Nguvu ya kimkakati ya nyuklia ya China ni dhamana thabiti ya amani ya kikanda na dunia

Nguvu ya kimkakati ya nyuklia ya China ni dhamana thabiti ya amani ya kikanda na dunia

Yoyo Zhou

Senior Member
Joined
Jun 16, 2020
Posts
199
Reaction score
322
Jeshi la Majini la China hivi karibuni lilipata mafaniko katika jaribio la kombora jipya la kimkakati lililorushwa chini ya maji katika Bahari ya Pasifiki. Hii ni hatua nyingine muhimu katika maendeleo ya nguvu ya nyuklia ya kimkakati ya China, kufuatia jaribio la kombora la kuvuka bara lililorushwa ardhini mwaka 2024.

Kombora hilo lililojaribiwa linaaminika kuwa la JL-3, lenye umbali wa zaidi ya kilomita 10,000 na uwezo wa kufika mahali popote duniani. Jambo linalofuatiliwa zaidi ni jukwaa lake la kurushia—nyambizi ya kimkakati ya nyuklia. Umuhimu wake ni kwamba hakuna nchi inayoweza kuharibu kabisa uwezo wa China wa kulipiza kisasi shambulio la nyuklia, na kuimarishwa kwa uwezo wake wa nyuklia wa shambulio la pili kwa China si tishio, bali ni hatua ya kuzuia vita vya nyuklia.

Kujizuia kwa China katika sera yake ya nyuklia ni kwa kipekee miongoni mwa nchi zenye nguvu za nyuklia duniani. Kama nchi pekee yenye silaha za nyuklia ambayo imeahidi “kutotumia silaha za nyuklia kwanza, na kutotumia silaha za nyukilia dhidi ya nchi zisizo na silaha hizo”, China imekuwa ikidumisha nguvu zake za nyuklia katika kiwango cha chini kinachohitajika kwa usalama wa taifa. China kuendeleza nguvu za nyuklia si kwa ajili ya kukandamiza nchi nyingine, bali ni kuhakikisha haitatishiwa na nchi nyingine zenye silaha hizo.

Katika miaka ya hivi karibuni, kanda ya Asia-Pasifiki imedumisha amani na maendeleo. Wakati huohuo, changamoto na matishio dhidi ya amani pia haviwezi kupuuzwa. Katika Mlango-Bahari wa Taiwan, nguvu za nje zinaendelea kushirikiana na kundi la ufarakanishaji la Taiwan. Katika Bahari ya Kusini ya China, nguvu za nje zinaendelea kuongeza mvutano. Mfumo wa OKUS una hatari ya kuenea kwa silaha za nyuklia. Japan imevunja kanuni ya kujilinda tu, na kujaribu kumiliki silaha za nyuklia. Chanzo cha changamoto na matishio hayo ni kwamba baadhi ya nchi zinaamini nguvu inaweza kuilazimisha China kufanya lolote zinazotaka. Kuimarishwa kwa uwezo wa kimkakati wa China ni kuvunja ndoto hii na kudumisha amani na utulivu wa kikanda.

Historia imethibitisha kwamba wakati China ilikuwa maskini na dhaifu, kanda ya Asia-Pasifiki na dunia haikupata amani. Kinyume chake, udhaifu wa China mara kwa mara ulisababisha uvamizi na hali ya kutokuwa na utulivu wa kikanda. Hivi leo, azimio la China la kujiendeleza kwa njia ya amani halibadiliki, na uwezo wake unaozidi wa kujilinda unatoa dhamana thabiti kwa amani ya kikanda.

Mafanikio ya jaribio la kombora la kimkakati la China lililorushwa kwa nyambizi yameleta ishara wazi kwa dunia: China yenye uwezo mkubwa wa kujilinda ni nguzo muhimu ya utulivu wa kimkakati katika kanda ya Asia-Pasifiki na hata dunia nzima.

Katika enzi ya nyuklia, kitu hatari zaidi si uwezo wa kujilinda, bali ni umwamba usiodhibitiwa. Kinachofanywa na China ni kuimarisha msingi wa amani na utulivu vya kikanda na kimataifa

1783409538538.png




==========

The Chinese People's Liberation Army (PLA) Navy on Monday successfully conducted the test launch of a strategic missile by a submarine.

The PLA Navy said that one strategic nuclear submarine of the navy successfully launched a strategic missile carrying a dummy warhead toward relevant high seas of the Pacific Ocean at 12:01 p.m., which landed precisely within the designated waters.

The test launch is a routine arrangement of the annual training of the PLA Navy, the navy said, adding that the Chinese side has already notified relevant countries in advance.

The test launch complies with international law and international practice, and is not directed at any specific country or target, the navy said.

Source: Ministry of national defence People's republic of China
 
Back
Top Bottom