Ngumu sana kwa vikundi kama Panya Road kushamiri kwenye tawala za Mkono wa chuma

Ngumu sana kwa vikundi kama Panya Road kushamiri kwenye tawala za Mkono wa chuma

Robert Heriel Mtibeli

JF-Expert Member
Joined
Mar 24, 2018
Posts
28,297
Reaction score
68,017
Kwema Wakuu!

Kutawala Kwa Mkono wa chuma Kwa faida na hasara zake. Moja ya faida ya kutawala Kwa Mkono wa chuma ni nadra Sana kusikia vikundi vya kipuuzi kama sijui panyaroad sijui nini. Ni ngumu Sana!

Watu wenye akili za kimabavu kikawaida hawapendi kushughulika na ishu ndogondogo Kama hizo. Kiufupi hawapendi kupoteza muda na vitu vya kijinga.

Ni tamko Moja tuu kutoa tahadhari kuwa vikundi na watoto HAO waache mara Moja vinginevyo kitakachofuata ni Ghadhabu ambayo haitazingatia Haki za Binadamu.

Dawa ya ku-deal na vikundi vya namna hiyo ni Moja tuu ambayo ukishawapata wa mfano basi wengine wanajifunza.

Mtu Kama hafuati haki za Binadamu hakuna haya ya kumpa haki za Binadamu.
Jino Kwa jino.

Kama wazazi na walezi watapiga kelele nao wawekwe ndani hata mwezi Kwa kushindwa Kulea watoto wao na kuletea taifa matatizo.

Ni kawaida wahalifu kutumia sheria vibaya hasa zile zinazowalinda. Ndio maana watu wanaotawala Kwa Mkono wa chuma kamwe sheria hawazizingatii Sana Kwa sababu huwezi zingatia sheria Kwa watu wasiozingatia sheria Kwa makusudi wakitegemea sheria hizo adhabu zake ni ndogo.

Hata NYUMBANI, Baba asipokuwa Anaongoza familia Kwa upole upole ni rahisi watoto kuharibika, lakini Baba akiwa mkora lazima familia inyooke. Yaani Kwa hiyari au Kwa lazima, watachagua wenyewe wanatakaje. Huwezi leta sheria za demokrasia katika nchi ya watu wajinga na watu Masikini Hilo nilishasemaga.

Hata hivyo, Watawala wanayohaja ya kuangalia namna watoavyo hukumu kulingana na Nia ya mkosaji au mtu anayetofautiana na Nchi. Kama ni Nia nzuri basi itajulikana lakini Kwa upande wa panya road au vitu vya namna hiyo kimsingi hapo ni Shaba.

Mtu Kama hataki mtoto wake asipigwe Shaba basi amfundishe vizuri. Au amwambie afanyie upanyaroad wake Kwa Baba au Mama yake. Akifanyia wengine aliwe kichwa. Wakipatikana wa mfano tuu hata watatu tuu. Huwezi sikia huo ujinga.

Ukatekate wenzako alafu ukikamatwa ATI haki zako zizingatiwe😀😀 labda watakaokukamata ni Baba zako.

Yaani Ukate wake na Watoto wa watu alafu uchekewe, embu kuweni serious kidogo.

Yaani uue watu alafu ati haki zako zizingatiwe, hizo sheria hata mbinguni hazijawahi kuwepo.

Mawazo haya ni Kwa wale wenye akili za mfumo wa Mkono wa chuma, wafuasi WA AZAZEL 😀😀

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Dar es salaam
 
Kama wazazi na walezi watapiga kelele nao wawekwe ndani hata mwezi Kwa kushindwa Kulea watoto wao na kuletea taifa matatizo.
Kesho yake utakuwa na mtoto kama huyo, ngoja tuone kama akipigwa shaba utafurahi kuwa UA maana naye ameua.

All in all, umeandika vizuri ila sweeping action/operations wataingia waliomo na wasiomo, kuzuia hilo unafanyaje?
 
Mungu alieumba mbingu na nchi alikuwa akiwapa "dhahama" jamii ya wanadamu wakiasi au kuendana kinyume na alichoelekeza. Fuatilia gharika, alivyochoma sodoma na gomora.

Uhalifu sio wa kucheka nao. Hii ikiachwa inaweza kuturejesha kwenye magari kusafiri mchana, maana usiku kuna jamaa wanafunga mitaa au barabara kuu kwa mawe.

IGP Wambura akaze buti, uhalifu na haki za binadamu havikai kwenye nyumba moja.
 
Kesho yake utakuwa na mtoto kama huyo, ngoja tuone kama akipigwa shaba utafurahi kuwa UA maana naye ameua.....

All in all, umeandika vizuri ila sweeping action/operations wataingia waliomo na wasiomo, kuzuia hilo unafanyaje?

Ishu ya kuwa na watoto wa Aina hiyo Hilo sio shida.

Mtoto kama halitaki kusikiliza maonyo ya Baba yake unataka Mimi kama Baba nifanyeje?
Apigwe Shaba hata kama nitaumia lakini No way.

Tabia za kuonea huruma matoto maasi Kama mashoga ni Dalili ya ushetani ambao wanaume tutalaumiwa.

Mama ndiye anapaswa na anayohaki ya kuwa na huruma na watoto lakini Baba, Kama toto linaendekeza ujinga ni Kupiga Shaba lisiendelee kukutia aibu.

Hizi sheria za siku hizi ndizo zinalea haya mambo
 
Uko sahihi under condition watakaouwawa wawe ni wale wahusika,hata viongozi huogopa kutoa amri kama hizo sababu watekelezaji wa amri huumiza hata wasiohusika na sometimes wahusika halisi wakiendelea kudunda mtaani.
 
Uko sahihi under condition watakaouwawa wawe ni wale wahusika,hata viongozi huogopa kutoa amri kama hizo sababu watekelezaji wa amri huumiza hata wasiohusika na sometimes wahusika halisi wakiendelea kudunda mtaani.

Yeah ni kweli kabisa.

Wewe Kama rafiki yako panyaroad ukiuawa ukiwa Naye sioni shida.
 
Mwishoni mwa Utawala wa JK mambo hayo yalikwepo lakini baada ya Kuingia JPM aliweza kudhibiti hili suala, aliwezaje ni kwamba alitoa amri Kwa Jeshi kuhakikisha wanawamaliza hao wahalifu.

Sio hao tu, hata wale waliokuwa wanaingia kwenye hifadhi za Wanyama Pori kufanya uhalifu kule waliuawa. Hii ilikuwa ni order kabisa ili kuthibiti uhalifu.

Hivi vyombo vinahitaji amri tu ya Amiri Jeshi Mkuu kuweza kutekeleza na kuwaondoa hao Panya Road
 
Not all the time unaweza jua rafiki yako anafanya nini akiwa gizani,especial Kwa watoto wa miaka 15 to 20
 
Exactly, yaani ukatekate wenzio mapanga, halafu eti wewe haki za binadamu zizingatiwe, kwakweli hao panya rodi nikuwaua tu kwa wale wataothibitishwa.
 
Mimi nadhani uanzishwe Uzi maalumu was kuwataja hap Panya road na maeneo yao itasaidia Sana kuwabaini. Kwa polisi kuwaanzisha upepelezi hao washukiwa.

Binafsi nawa Nitatoa ushirikiano ktk hili.
 
Nakumbuka kipindi Afande Mangu akiwa IGP Askari walikua wanauwawa vibaya Sana kwenye mabenki yaani unakuta Leo Askari wawili Tena baada ya siku kadhaa Askari Tena kapigwa lisasi aisee Magu alipomtoa Mangu na kumuweka siro ikawa ni ukikamatwa ni shaba tu mpaka Siro anatoka ujambazi ulipungua sana wakuua Askari na ukawa haupo kabisa , kwaiyo hawa madogo wanahitajika kuuwawa tu hakuna njia nyingine
 
Hii serikali sijui tu kwa kweli. Umeongea vyema sana
 
Nakumbuka nikiwa mkoa wa kagera Kulikua na ujambazi sana ila Barabara yakutoka wilaya ya bihalamulo kwenda muleba ,Kuna sehemu wanaita mlima wa Simba aisee magari yalikua yanatekwa haswa na watu kuuwawa na pia njia ya kutoka nyakanazi kueleke kigoma na Ile yakutoka rusahunga kuelekea ngara aiseee ilitolewa oda yaani polisi wakikamata mrundi ni shaba shabani Tena shamba kwenye zile point wanazoletea uhalifu baada ya kuwafyeka wale wa demo tu basi warundi wote wakaaufyata mkia mpaka leo hakuna Cha kuteka mabasi Wala nini
 
Kwamba unahamasisha Sheria na Katiba viwekwe pembeni, POLISI waruhusiwe kuua bila ushahidi!!!! POLISI uchunguzi wao itoshe na kuwa ushahidi wa kutosha mtu kuuwawa?

Ama Kweli ndani ya JAMII Pana WAUWAJI wengi kuliko MAGEREZANI .
 
Kabisa huu mchezo inatakiwa tuumalize wenyewe kwa kuwatoa watu wawili watatu kama mfano, maana mpaka sasa panyaroad 2 sisi 0.
 
Back
Top Bottom