Nguo ya kuazima/ kukodi/ sikuzote haistili mwili

Nguo ya kuazima/ kukodi/ sikuzote haistili mwili

Kumekua na makelele ya fijo pamoja na ndelemo za kuimba nakumsifu Jean baleke, Kama hufatilii mpira unaweza kudhani baleke kafunga magoli miambili la hasha Bali kaonyesha uwezo kidogo hata robo ya meddi kagere enzi zake hajafika kiwango Cha mwamba mk 14.

Babu yangu mzee NGWENA /WAHENGA walisema "nguo ya kuazima haistili mwili " nakubali kabisa huu msemo bila pingamizi,
Unaacha kusifu midabwada yako uliyoinunua karume/ mtumbani sagula sagula/ nguo za mafungu kwa buku jero unapata midabwada ya kutosha takiribani kumi kwa buku jero.

Inakuaje badala yakusifu mitumba yako ya Bei Chee unakuja kusifu suti ya kuazima kwa jirani Tena unatamba nayo na kudunda/unachekelea kwa madaha nakujiona wewe ndiyo kila kitu.

Hii inachekesha sana, Tena mpaka jirani aliyekuazima suti yake anakukumbusha kabisa kuwa "suti niliyokuazima ni suti yangu halali kabisa"
Kutokana na ujua ulio nao/ umbumbumbu unafurahi kwenda huku na huko ukiinadi kuwa suti yako ni "the talk of the Town' unasema kuwa suti yako ni "goal machine"

Nataka nione mzamiru,john bocco,Sawadogo,kapama, kibu Denis, na wachezaji wengine wakiimbwa na mashabiki wa Simba kwa vifijo na nderemo nyingi maana hao ndiyo wachezaji wetu tuliowasajiri kwa pesa zetu lakini Jean baleke kaja kwa mkopo kaja kupambana ili apate namba huko alikotolewa baada ya kuonekana kuwa kiwango kimeshuka.

Tukubali tukatae sikuzote nguo yakuazima haistili mwili, mwenye nayo akiichukua unabaki na midabwada yako kutoka karume, hii midabwada lazima ujivunie nayo na ulinge nayo maana ni vya kwako.
Leo unasema Baleke hajafikia hata robo ya uwezo wa Kagere.
Naomba uthibitishe ni lini uliwahi kuukubali ubora wa Kagere. Nje ya hapo itakuw ni vijembe tu
 
Ushawahi kuishi nyumba au chumba cha kupanga? Mwenye nyumba hana mamlaka na chumba nilichopanga mpaka mkataba uishe. Nina uwezo wa kimzuia mwenye nyumba kuingia chumbani kwangu na asinifanye kitu.

Shida ikwapi kama kwa miaka miwili BALEGOLI nampa full mshahara, matibabu, kambi na huduma nyingine huku tukiwa tumekubaliana anafunga tuu magoli mpaka 2025 January. Nambie mchezaji gani bongo anasajiliwa zaidi ya miaka miwili kwa mkataba?

Balegoli twende kazi ana hasira kweli kukosa hatrick kwa ihefu so amezamilia kuipata kwenye mechi ijayo ya tar 16, sijui anacheza na nani?
 
Leo unasema Baleke hajafikia hata robo ya uwezo wa Kagere.
Naomba uthibitishe ni lini uliwahi kuukubali ubora wa Kagere. Nje ya hapo itakuw ni vijembe tu
Umekuja tubishane kwa hoja au umekuja tufanyaje ?
 
Ushawahi kuishi nyumba au chumba cha kupanga? Mwenye nyumba hana mamlaka na chumba nilichopanga mpaka mkataba uishe. Nina uwezo wa kimzuia mwenye nyumba kuingia chumbani kwangu na asinifanye kitu.

Shida ikwapi kama kwa miaka miwili BALEGOLI nampa full mshahara, matibabu, kambi na huduma nyingine huku tukiwa tumekubaliana anafunga tuu magoli mpaka 2025 January. Nambie mchezaji gani bongo anasajiliwa zaidi ya miaka miwili kwa mkataba?

Balegoli twende kazi ana hasira kweli kukosa hatrick kwa ihefu so amezamilia kuipata kwenye mechi ijayo ya tar 16, sijui anacheza na nani?
Kwa hiyo nyumba uliyopanga unaweza ukajisigia nakuimba huko mitaani "this is my house"

Kama unafanyaga hivyo mkuu hongera sana.
 
Mbona wewe na wenzio kila siku mnatupigia kelele na mfungaji wenu ambaye naye hajamfikia hata kidogo predator MK14 na ambaye msimu uliopita alizidiwa na kijana mdogo mpole!?
Kazidiwa kimichongo au hufatilii mpira
 
Back
Top Bottom