Nguvu wanayotumia vijana kwenye Simba na Yanga wangeitumia kushinikiza serikali kufufua viwanda vyote vilivyokufa nchi ingesonga mbele

Nguvu wanayotumia vijana kwenye Simba na Yanga wangeitumia kushinikiza serikali kufufua viwanda vyote vilivyokufa nchi ingesonga mbele

Mwamuzi wa Tanzania

JF-Expert Member
Joined
Apr 7, 2020
Posts
15,486
Reaction score
45,256
Maisha si bahati, maisha ni mikakati thabiti na mipango. Ingawa mara chache maisha huweza kuwa bahati. Binafsi nasema kuwa mtu yeyote anayeishi kwa kusubiri bahati imwangukie huyo ni tahira.

Vijana maisha si bahati, sasa wasomi wa vyuo vikuu wako wengi, vya kati pia wako wengi na vyuo vya chini hivi vya maghorofani ndo usiseme.

Je, tuishi kwa kusubiri mkeka wa kamari utiki?
Je, tuishi kwa kutegemea ajira from unknown source?

Vijana hebu ishinikizeni Serikali huenda itawasikia. Serikali ina mambo mengi hivyo kwenye mijadala mbalimbali msiache kuishinikiza iwajengee viwanda na kufufua viwanda vyote vilivyokufa hapa nchini.

Kama mwaka 1980 Serikali ilikuwa na viwanda kila mkoa sasa hivi hamna viwanda vya Serikali. Bahati mbaya hata vilivyotaifishwa sasa vimegeuka magodown ya wahindi na magofu.
Kazi kuomba connection za video za ngono tu mambo ya msingi wanakaa pembeni.

Tunarudi nyuma kama Taifa.
Simba na Yanga viwe ajenda baada ya kazi na si ajenda kuu.
 
Ujumbe wa maana sana huu, nguvu na akili zao zipo kwenye Simba na Yanga, Diamond na Harmonizer, mapenzi na pombe
 
Kama kina JokaKuu tunapenda kuona tatizo liko Kule SI sisi.

Kwani wewe na nani mmefanya nini wapi?
 
Afu ungekua wazee ndio wengi kwenye mambo ya Simba na Yanga ungepiga kimya tu

Vijana wa Tanzania msitafute kichaka. Mmelala tu kwa malezi yenu msisingizie Yanga wala Simba
 
Kuna siku nikawaambia hivyo kwenye daladala,aisee walinijia juu balaa kuwa nisiwapangie wao wana kazi zao na wanajishughulisha.Tanzania ina vijana wa hovyo sana
 
Afu ungekua wazee ndio wengi kwenye mambo ya Simba na Yanga ungepiga kimya tu

Vijana wa Tz msitafute kichaka. Mmelala tu kwa malezi yenu msisingizie Yanga wala Simba
Hao wazee muda wao ushaisha.
Pia hao wazee ni vijana wa miaka ya 1990 na 2000 hivyo nao walikwepa wajibu wao wa kudai viwanda vya taifa
 
Maisha si bahati, maisha ni mikakati thabiti na Miata. Ingawa mara chache maisha huweza kuwa bahati. Binafsi nasema kuwa mtu yeyote anayeishi kwa kusubiri bahati imwangukie huyo ni tahira...
Mkuu,

Serikali ifufue viwanda?? Nilidhani hoja iwe private sector ndiyo iongoze njia na serikali itengeneze mazingira wezeshi ya viwanda hivyo kufanya kazi kwa kuwa na sera zinazotabirika na kutengeneza mazingira wezeshi ya bashara nchini.

Vijana tukiendelea kuilaumu serikali wa kila kitu tutabaki kama tulivyo na hakika tutakuwa mzigo kwa taifa. ( ndiyo maana Marekani waliwahi kuambiwa kabla hujauliza taifa limekufanyia nini jiulize wewe umelifanyia nini taifa?)

Vijana tunatakiwa kufanya kazi kwa nguvu juhudi na maarifa. “Over” kama tunataka kuikomboa nchi yetu. hakuna shortcut.

Uzuri ni kuwa, Tanzania ina un utilized potential kubwa, mtu yeyote akiweka jitihada probability ya kufanikiwa ni kubwa kuliko ya kufeli.
 
Maisha si bahati, maisha ni mikakati thabiti na mipango. Ingawa mara chache maisha huweza kuwa bahati. Binafsi nasema kuwa mtu yeyote anayeishi kwa kusubiri bahati imwangukie huyo ni tahira...
Elimu, elimu elimu!!! Yaani ni hasara kubwa sana, wao habari za siasa wanakwambia hawazitaki, ambazo ndio zinaamua hatima yao, wao muda wote ni simba yanga,
 
Kwenye Simba na Yanga wako tayari kupugana
Ni hasara kubwa sana, na ccm ndio imeshagundua hilo, sasa hivi mpira wa nchi hii ni full siasa!! Kuna bwege mmoja nimemuona zanzibar uwanjani ameshika kikapu kimeandikwa MWINYI MITANO TENA!!,
 
Wewe ambaye hushabikii simba na yanga umefanya nini unataka nani akupambanie pambana na maisha Yako wenzio tunashabikia simba na yanga na pesa tunazo njaa zako peleka huko
 
Back
Top Bottom