Ngumu sana kwa vikundi kama Panya Road kushamiri kwenye tawala za Mkono wa chuma

Nimekuelewa vema kabisa. Si sahihi kuwapa polisi ruhusa ya kuua maana wataua waliomo na wasiokuwemo. Si sahihi kupewa ruhusa ya kuua!
 
Mimi nadhani uanzishwe Uzi maalumu was kuwataja hap Panya road na maeneo yao itasaidia Sana kuwabaini. Kwa polisi kuwaanzisha upepelezi hao washukiwa
Binafsi nawa Nitatoa ushirikiano ktk hili
Hapana, kuna wasiohusika watatajwa kuwakomoa kutokana na chuki binafsi tu. Maana hadi wanathibitishwa kuwa hawana hatia wameshalika sana.
 
Kesho yake utakuwa na mtoto kama huyo, ngoja tuone kama akipigwa shaba utafurahi kuwa UA maana naye ameua.

All in all, umeandika vizuri ila sweeping action/operations wataingia waliomo na wasiomo, kuzuia hilo unafanyaje?
Kwahyo mtoto wako akienda ua raia wasio na hatia na kuwaibia wewe kama baba unafurahia? Akiua naye auliwe period. Uchungu unaoutaja ndo huo mzazi wa mwingine anaupata sababu ya mtoto wako acheni kutetea upumbavu
 
Wazee baba nchi ikiwa na ajira hamna watu watajiingiza kwenye shughuli za uhalifu hata wanasiasa wataacha rushwa maana raia wanakuwa na nguvu za kuwaadhibu
 
Hata sasa wakiamua kuwasaka na kuwakomesha wote watatokomea..

Ila pamoja na hayo kuleana kindezi kumezidi ndio maana watu hata tozo hamtaki kulipa..

Angekuwepo yule jamaa tozo mungelipa na panyaroad wangetokomea ila hadithi za sijui haki sawa huwa zinakwamisha maendeleo..
 
Kwahyo mtoto wako akienda ua raia wasio na hatia na kuwaibia wewe kama baba unafurahia? Akiua naye auliwe period. Uchungu unaoutaja ndo huo mzazi wa mwingine anaupata sababu ya mtoto wako acheni kutetea upumbavu
Hayupo anayefurahia Damu ya raia kumwagika. Damu Si kitu kinatakiwa kizoeleke kumwagwa.

Damu Ina TABIA ya kudai KISASI endapo itamwagwa na raia au POLISI isivyo halali.

POLISI au raia wamewahi ua watu waliamini ni wahalifu baadae ikaja thibitika hawana HATIA.

Najua umekasirika bt tusiue kama wauaji wafanyavyo.

Sheria ichukue mkondo wake.

Ameeen.
 
Tatizo panyaroad mitaa ndo unawalea kama raia wengelikua na umoja wote wengekua ni vilema saiv
 
police,tiss,takukuru,tra nk wana act kama wasimamizi wa sheria ila lazima kuwe na ile kitu tunaita hydrolic,ktk mtambo.

hiyo inatoka kwa rais peke yake.
 
Wahalifu kama panya road wakifanya uhalifu asasi za haki za binadamu kimya ila wahalifu wakishughulikiwa asasi hizo hizo zinaamka kuwatetea. Makes you wonder wapo kwa maslahi ya nani?
 
Wahalifu kama panya road wakifanya uhalifu asasi za haki za binadamu kimya ila wahalifu wakishughulikiwa asasi hizo hizo zinaamka kuwatetea. Makes you wonder wapo kwa maslahi ya nani?

Hizo ni asasi za kutetea wahalifu.

Mashoga wakifanya ushoga zipo kimya Ila wakiguswa kelele.
Hizo ni asasi ni Kama wakala wa lusifa
 
Umeongea vyema. Mtoto akihasi, huyo ni adui hata kwa wazazi wake. Watoto kama hawa hawaoni hatari kuwadhuru au hata kuwaua wazazi pindi wakizuiwa kupata wanachotaka. Miaka ya nyuma kidogo, maeneo ya Kimara Mwisho, mtoto mmoja alimvizia baba yake na kumuua, kisa hakumpa alichohitaji kwa wakati aliotaka yeye. Nyie mnaoshupalia haki za binadamu naombea yawakute haya mambo ili akili iwakae sawa! Unateteaje ujinga?!
 

Mwanaume kikawaida hapaswi kuchekea upuuzi wala hapaswi kuwa na huruma na wapuuzi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…