Nguvu inawezaje kutengeneza object?

Nguvu inawezaje kutengeneza object?

Mashahidi wa Yehova nimesoma nao miaka miwili.

Mzee wa Kanisa niliyekuwa assigned alishindwa kunijibu swali hili.

Hiyo sura ya 11 uliyoisema ni ya kitabu gani? Mstari wa ngapi?

Hiyo link sijaona jibu.
kitabu nimekiupload hapo juu. kinaitwa Biblia inafundisha nini? sura ya 11 inamaelezo kuhusu kuteseka na uovu. kwenye hiyo tovuti ukienda sehemu ya vitabu kinapatikana pia.
 
Kwa elimu yangu ya form two, JUA ndiyo chanzo cha nguvu zote za uumbaji hapa duniani. Unaweza kuona circulation ya maji inategemea uwepo wa jua. Kustawi kwa mimea kunategemea uwepo wa jua kwa maana ya kuyengeneza chakula chake kupitia PHOTOSYNTESIS. Hata ukiangalia uwepo wa milima, mabonde, mito, maziwa nk vinategemea uwepo wa jua. Hivyo basi, energy inakua circulated katika viumbe vilivyopo duniani ili kuunda objects. Energy pekeyake haiwezi kujitegemea na kuunda objects. Inategemea uwepo wa viumbe au vitu vingine ambavyo huunganishwa na energy ili ku form objects. Kwa jinsi ninavyoona formula itakuwa hivi:

Energy ➕ living/non living organism= object
Hii ni kwa upande wa sayansi

Kwa upande wa imani za kimungu wataalamu wanasema unapwofikiria jambo fulani kwa muda mrefu mawazo yako hu transform kuwa real objects. Nguvu iliyopo ndani yako hukusukuma kufanya kitu unachokifikiria kwa muda mrefu. Uwepo wa magorofa pacha ya BOT ni mtu alikuwa na wazo baadae akalibadiri kuja kwenye uhalisia.

Mshua
 
kitabu nimekiupload hapo juu. kinaitwa Biblia inafundisha nini? sura ya 11 inamaelezo kuhusu kuteseka na uovu. kwenye hiyo tovuti ukienda sehemu ya vitabu kinapatikana pia.
Kwa nini Mungu pale alipoanza kuumba ulimwengu, kabla hajaumba chochote, hakuamua kuumba ulimwengu ambao maovu hayawezekani?

Sijaona jibu la swali hili.

Unaweza kunijibu?

Ukiniambia habari za watu kuasi, hilo si jibu. Kwa sababu hilo lilitokea baada ya uumbaji wa Mungu.

Ukiniambia shetani ndiyo sababu, hilo si jibu. Kwa sababu hilo lilitokea baada ya uumbaji wa Mungu.

Sijaona jibu linaloelezea kwa nini Mungu, kabka ya kuumba chochote, aliamua kuumba ulimwengu ambao mabaya yanawezekana wakati alikuwa na uwezo wa kuumba ulimwengu ambao maovu hayawezekani.

Yehova alichagua kuumba viumbe ambao wangepata matokeo kulingana na matendo yao. sizani kama hilo linamfanya kuwa mkatili. kuwapa watu uhuru wa kuchagua halafu ukawa unacontrol matokeo ni kupoteza maana ya uhuru wa kuchagua. Mungu anaenda kwa principle na sheria.
 
Unajuaje kwamba huyo Mungu yupo na si hadithi tu?
Rejea post zangu #49 na #52. Kisha uthibitishe kuwa huyu si Mungu ni Mdoli. Ninasubiri uthibitisho wako wa kuwa Nguvu na Sheria isiyoweza kujipinga ni Mdoli. Tafadhali thibitisha madai yako. Anaita sasa.
 
Yehova alichagua kuumba viumbe ambao wangepata matokeo kulingana na matendo yao. sizani kama hilo linamfanya kuwa mkatili. kuwapa watu uhuru wa kuchagua halafu ukawa unacontrol matokeo ni kupoteza maana ya uhuru wa kuchagua. Mungu anaenda kwa principle na sheria.
Watu wanamjua Mungu kwa neema ya Mungu au kwa jitihada zao?

Huyo Yehova ambaye kashajua maisha ya watu wote tangu wanazaliwa mpaka wanakufa kabla hawajazaliwa, kawapa watu hao uchaguzi gani katika kuamua matendo yao?

Kama upo njia panda leo 2016, unataka uamue kwenda kulia au kushoto, na Mungu alishajua kwamba utakwenda kushoto tangu kabla ulimwengu haujaumbwa, unaweza kwenda kulia?
 
Rejea post zangu #49 na #52. Kisha uthibitishe kuwa huyu si Mungu ni Mdoli. Ninasubiri uthibitisho wako wa kuwa Nguvu na Sheria isiyoweza kujipinga ni Mdoli. Tafadhali thibitisha madai yako. Anaita sasa.
Nikikwambia kwamba chumbani kwako kuna ta ya dhahabu isiyoonekana inazunguka hewani utakubali au utakataa?
 
Mpo salama waungwana?

Swali hili ningependa haswa kulipeleka katika pande mbili (2) kwenye sayansi na wanaoamini uwepo wa Mungu.

Katika sayansi ningependa kuhoji hivi je, ni kivipi nguvu inaweza kutengeneza/kutokeza object?

Katika upande wa Waumini wa Mungu naomba kuhoji hivi
kama ilivyoandika na vitabu vyake kwamba kwa kutumia uweza wake ama nguvu zake Mungu aliumba kila kitu. Swali hapa ni je, ni kivipi nguvu hiyo ya Mungu iliweza kuumba/kutokeza/kuunda objects kama dunia,nyota n.k?

Ni hivyo tu wakuu mnakaribishwa.

KISAYANSI:
Mass to energy
- Einstein ametuonesha namna ya kubadili matter (object) kuwa nishati au nguvu (E=MC2). Hii ilm yake ndiyo tunayotumia kutengeneza mabomu ya nyuklia au umeme wa nyuklia (pia ndicho kinachotokea kwenye jua letu na kutuletea mwanga na joto).

Energy to mass - Hii pia inawezekana na ndicho kilichotokea wakati wa BIG-BANG ambapo energy-fields zilipata mass na kutengeneza Hydrogen. Particles kwenye energy fields zinazoweza kuweka mass zinajulikana kama HIGGS-BOSONS.
Hizi fields zinaweza kutengeneza (create, YES KUUMBA) mass from pure energy. Wanasayansi huziita hizi Higgs bosons - GOD particles kwa sababu zinaweza kuumba kitu kutoka pure energy. Uwepo wa hizi Higgs Bosons umethibitishwa na utafiti unaoendelea Switzerland kwenye lile collider lao.

Sijui hapa ndio wanasayansi wanatuambia kuwa Mungu yupo in the form ya hizi Higgs bosons?

Ukitaka kujua zaidi kuhusu hizi GOD-Particles google au anza hapa chini.

Higgs boson - Wikipedia, the free encyclopedia

KIDINI:
Sijui!
 
Nikikwambia kwamba chumbani kwako kuna ta ya dhahabu isiyoonekana inazunguka hewani utakubali au utakataa?
Isiyoonekana na nani, na nini? Thibitisha. Pia usikwepe swali langu, je Nguvu na Sheria zilizofanya ulimwengu na zisizoweza kujipinga zenyewe zinakuwaje Mdoli? Anaita sasa.
 
Watu wanamjua Mungu kwa neema ya Mungu au kwa jitihada zao?

Huyo Yehova ambaye kashajua maisha ya watu wote tangu wanazaliwa mpaka wanakufa kabla hawajazaliwa, kawapa watu hao uchaguzi gani katika kuamua matendo yao?

Kama upo njia panda leo 2016, unataka uamue kwenda kulia au kushoto, na Mungu alishajua kwamba utakwenda kushoto tangu kabla ulimwengu haujaumbwa, unaweza kwenda kulia?

mungu anawabariki wanaomtafuta kwa bidii. waebrania 11:6 inasemaa ''6 Lakini pasipo imani haiwezekani kumpendeza; kwa maana mtu amwendeaye Mungu lazima aamini kwamba yeye yuko, na kwamba huwapa thawabu wale wamtafutao''. pia biblia inasema "utafute kwanza ufalme". kwahiyo rehema na jitihada vyote vinahitajika.
kwahiyo kama hauamini yupo na haumtafuti, hautaweza kumjua.

wakristo tunatumia biblia kutafuta majibu. biblia inaonyesha Mungu hawapangii watu mwisho wao. anajua mwisho wetu kulingana na matendo ya sasa. uwezo wa kubadilisha matendo yetu na mwisho wetu.
Mungu alimsihi Kaini abadili mawazo ili asipatwe na mabaya.
mwanzo 4:6-7.
'' 6 Bwana akamwambia Kaini, Kwa nini una ghadhabu? Na kwa nini uso wako umekunjamana?
7 Kama ukitenda vyema, hutapata kibali? Usipotenda vyema dhambi iko, inakuotea mlangoni, nayo inakutamani wewe, walakini yapasa uishinde". kumshauri Kaini wakati fate yake iko sealed ingekuwa kazi bure na unafiki.

kitabu cha Joshua sura ya 24 kinaeleza kwamba tuna uamuzi wa kuchagua na kusababisha mwisho mzuri au mbaya.

15. Nanyi kama mkiona ni vibaya kumtumikia Bwana, chagueni hivi leo mtakayemtumikia; kwamba ni miungu ile ambayo baba zenu waliitumikia ng'ambo ya Mto, au kwamba ni miungu ya wale Waamori ambao mnakaa katika nchi yao; lakini mimi na nyumba yangu tutamtumikia Bwana.

20. Kama mkimwacha Bwana na kuitumikia miungu migeni, ndipo atageuka na kuwatenda mabaya na kuwaangamiza, baada ya kuwatendea mema.
 
Ukitaka kujua mengi anza na kujifunza hiyo lugha.

Kiranga hawezi kukutafsiria kila kitu.
Sio kwamba huwezi kutafsiri kila kitu ila we mwenyewe una meza tu hiyo midubwasha na unashindwa kufanya uchambuzi. Mtu kaanzisha mada humu ili watu wajadiliane kwa pamoja kila mtu aeleze anachokijua,we unajaza mi link tu.
 
Isiyoonekana na nani, na nini? Thibitisha. Pia usikwepe swali langu, je Nguvu na Sheria zilizofanya ulimwengu na zisizoweza kujipinga zenyewe zinakuwaje Mdoli? Anaita sasa.
Hilo swali lako la "thibitisha" ndilo nililolitaka.

Unaniambia nithibitishe kitu ambacho hakipo na hakionekani, nitaanzaje kuthibitisha?

Hapo ndipo utaona ugumu wa kuthibitisha Mungu hayupo.

Ila, kwa mantiki, nimeshathibitisha Mungu hayupo kwa contradiction.

An all loving, all knowing and all capable God couldn't have created this imperfect world which is full of evil. He would have done a much better job.

Swali lako la "Pia usikwepe swali langu, je Nguvu na Sheria zilizofanya ulimwengu na zisizoweza kujipinga zenyewe zinakuwaje Mdoli?" lina msingi wa uongo.

Lina msingi wa uongo kwa sababu linasema "zisizoweza kujipinga zenyewe" wakati nakuonyesha kwamba huyo Mungu wenu mwenye upendo wote, ujuzi wote na uwezo wote kuumba ulimwengu huu ambao mabaya yanawezekana ni kujipinga mwenyewe tayari.

Hawezi kuwepo kwa sababu idea ya kuwepo kwake inajipinga yenyewe.

Hawezi kuwepo kama pembetatu ambayo hapo hapo ni duara isivyoweza kuwepo.

Habari za Mungu, sawasawa na habari ya pembetatu duara, inajipinga yenyewe.
 
mungu anawabariki wanaomtafuta kwa bidii. waebrania 11:6 inasemaa ''6 Lakini pasipo imani haiwezekani kumpendeza; kwa maana mtu amwendeaye Mungu lazima aamini kwamba yeye yuko, na kwamba huwapa thawabu wale wamtafutao''. pia biblia inasema "utafute kwanza ufalme". kwahiyo rehema na jitihada vyote vinahitajika.
kwahiyo kama hauamini yupo na haumtafuti, hautaweza kumjua.

wakristo tunatumia biblia kutafuta majibu. biblia inaonyesha Mungu hawapangii watu mwisho wao. anajua mwisho wetu kulingana na matendo ya sasa. uwezo wa kubadilisha matendo yetu na mwisho wetu.
Mungu alimsihi Kaini abadili mawazo ili asipatwe na mabaya.
mwanzo 4:6-7.
'' 6 Bwana akamwambia Kaini, Kwa nini una ghadhabu? Na kwa nini uso wako umekunjamana?
7 Kama ukitenda vyema, hutapata kibali? Usipotenda vyema dhambi iko, inakuotea mlangoni, nayo inakutamani wewe, walakini yapasa uishinde". kumshauri Kaini wakati fate yake iko sealed ingekuwa kazi bure na unafiki.

kitabu cha Joshua sura ya 24 kinaeleza kwamba tuna uamuzi wa kuchagua na kusababisha mwisho mzuri au mbaya.

15. Nanyi kama mkiona ni vibaya kumtumikia Bwana, chagueni hivi leo mtakayemtumikia; kwamba ni miungu ile ambayo baba zenu waliitumikia ng'ambo ya Mto, au kwamba ni miungu ya wale Waamori ambao mnakaa katika nchi yao; lakini mimi na nyumba yangu tutamtumikia Bwana.

20. Kama mkimwacha Bwana na kuitumikia miungu migeni, ndipo atageuka na kuwatenda mabaya na kuwaangamiza, baada ya kuwatendea mema.
Huo uwezo wa fulani kumtafuta Mungu kwa bidii na mwingine kukosa uwezo huo huwa unatoka wapi?
 
Sio kwamba huwezi kutafsiri kila kitu ila we mwenyewe una meza tu hiyo midubwasha na unashindwa kufanya uchambuzi. Mtu kaanzisha mada humu ili watu wajadiliane kwa pamoja kila mtu aeleze anachokijua,we unajaza mi link tu.

Unaweza kunipa mfano unaoonesha kwamba maneno yako ni ya kweli na si hadithi za uongo tu?

Kitu gani nimeshindwa kukichambua?

Hoja gani nimeshindwa kuichambua?

Mimi naweza kukupa mfano wewe.

Kati ya mimi niliyekuuliza imekuwaje Mungu mwenye uwezo wote, ujuzi wote na upendo wote kaumba ulimwengu ambao mabaya yanawezekana wakati alikuwa na uwezo wote, ujuzi wote na upendo wote wa kuumba ulimwengu ambao mabaya hayawezekani, na wewe uliyeshindwa kujibu swali, nani kashindwa kufanya uchambuzi?
 
Huo uwezo wa fulani kumtafuta Mungu kwa bidii na mwingine kukosa uwezo huo huwa unatoka wapi?
siyo uwezo ni uchaguzi. na mara nyingi tunachagua kwa kuangalia faida. kuna wengine wanaona kumtafuta Mungu kuna faida na wengine wanaona hakuna faida. kuna wengine hadi walichagua kumtumikia/kumtafuta Mungu dhidi ya uhai wao. hakuna watu wenye kuzaliwa na uwezo mdogo wa kumtafuta mungu.
 
Unaweza kunipa mfano unaoonesha kwamba maneno yako ni ya kweli na si hadithi za uongo tu?

Kitu gani nimeshindwa kukichambua?

Hoja gani nimeshindwa kuichambua?

Mimi naweza kukupa mfano wewe.

Kati ya mimi niliyekuuliza imekuwaje Mungu mwenye uwezo wote, ujuzi wote na upendo wote kaumba ulimwengu ambao mabaya yanawezekana wakati alikuwa na uwezo wote, ujuzi wote na upendo wote wa kuumba ulimwengu ambao mabaya hayawezekani, na wewe uliyeshindwa kujibu swali, nani kashindwa kufanya uchambuzi?
Haujaniuliza swali katika Uzi huu halafu ulivyomuongo unasema sijajabu swali lako wakati haujaniuliza swali.

Kama ungeweza kufanya uchambuzi ingekuwa hakuna ya kuweka link,unafikiri kila mtu akiwa mtu akiweka link ndiyo itakuwaje humu?
 
siyo uwezo ni uchaguzi. na mara nyingi tunachagua kwa kuangalia faida. kuna wengine wanaona kumtafuta Mungu kuna faida na wengine wanaona hakuna faida. kuna wengine hadi walichagua kumtumikia/kumtafuta Mungu dhidi ya uhai wao. hakuna watu wenye kuzaliwa na uwezo mdogo wa kumtafuta mungu.
Kichaa ana uchaguzi gani wa kumtafuta Mungu?
 
Haujaniuliza swali katika Uzi huu halafu ulivyomuongo unasema sijajabu swali lako wakati haujaniuliza swali.

Kama ungeweza kufanya uchambuzi ingekuwa hakuna ya kuweka link,unafikiri kila mtu akiwa mtu akiweka link ndiyo itakuwaje humu?
Wewe husomi ninavyokujibu au una makengeza au huna uwezo wa kulijua swali ukiliona?

Unasema sijakuuliza swali katika uzi huu wakati post unayonukuu imekuuliza maswali?
 
Kichaa ana uchaguzi gani wa kumtafuta Mungu?
Mungu ana njia ya kushughulika na watu kama hao na wale ambao hawakuwahi kabisa kusikia habari njema. hata kibinadamu tunajua wagonjwa wa akili ni special cases.
 
Back
Top Bottom