Wapinzani na wanaharakati walikuwa wakihoji kuwa Rais wetu si msikivu. Hata hivyo, leo Rais Samia amemtuma mwakilishi wake wa ngazi ya juu kabisa kuwasikiliza na kuzungumza na Wamasai wa Ngorongoro.
Walimaanisha kwamba Wamasai hawawezi kuzungumza na mtu mwingine zaidi ya Rais, lakini leo wamempokea Mkuu wa Mkoa na wameweza kuzungumza naye kwa uwazi.
Ukweli ni kwamba, kuna tofauti kubwa kati ya propaganda za mitandaoni na hali halisi ilivyo kwenye ardhi. Rais Samia ni mtu wa maridhiano, na wananchi wamejitokeza kwa wingi kusikiliza ujumbe kutoka kwake.