Wapinzani na wanaharakati walikuwa wakihoji kuwa Rais wetu si msikivu. Hata hivyo, leo Rais Samia amemtuma mwakilishi wake wa ngazi ya juu kabisa kuwasikiliza na kuzungumza na Wamasai wa Ngorongoro.
Walimaanisha kwamba Wamasai hawawezi kuzungumza na mtu mwingine zaidi ya Rais, lakini leo wamempokea Mkuu wa Mkoa na wameweza kuzungumza naye kwa uwazi.
Ukweli ni kwamba, kuna tofauti kubwa kati ya propaganda za mitandaoni na hali halisi ilivyo kwenye ardhi. Rais Samia ni mtu wa maridhiano, na wananchi wamejitokeza kwa wingi kusikiliza ujumbe kutoka kwake.
Makonda aangalie huku kutumwa kwake, faili lake Marekani bado hawajalifunga sasa wanamwingiza tena katika uhalifu wa kutumia chakula kama silaha ya kivita. Kwa kuzuia chakula kufika Ngorongoro, akumbuke Magufuli alikuwa ana kinga ya ki uRais naye mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan ana kinga ya kiuRais ya kutoshitakiwa.
Angalizo :
Shirika la Mpango wa Chakula Duniani WFP
Kupitia umoja wa mataifa UN baraza la usalama na baraza kuu la UN imepiga marufuku kutumia chakula kama silaha ya kivita.
Tanzania ni mwanachama wa kudumu wa Umoja wa Mataifa na imesaini makubaliano hayo na Azimio la Umoja wa Mataifa ya kutotumia chakula kama silaha ya kivita..
Sasa huko Karatu na Ngorongoro nchi ya Tanzania inakiuka maazimio ya Umoja wa Mataifa, hivyo wadau kama UN, WFP, FAO, EU / UMOJA WA ULAYA, wadau wa maendeleo kama nchi kubwa za Marekani ya Kaskazini, Ulaya zinaweza kuchukua hatua dhidi ya ....
Hii inaweza kuwa mlolongo wa ushahidi wa kesi kwenda The Hague ICC Mahakama ya Kimataifa Uholanzi ambapo Uhuru na Ruto waliponea chupuchupu lakini je makamanda wa polisi wana kinga ya kutoshitakiwa ?
CHAKULA KAMA SILAHA YA KIVITA
Jeshi la Polisi Karatu ladaiwa kuzuia chakula na mizigo kuingia Ngorongoro
View: https://m.youtube.com/watch?v=ov3Jd148cQc
Wananchi wa tarafa ya Ngorongoro ambao wanafanya maandamano ya amani katika tarafa hiyo wamesema kuwa Jeshi la Polisi Karatu linazuia magari yenye mizigo na chakula kuingia Ngorongoro.Wananchi hao wamesema kuwa zoezi hilo limewalenga wao waandamani.