Juandeglo
JF-Expert Member
- Dec 20, 2014
- 1,040
- 2,806
Hii sentensi nina kaka yangu alikuaga anaipenda sana. Alikuwa anadate na mdada ambae kwao..mama yake anaruka usiku. Sasa akawa anaambiwa na watu mtaani....yeye akawa anajibu hiv.Vaa tu mkuu. Uchawi hauendi kwa mentali 😅
Siku akiwa amelala, akatokewa na mama yake mkwe na shem wake mmoja...akashtuka sana...akaamka. akawa katika hofu nini hiki kimenitokea...akasema alale kwenye mkeka sio kitandani...akatokewa tena. Wakamwambia tumekukubali..kama mkwe wetu...and all other shit.
Mwenyewe alijikuta ameamka..akasali Baba yetu..na kukemea. Kuanzia siku hiyo...appetite na yule duu ikasepa, akabreak mahusiano...asubuhi alivyotusimulia tulicheka sana.. tukamuuliza si ulisema uchawi..hauendi kwa mentali?? Imekuaje...mentali kafa ama??