Huyu mwamba kawa N/waziri wa ujenzi na baadae Waziri 1995-2005
akawa waziri wa nyumba na makazi 2006-2007
akawa waziri wa mifugo & uvuvi 2007-2010
akawa tena waziri wa ujenzi 2010-2025
Rais wa JMT 2015-March 2021
kama kiongozi kuna mengi mema kafanya (hii inamfanya akumbukwe kwa wema)
kama kiongozi kuna watu waliumia kwenye kutendaji wake wa kazi (hii itafanya watu wamkumbuke pia, kwa namna walivyoumia)
Wengi wote tumesoma shule na baadae vyuoni, it was not smooth all the way through ila ndio shule ilivyo.
Wakazi kama wa Magomeni kota, unadhani wana kumbukumbu gani kwa mtu aliewarejeshea hadhi yao ya ukaazi kwa kuwajengea nyumba bora zaidi?
Wazee wa tembo (kipindi kabla Urais wake tembo walipungua sana) bila shaka watakuwa na ill feeling.
Kuna watu kawatoa kwenye professional zao na huenda hawakuwahi kuwaza kuwa wanasiasa kwenye level ya uwaziri Dr. Mpango, Prof. Mkumbo, Prof. Kabudi, Prof. Mkenda; hawa wote walikuwa wananzuoni, at some point kupitia mikononi mwake, leo hii wengine bado ni mawaziri, mwingine VP na wengine wanakumbukwa kukalia cabinet post.
SUMA JKT, Watumishi Housing na TBA watamkumbuka kwa kuwa-empower kwa local content kwenye ujenzi wa Idodomya, jambo ambalo zamani construction of many public buildings walikuwa wachina na kuna waliokuwa wanavuta 10%.
Amecha gold purification plant ya kwanza EA na serikali (STAMICO) akiwa mbia
Amenzisha SGR project ambayo itakuwa ndefu kuliko zote africa siku ikikamilika
Ameanzisha JNHPP ambayo ikikamilika itakuwa na umeme nafuu na wa kutosha kuliko uwezo wa mitambo ya sasa.
Amecha kumbukumbu ya kujenga ukuta Mirerani ili kudhibiti utoroshwaji wa gemstone (Tanzanite)
Fika Mafinga, aliwafanya wauza nguzo kupata biashara, wakati zama zile nguzo zilikuwa zinatoka bondeni.
Aliasisi mikoa ya ofisi za madini iwe na masoko ya madini na biashara ya madini iwe na uhalali na serikali ipate kodi na watu kudhulumiana kukome.
Alisimimia maslahi ya taifa ya kuifanya serikali kuwa na ubia kwenye Twiga Corporation (Barrick akiwa mbia) na Tembe Corporation (Kabanga Nikel)
Nidhamu ya kazi iliongezeka na wananchi walihudumiwa bila kuwa "unajua mimi ni nani"
Aliweza kudhibiti/kuondoa wapiga deals za mishahara hewa.
Alimpa Bakheresa shamba na kumsisitiza azalishe sukari badala ya kuendelea ku-import sukari huku, akijua sukari ni raw material ya viwanda vyake,
Wakulima wa korosho kupata mpaka elfu 4 kwa kilo moja ikapelekea mpaka mbuzi, kunyweshwa soda.
Amekuwa sehemu ya ujenzi wa madaraja makubwa akiwa waziri na Rais (Mkapa bridge, Kigamboni bridge, Tanzanite Bridge, Mfugale Flying over na Kijazi) unganisha vile kaviacha vinajengwa.
Amekuta nchi haina ndege hata moja, na sasa wana ndege za abiria na ya mizigo iko njani kukamilika.
Ameikuwa Channel 10 na Magic FM zikimilikiwa na mtu aliezinunua kwa hela ya CCM na sasa wana-CCM imekuwa mali yao.
Alihakiki mali za chama chake na kuwaondoa wana-CCM wenzake kwenye ulaji ambao waliozoea.
Namna alivyo-handle covid 19 na kutokuweka lockdown na kusisitiza watu wafanye kazi, wachukue tahadhari, wavae barakao za vitenge, vitambaa kujikinga then akafungua shule na vyuo watoto/vijana wakarejea shule/vyuo; uamuzi ule haukuwa mwepesi, ila alisimama na Watanzania.
Kiubinadamu, atakuwa celebrated kwa mema. Ila kuna ambao waliumia au kuumizwa nao, watakuwa na yao ya kusema.
Kiufupi, jina lake liko vijiweni, whatsapp group chats, mainstream media, social media. Vyovyote vile, itachukua muda JPM kusahaulika.
Ameacha historia ya kuwa na VP wa kwanza mwanamke ambae amegombea nae vipindi viwili (2015, 2020) ambae kwa sasa pia ndio CinC.
Ameacha watoto ambao hawajulikani kama wana "ma-deal" kama walivyo watoto wa.....