YE67NBE
JF-Expert Member
- Nov 30, 2015
- 15,155
- 36,337
Salaam kwenu wote,
Mimi ni mgeni humu ila ningependa kushare kisa kidogo cha maisha ya ujana wangu. Nimezaliwa 1953.
Kusema kweli mwenyezi Mungu alinijalia sana mimi, kwenye elimu ya darasani nilikuwa vizuri sana nikafanikiwa kumaliza chuo mwaka X kipindi hicho. Bahati nzuri nikapata kazi yangu kwenye kampuni Y, nilifanya kwa miaka 3 kabla ya kuhamishwa kupelekwa kwenye kituo kingine. ambapo nilipata mshahara na marupu marupu matamu kweli. Nilitumikia hiyo nafasi kwa miaka 35.
Mpaka nilivyostaafu rasmi 2016, namshukuru Mungu sana kwa kunijaalia akili ya kuona mbele, na kuweza kupanga hatma ya maisha yangu.
Niliweza kujiingiza kwenye kuwekeza kwenye vitega uchumi mbalimbali ambavyo ndo vinanilea sasa hivi.
Nawashauri vijana mtakaosoma hiki kisa tafadhali tafadhali tumieni muda wenu vizuri, msije mkajuta baadae mkiona mzee ni masikini jua haikuja hivi hivi, likewise mkiona mzee ni tajiri jua ni tu watu walijitoa haswa haswa,
Zingatia: Tumieni ujana wenu vizuri, narudia tena tumieni ujana wenu
Vizuri, narudia tumieni ujana wenu vizuri. Msije Mkajuta kwenye uzee wenu, maana muda utakuwa umekutupa mkono na ndipo maradhi yatakavyoanza kukushambulia.
Kwangu mimi navyoona umri wa kuweka nguvu ni (25-55) hapa ndo inabidi ufanye uwekezaji mkubwa na uchakarike sana.
Lakini kumbukeni pia kumtanguliza Mungu kwenye kila mfanyacho ili azidi kuwabariki. Mimi namshukuru Mungu wanangu 4 wapo vizuri kila mtu yupo kwao na famili zao. Mimi nalea wajukuu tu wakija likizo. Hivyo ni faraja sana kwangu.
Namshukuru Mungu kwa kunijaalia uzee mzuri, japo haikuwa rahisi mpaka kufikia hapa nilipo.
Muwe na Jumapili njema 👐👐👐👐👐
=========================
Edit: wengi wenu mmeniuliza ni vitega uchumi gani nimewekeza
Jibu langu ni kuwa ni hivi hivi vya kawaida hamna biashara mpya duniani hapa
1. Kilimo cha mboga mboga
2. Ufugaji wa ngombe na nguruwe pamoja na kuviuza butcher (supplier)
3. Appartment kadhaa nzuri, sina nyingi
4. Savings kwenye bank yenye interest nzuri
5. Uwakala wa mpesa
Basi ni hivi tu ndo navyo tegemea,
Hapo naweza kukuachia wewe kufuatilia mwenyewe, Asante