Watu wanamjua Mungu kwa neema ya Mungu au kwa jitihada zao?
Huyo Yehova ambaye kashajua maisha ya watu wote tangu wanazaliwa mpaka wanakufa kabla hawajazaliwa, kawapa watu hao uchaguzi gani katika kuamua matendo yao?
Kama upo njia panda leo 2016, unataka uamue kwenda kulia au kushoto, na Mungu alishajua kwamba utakwenda kushoto tangu kabla ulimwengu haujaumbwa, unaweza kwenda kulia?
mungu anawabariki wanaomtafuta kwa bidii. waebrania 11:6 inasemaa ''6 Lakini pasipo imani haiwezekani kumpendeza; kwa maana mtu amwendeaye Mungu lazima aamini kwamba yeye yuko,
na kwamba huwapa thawabu wale wamtafutao''. pia biblia inasema "utafute kwanza ufalme". kwahiyo rehema na jitihada vyote vinahitajika.
kwahiyo kama hauamini yupo na haumtafuti, hautaweza kumjua.
wakristo tunatumia biblia kutafuta majibu. biblia inaonyesha Mungu hawapangii watu mwisho wao. anajua mwisho wetu kulingana na matendo ya sasa. uwezo wa kubadilisha matendo yetu na mwisho wetu.
Mungu alimsihi Kaini abadili mawazo ili asipatwe na mabaya.
mwanzo 4:6-7.
'' 6 Bwana akamwambia Kaini, Kwa nini una ghadhabu? Na kwa nini uso wako umekunjamana?
7 Kama ukitenda vyema, hutapata kibali? Usipotenda vyema dhambi iko, inakuotea mlangoni, nayo inakutamani wewe, walakini yapasa uishinde". kumshauri Kaini wakati fate yake iko sealed ingekuwa kazi bure na unafiki.
kitabu cha Joshua sura ya 24 kinaeleza kwamba tuna uamuzi wa kuchagua na kusababisha mwisho mzuri au mbaya.
15. Nanyi kama mkiona ni vibaya kumtumikia Bwana, chagueni hivi leo mtakayemtumikia; kwamba ni miungu ile ambayo baba zenu waliitumikia ng'ambo ya Mto, au kwamba ni miungu ya wale Waamori ambao mnakaa katika nchi yao; lakini mimi na nyumba yangu tutamtumikia Bwana.
20. Kama mkimwacha Bwana na kuitumikia miungu migeni, ndipo atageuka na kuwatenda mabaya na kuwaangamiza, baada ya kuwatendea mema.