Ngorongoro huenda kuna "crime against humanity" ya kutisha

Utaratibu wangu siku hizi watu kama nyie msio na adabu nawapeleka kwenye ignore list.

Personal sina muda wa kumtusi mtu au kuvumulia matusi anymore.

Thanks JF for the ignore option.
You're so sick today my friend what's your problem? Tell me I can help you, did you pay your bills?

Speak English!
 
Hapa kuna kitu, huenda kuna crime against humanity ya kutisha sana huko ngorongoro, na ninapenda kuwaonya wote wanaohusika

Mchanganuo wa hayo mambo ya kutisha ya ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu umebainisha bayana na Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu LHRC kama ifuatavyo :
SERA ZA KIKABURU ZA SERIKALI ZILIZOAMBATANA NA VIKWAZO VIKALI KWA WANANCHI ZAANIKWA

LHRC : Mpango wa Kuwahamisha Wakaazi wa Ngorongoro Usitumike Kunyanyasa Wananchi


View: https://m.youtube.com/watch?v=bqY1GrUeB5MMazito yaliyobainika huko Ngorongoro ambayo umma mkubwa wa ndani ya nchi na jumuiya za kimataifa inafaa kuyafahamu ni haya yafuata katika taarifa kwa umma toka LHRC Kituo Cha Sheria na Haki za Binadamu :
  • Makosa makubwa ya ukiukwaji wa haki za binadamu yanaendelea Ngorongoro
  • Maeneo hayo kugeuzwa gereza kubwa la wazi na kuzuia watu kuingia kufahamu madhila ya wakaazi wa eneo la Ngorongoro
  • Wananchi wawekewa vikwazo vikali vya kiuchumi kijamii na kimaendeleo
  • Wananchi kuhamishwa kinguvu
  • Kuzuiwa wananchi kuendeleza maisha ya hivyo njaa na utapiamilo kushambulia wakaazi
  • Serikali kusitisha kupeleka fedha za huduma za afya na vifaa tiba
  • Zahanati na shule kufungwa huku wahudumu na wafanyakazi wa sekta ya elimu na afya kuondolewa
  • Akaunti za fedha za asasi zilizokuwa wadau wa maendeleo kwa kushirikiana na serikali zimefungwa
  • Medical Flying doctors iliyokuwa ikishirikina na kanisa katoliki yazuiwa kutoa huduma
  • Zaidi ya watoto 24,000 kukosa huduma za chanjo hivyo kutishia magonjwa ya polio, TB na mengineo hatari yanaweza kulipuka kwa kasi kuathiri jamii na nchi nzima ya Tanzania
  • Kinamama wajawazito na watoto huduma zao za ambulance zasitishwa
  • N.k n.k
 
Kabla ya Ngorongoro kuwa Hifadhi tayari ni nyumbani kwao,

Kabla ya kuwa na Rais Wamasai walikuwepo Ngorongoro,

Kabla ya Samia kuwa Rais wameshapita Marais na wazalendo wa Taifa, Ngorongoro ni kwa Wamasai.

Amtafutie Mwarabu eneo lingine la kujenga hotels na kuchimba madini, Wamasai waendelee kuwepo kwenye ardhi yao ya Ngorongoro.

Mimi ni MTANGANYIKA, kura yangu ya Urais 2025 nitapiga KITANGANYIKA!
 
Mama Samia anaona Maasai kama sub human, digidigi, dawa huyu ni kutompa kugombea, akigombea anyimwe kura!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…