Nguvu nilizowekeza kwenye ujana wangu nakula Matunda yake sasa

Nguvu nilizowekeza kwenye ujana wangu nakula Matunda yake sasa

Mwisho wa siku yote ni kujilisha upepo,usijifanye bingwa wa ushauri kila mtu ana maisha yake.Usije ukajiona mjanja sanaaa.
 
Usihofu hujanikwaza hata

Changamoto kuu niliyoipata ni kupata ule ujasiri wa uthubutu basi, kabla ya hapo nilikuwa muoga sana ila ile courage ndo ilikuwa msaada wangu

Nilianza na appartment kwanza mkuu, na savings

Ila 2016 nilivyostaafu nilikuwa na muda mwingi ndo nikajiingiza kwenye (kilimo cha mboga, ufugaji,)

Hapa nilitumia miaka 3 mpaka kuwa stable changamoto kuu ni usimamizi bora, na inabidi uwe na elimu nzuri kuhusu hili suala,

Sema haikunipa shida maana ilikuwa small scale hivyo ilikuwa rahisi ku menage
Hongera sana kwani JF ni shule inayotembea
 
-Mashamba(kilimo cha mbogamboga)
-ufugaji wa ngombe na nguruwe(butcher) supplier
-appartment kadhaa.
-bank savings.
-mpesa wakala,,,, hivyo tu
Vizuri saana mzee,watumishi siku hizi tunawaza kuchukua mkopo na kujenga kijumba kisicho isha na kumiliki IST. Tunasubir kustaafu. Unatushaurije?
 
Asante kwa maoni yako,

Ila nilishaeleza hapo awali vitega uchumi vizuri ni
-shamba la mboga
-ufugaji wa ngombe, nguruwe
-appartment kadhaa
-wakala mpesa
- savings kwenye bank yenye interest nzuri

Hivi havijawahi kunipa stress hata kidogo mkuu
Hapo kwenye uwakala changamoto hakuna?
 
Salaam kwenu wote,

Mimi ni mgeni humu ila ningependa kushare kisa kidogo cha maisha ya ujana wangu. Nimezaliwa 1953.

Kusema kweli mwenyezi Mungu alinijalia sana mimi, kwenye elimu ya darasani nilikuwa vizuri sana nikafanikiwa kumaliza chuo mwaka X kipindi hicho. Bahati nzuri nikapata kazi yangu kwenye kampuni Y, nilifanya kwa miaka 3 kabla ya kuhamishwa kupelekwa kwenye kituo kingine. ambapo nilipata mshahara na marupu marupu matamu kweli. Nilitumikia hiyo nafasi kwa miaka 35.

Mpaka nilivyostaafu rasmi 2016, namshukuru Mungu sana kwa kunijaalia akili ya kuona mbele, na kuweza kupanga hatma ya maisha yangu.

Niliweza kujiingiza kwenye kuwekeza kwenye vitega uchumi mbalimbali ambavyo ndo vinanilea sasa hivi.

Nawashauri vijana mtakaosoma hiki kisa tafadhali tafadhali tumieni muda wenu vizuri, msije mkajuta baadae mkiona mzee ni masikini jua haikuja hivi hivi, likewise mkiona mzee ni tajiri jua ni tu watu walijitoa haswa haswa,

Zingatia: Tumieni ujana wenu vizuri, narudia tena tumieni ujana wenu
Vizuri, narudia tumieni ujana wenu vizuri. Msije Mkajuta kwenye uzee wenu, maana muda utakuwa umekutupa mkono na ndipo maradhi yatakavyoanza kukushambulia.

Kwangu mimi navyoona umri wa kuweka nguvu ni (25-55) hapa ndo inabidi ufanye uwekezaji mkubwa na uchakarike sana.

Lakini kumbukeni pia kumtanguliza Mungu kwenye kila mfanyacho ili azidi kuwabariki. Mimi namshukuru Mungu wanangu 4 wapo vizuri kila mtu yupo kwao na famili zao. Mimi nalea wajukuu tu wakija likizo. Hivyo ni faraja sana kwangu.

Namshukuru Mungu kwa kunijaalia uzee mzuri, japo haikuwa rahisi mpaka kufikia hapa nilipo.

Muwe na Jumapili njema 👐👐👐👐👐
Asante, swali je Ulikuwa unalewa pombe?

Je hukuwa unahonga wanawake au hukuwa na michepuko??

Mwenzi wako alikiwa mama wa nyumbani au mfanyakazi/mfanyabiashara? Katika kupangilia maisha yenu mkeo alishughulika na jambo lepi

Ukijibu nanufafanuzi utasaidia wengi humu
 
Sasa tufanye kweli wewe ni mzee, maisha umeyala mda gani sasa??!!

Au hiyo akiba yako umehisi itakubakisha milele[emoji23][emoji23]
Life is good and better u enjoy life when u are youth
Maisha ya uzee ni mafupi sana na changamoto zake ni nyingi lakini ni maamuzi yako tu ww ule bata ujanani halafu usumbue nduguzo au uwekeze ujanani na ule bata uzeeni
 
Maisha ya uzee ni mafupi sana na changamoto zake ni nyingi lakini ni maamuzi yako tu ww ule bata ujanani halafu usumbue nduguzo au uwekeze ujanani na ule bata uzeeni
Utakulaje bata uzeeni wakati kama ulivyosema maisha ya uzee ni mafupi pia yana changamoto nying??!!

Uzee ni kama vile mlango wa kutokea[emoji24][emoji24]
Na utoto ni mlango wa kuingilia but u can enjoy life at the peak when u are youth
 
Asante sana kwa ushauri mzuri mkuu, nimepokea hiyo naweka juhudi zangu katika kuwekeza
 
Usifanye hivyo mkuu, mimi nilijenga 2005 nikiwa na miaka 52, sikuwahi kabisa kujenga nilinunua gari nikiwa na 55,

Hivyo vilikuja baadae, nilijibana sana, mkuu,
Ahsante sana babu.
 
Mzee ungeelekeza vizuri namna ulivyoanza kuwekeza na sehemu ulizowekeza uzi wako ungekuwa na manufaa sana Kwa wasomaji, ila Kwa style hii uliyokuja nayo uzi wako umejaa majigambo na mipasho.

Uwe na j.pili njema nawe pia
Mkuu mbona babu/baba yetu kaongea vizuri tu.Hakuna majigambo bali angalia msisitizo wake kwenye kuchacharika then siyo lazima aseme uwekeze wapi.Wewe fanya utafiti wako upate mahala pazuri pa kuwekeza.
 
Sometimes unakuwa na akili sana mshamba_hachekwi we Lovie Lady kamata huyu kijana mtafika mbali sana pamoja😅 usije kusema sikukwambia
rabbitus ndio nini kuchange username sasa?😔😔😔 unadhani utanikimbia🤣👋 af lile jambo langu umelipotezea eeh🤣🤣🤣👋

Uyu mshamba_hachekwi nishamwambia atafute kwanza💰💰💰💰💰af tutazungumza lugha moja🤣🤣🤣👋
 
Back
Top Bottom