Hayo maswali yako yanaakisi mpasuko alioukuwa ameutengeneza(kwa makusudi) ili iwe rahisi kwake kuliburuza taifa vile atakavyo.
Watu wa middle class na upper class ndiyo aliwaona kama threat kwa kuwa wengi wao wanajitambua hivyo alihakikisha anawatesa, anawadhulumu na alihakikisha anaharibu biashara zao(hakutaka private sector ikue) labda kwa zile biashara alizokuwa na maslahi nazo. Sasa kwa wale wenzangu na mimi wasiojielewa(wanyonge) alifanikiwa sana kuwahadaa kwa kuwa wengi wao hawana exposure na aliwa-brainwash mpaka hivi leo muda umeshapita wa kutosha tangu amefariki bado wanamuona ni 'mungu-mtu' hivyo hawaachi kumuabudu, alitengeneza kitu kinachoitwa divide and rule kwa makusudi kabisa.
Huu mpasuko utachukua muda mrefu kufutika kwani sumu aliyoipabdikiza ilikolea haswa, watu wenye mitazamo tofauti walichukuliana kama maadui hata mtu akiuawa, akitekwa, akipoteza au akidhulumiwa biashara zake wale wa upande tofauti walifurahia bila haya. Utu na udugu wa Kitanzania ulipotezwa kabisa.
View attachment 2553183