Nguvu ya CHADEMA imeonekana nchi nzima na hofu ya vyombo vya dola ni kubwa sana. Je huu ni ushindi kabla ya mechi?

Nguvu ya CHADEMA imeonekana nchi nzima na hofu ya vyombo vya dola ni kubwa sana. Je huu ni ushindi kabla ya mechi?

Tangu CHADEMA washikilie msimamo wa kuandamana tar. 23.09.2024, askari wamepata taabu sana. Wamekuwa wakizunguka huku na huko ili kutuliza joto la maandamano.
Pole sana askari wetu.
 
Safi kabisa walikuwa wanakaa tu hawafanyi nazoezi ya utayari hata nchi ikipatwa na taahuruki wawe wanaweza kutulinda sisi wananchi wa kawaida .
 
Tangu CHADEMA washikilie msimamo wa kuandamana tar. 23.09.2024, askari wamepata taabu sana. Wamekuwa wakizunguka huku na huko ili kutuliza joto la maandamano.
Pole sana askari wetu.
Ni mbinu kubwa sana CDM wamecheza hapo.
 
Halafu hawatalipwa watakuja hapa kulalamika posho zao wamekula wakubwa kama kawa! Kama ule mfuko wao ulikufa kifo cha kawaida na yakaisha kama kawaida kibongobongo
 
Nimekumbuka UKUTA.. afu nayo ilikuwa september. Wale wazee wa rohoni Mshana Jr na Rabbon hii inamaana gani kwa taifa letu.

Ukuta majeshi yote yalijitokeza kufanya usafi, hawa sasa wapo doria tu.
Tukifiata callendar OG ya Israel, mwaka wa uchaguzi 2025 uneshaingia.

Iwapo CCM itashindwa kuamua juu ya mtu sahihi wa kugombea nafasi nyeti Hasa Ile ya juu,

Upinzani utafaidika ikiwa nao wataungana na kupata mtu sahihi.

Tusubiri.
 
ishakuingia tayari lazima uweweseke šŸ˜€ ...pole
Unapambana kujibu lakini hujui unajibu nini. Hata kama ni roboti nakushauri kunywa maji upumzishe komwe kesho nayo ni siku utaendelea kufanya ka i yakošŸ˜…šŸ˜…šŸ˜…
 
Kama ni ushindi, basi CHADEMA walishashinda mechi kabla hata ya mechi yenyewe kuchezwa. Hii mbinu ya kimapambano ni kubwa sana na haijapata kutokea hapa Tanzania.

Nimeona polisi kila kona ya jiji na unaweza ukafikiri kuna shambulio la kijeshi linasubiriwa kutoka majeshi ya nchi jirani au kutoka taifa kubwa duniani. Ni wazi kabisa kuwa hofu ya jeshi la polisi na uongozi wa nchi hii kwa CHADEMA ni kubwa sana.

Tafsiri yake:
1. CHADEMA inaogopwa sana kutokana na kuwa na nguvu kubwa ya ushawishi
2. Watanzania wanaosemwa kuwa wapole na watulivu ukweli ni kwamba wanaogopwa kuliko majeshi ya nchi jirani
3. Viongozi wetu wapo tayari kutumia nguvu kupitiliza na hawako tayari kufanya mazungumzo na kusikiliza haja za wananchi
4. Watanzania wakiwa na umoja wanatatua matatizo sugu mara moja
5. Serikali ya Samia imeendelea kujitangaza kwa jumuiya ya kimataifa kama serikali yenye kutumia nguvu kupindukia na hairuhusu njia ya mazungumzo

Hitimisho
CHADEMA wameonesha nguvu kubwa kama chama cha upinzani kuweza kutetemesha vyombo vya dola na kwamba viongozi wa CHADEMA na CHADEMA kama taasisi ya kisiasa wana nguvu na ushawishi mkubwa sana katika nchi hii. Hata kama maandamano hayatafanyika, CHADEMA tayari wameshafikisha ujumbe, na kazi sasa ni kuendelea kushinikiza hadi hali ya uongozi wa nchi hii ibadilike.
Kenge we!
 
Haya endeleeni kufanya maandamano wakati huo walioandaa maandamano haya wamejifungia manyumbani kwao.
 
Yaani tunataka hao polisi wakaa dar week nzima
 
Ni hivi, Chadema ilishaimaliza ccm miaka mingi mno! Sasa inamalizia kupambana na vibaraka wa ccm ambao ni Polisi
Binafsi hili la maandamano lishapita kwa mafanikio makubwa kwa CHADEMA.
Nasubiri tu wamalize kazi na "Serikali za Mitaa"; na hiyo 2025.

Chama ni lazima kielekeze nguvu zote katika malengo hayo.
 
Huu ndio ukubwa wa Chadema ambao vijana wengi Mamluki hawakuujua.

Sasa unapaswa kujiuliza kulikoni jambo hili kufanyika kabla ya maombolezo ya Kitaifa?
 
Back
Top Bottom