The Phylosopher
JF-Expert Member
- Mar 11, 2015
- 1,968
- 2,957
Inavyoonekana kupata uongozi ndani ya ccm ni jambo la kufa na kupona ndio maana uchaguzi wao una vitimbi na vituko vingi Kwa kiwango cha kufuatiliwa sana na wafuasi na wasiowafuasi.
Kilichonitisha ni misuli inayotumika kushinda uchaguzi. Misuli hii inawajengea ccm uzoefu wa kushinda kwa njia yoyote.
Natamani wapinzani wapate somo kwamba kushindana na ccm ni kushindana na jitu lililozoea game za staili zote.
Ikiwa wao kwa wao ambao mwisho wa siku wanatumikia maslahi ya chama chao wanaweza kukwidana kukabana kutoana nundu na ngeu namna hii, vipi kuhusu ww mwenzangu na mm ambae Kwa sehemu ni adui wa maslahi ya chama nini kitakupata?