli. Kama hakuna uovu, unaogopa na kuficha nini? Kama serikali ingekuwa safi katika hili ingefurahia taasisi mbalimbali huru, vikiwemo vyombo vya habari vya kimataifa kwenda maeneo hayo ili ijisafishe na tuhuma za uovu.
 
Huu ndio ulinzi wenyewe. Wanyama wanalindwa kwelikweli
Your browser is not able to display this video.
 
Na wewe acha ukasuku,Wamasai ni jamii ya Wafugaji na wala hawali nyamapori na vilevile hawalimi.Sasa wanaathiri nini kama siyo Uhuni wa viongozi wa serikali.Unapozungumzia utunzaji wa misitu na uoto Tanzania huwezi kuwaweka kando Wamasai.
 
Mwambie Mama yako awaondoe na Waadzabe porini Ili waache kula mizizi,nyamapori na matunda,wanaharibu Mazingira.
 
Shida yenu amfuatalii mambo ya wanyamapori, taratibu zao, namna serikari inavyo manage ecosystem zao na kwanini mpaka leo tuna maeneo ya wanyama pori na hifadhi za taifa

Kwenye vichwa vyenu mnadhani bila ya management ya TANAPA mpaka leo mngekuwa na hifadhi za taifa; wakiachia tu binadamu waingilie maeneo ya wanyama pori,

Masaai ni wazimu tu
 
Mwarabu kaleta maendeleo gani? Zanzibar yenyewe aliijenga ovyoovyo,vichochoro kama Uswahilini,Buguruni kwa Madenge!
 
Wakenya wanafanyaje kule Masai Mara,mbona hatujasikia hamisha hamisha kama kwetu!
 
Na wewe acha ukasuku,Wamasai ni jamii ya Wafugaji na wala hawali nyamapori na vilevile hawalimi.Sasa wanaathiri nini kama siyo Uhuni wa viongozi wa serikali.Unapozungumzia utunzaji wa misitu na uoto Tanzania huwezi kuwaweka kando Wamasai.
Ukiwaacha wajifanyie mambo wanavyotaka na idadi yao inaongezeka hadi kuingia maeneo ya wanyamapori; mwisho wa siku nani atatwaa hayo maeneo Maasai au Simba.

Think
 
Wakenya wanafanyaje kule Masai Mara,mbona hatujasikia hamisha hamisha kama kwetu!
Hao sio ndio wanaotuongezea shida wanakuja upande wetu na kuongeza population density. Halafu hao Keretu wa Karatu wanadai ni ndugu zao wenyeji.

Maasai lazima atambue nchi ina sheria na hazieshimu.
 
Mbona msitu wa Amazon una Wanyama wakali lakini kuna jamii zinaishi umo kwa utaratibu maalumu uliowekwa na serikali,Why not Ngorongoro and Serengeti!!
Samia anapewa ushauri wa ovyo sana!
 
Ukiwaacha wajifanyie mambo wanavyotaka na idadi yao inaongezeka hadi kuingia maeneo ya wanyamapori; mwisho wa siku nani atatwaa hayo maeneo Maasai au Simba.

Think
Wewe huo utafiti ulifanya lini wa kuonesha kuwa uwingi wa Masai unaharibu ikolojia ya Ngorongoro?
Masai wamekuwepo hapo miaka mingi sana na wanatunza Mazingira,labda ungeniambia Kuna jamii ya Wakulima na jamii zingine zimehamia Ngorongoro,hapo ningekuelewa.
 
Mbona msitu wa Amazon una Wanyama wakali lakini kuna jamii zinaishi umo kwa utaratibu maalumu uliowekwa na serikali,Why not Ngorongoro and Serengeti!!
Samia anapewa ushauri wa ovyo sana!
Una fahamu size ya Amazon forest, ukubwa wake, hipo nchi ngapi na jinsi ushirikiano wa ulinzi.

Amazon Forest ni size ya EU continent if not more unaifananisha Ngororo; ukiona watu wanaharibu mazingira ni very remote places; sio wazi kama Masaai wanavyotaka kuharibu mbuga za Tanzania.

Jitihada za kumdhibiti Maasai kwa sasa sio optional ni za lazima.
 
So what usually happens to an eco system; when population density grows.

Shida yenu ni kwamba hamfuatilii hoja ya serikali; Maasai hawajafukuzwa Ngorongoro isipokuwa inahitaji control ya population ya watu kulinda wanyapori.

Serikali haivunji boma la mtu lilikuwepo kwa miaka mingi, ni muda wa wengine kusogea kutoingilia maeneo ya wanyamapori.
 
Bro tumia akili mnawahamisha Hao watu mnawapeleka wapi hio Jamii ni ya tofauti na Jamii zingine

Hauwezi ukaniambia unampeleka mmasai mwenye wake wa Tano na watoto 15 kwenye kijumba Cha room mbili na sebule ni udhalilishaji dhidi ya Hao watu ni mateso hamjawalipa pesa zao

Lakini pia Hawa jamaa wamekaa miaka mingapi huko wameharibu Nini?
 
Hakuna mtu anapelekwa mjini.

Wametengewa maeneo ambayo wanaweza kuranda kama wanavyopenda.

Na hawajafukuzwa Ngorongoro kama unavyosimuliwa ni kwamba hilo eneo kwa sasa imezuia expansion ya majengo mapya raia to preserve the wildlife habitat; wao hawataki kuelewa wanataka hakina swala na Simba ndio wawapishe wao.
 
ikiwa kama kuna crime against humanity kama unavodhani, then ni "Crime Scene".
kama mtu sio polisi au mpelelezi anakwenda kufanya nini kwenye crime scene area?
itakuwa ni jeshi dhaifu tu linaloweza kuruhusu mtu yeyote tu kuingia creime scene area.
therefore polisi wako sahihi ikiwa ngorongoro kuna crime agaist humanity. Hilo ni jambo moja.

Pili,
Aridhi yote Tanzania ni mali ya umma.
Imekabidhiwa kawa Rais kama mdhamini au msimamizi mkuu wa ardhi yote ya Tanzania kwa niaba ya waTanzania wote.

Kwahiyi basi mamalaka ya juu ya usimamizi wa ardhi Tanzania, ni Raisi wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania.

wsimamizi wengine wa ardhi, wakimsaidia Rais kwa mujibu wa sheria za nchi ni pamoja na;-

waziri wa ardhi.
kamishna wa ardhi.
Makamu kamishna.
Makamishna wasaidizi wa ardhi.
kamati za ugawaji ardhi.
baraza la kitaifa la ushauri la ardhi.
mamlaka za serikali za mitaa.
halmashauri ya kijiji.

sasa pamoja na mtazamo na maoni tofauti ya wanasiasa na wananchi kuhusu ardhi ya Ngorongoro, bado uamuzi wa taasisi zilizochukua hatua dhidi ya matumizi ya ardhi ya Ngorongoro ni sahihi na hata kesi za zuio zilizofunguliwa na wananchi hazitafua dafu bali, uamuzi wake utatoa elimu zaidi kwa wanasiasa na wanachi, juu ya nani anaweza kuamua nini kinaweza kufanyika kwenye ardhi ya Tz, kwasababu ukweli na haki ya mwenye uamuzia wa matumizi ya ardhi tanzania upo wazi kisheria.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…