Nguvu ya matajiri itakapoanza kuchukua nafasi yake, kilio cha wanyonge kumlilia Dkt. Magufuli itazidi kusikika na wa kuwazuia hatakuwepo

Nguvu ya matajiri itakapoanza kuchukua nafasi yake, kilio cha wanyonge kumlilia Dkt. Magufuli itazidi kusikika na wa kuwazuia hatakuwepo

Ndiyo!
Nguvu ya matajiri ikiilemea serikali hii mpya, wanyonge watalitaja Jina la JPM Kwa uchungu mkubwa na hakuna atakayewazuia

Pale rushwa itakapowafanya wanyonge, wamachinga, wamama ntilie, bodaboda, bajaji n.k ambao idadi Yao ni kubwa mno Kwa sasa katika nchi hii kuanza kufukuzwa kwenye maeneo Yao ya kazi aliyokuwa amewaruhusu Jembe Lao JPM R.I.P kufanyia biashara zao,

Ndipo sauti zao zitapazwa wakimlilia Kwa upya tena JPM na Jina lake litatawala Kwa upya kwenye vyombo mbalimbali za habari kote Tanzania na hata duniani

Pale majambazi ya kupora muda wowote yatakapojitokeza iwapo serikali hii haitasimama Kiume, sauti za wananchi wengi watakapoanza kumlilia JPM Kwa upya na watu watasema ni Bora alipokuwepo Jembe

Pale matajiri wakubwa watakapoizidi serikali ujanja aidha Kwa rushwa Ili wasilipe Kodi na Kodi nyingi kuelekezwa Kwa wafanya biashara wadogo wadogo, watu hawa wataanza kumlilia upya Jembe lao, watasema, ni Kwa sababu hayupo JPM ndio Maana wananyanyaswa?

Ingawa Nina Imani kuuubwa Sana na Raisi wetu Madame SHS, kwamba ni jemedali na jasiri asiyeogopa na asiyerudishwa nyuma, Kwa kuwa pia ufanisi wa serikali hii Naamini ni Kwa sababu mama alisimama nyuma yake kuhakikisha tunakuwa hapa tulipo

Mbali na hayo, Sisi ni binadamu tunaweza kujisahau yakarudi hayo na yakawa sababu ya Jina la Jembe kutajwa kila pahala kuwa yeye alikuwa ndiye na kimvuli chake kutawala midomo mwa watu wanyonge

Mh Raisi Madame Samia suluhu Hasan Tunakuombea, kwani tunajua ilivyongumu kuongoza nchi bila ya Mungu Kusimama Mbele yako

Wasalaam
Hao wanyonge siku zote, miaka yote 6 wameshindwa kujiondoa unyonge baada ya kupata mtetezi ???
 
Ss tunajenga barabara za nn kama wamachinga watazifunga na bidhaa zao? Tufute basi biashara za aina zote tuwe na wamachinga tu. Magari nayo yaondolewe watu wauze vitu kwenye lami.

UTARATIBU NI JAMBO ZURI, HAKUNA CHA MATAJIRI WALA NN NI UTARATIBU.
 
Aaah wapi labda wanufaika wa upigaji kama nyie.lkn ni neema tele tu.
Waislamu awajawahi tulaza njaa soma historia
Kuna wakristo roho mbaya na waislamu roho mbaya wapo, hivi Kwa nini tusitumie kutaja Tu utanzania na sio udini mkuu, anayeongoza Kwa sasa ni mtanzania na sio kiongozi wa waislamu mkuu

Ongeza hekima
 
Na hiyo ndio shida aliyotuachia, alitaka kufanya kila kitu mwenyewe badala ya mfumo ndio maana tunaona bila yeye hakuna kitakachofanyika, akalazimisha tuamini hivyo na wengine mukaamini, sikatai ukali wake kuna sehemu ulisaidia lakini kuna sehemu ulivurunda, tumuombee mama ajenge mfumo mzuri wa kuwajibishana pale kwenye makosa, Nchi iende kama Nchi na sio kwa matakwa ya mtu.
 
Ss tunajenga barabara za nn kama wamachinga watazifunga na bidhaa zao? Tufute basi biashara za aina zote tuwe na wamachinga tu. Magari nayo yaondolewe watu wauze vitu kwenye lami.

UTARATIBU NI JAMBO ZURI, HAKUNA CHA MATAJIRI WALA NN NI UTARATIBU.
umewaza kipumbavu sana,tathmini umri wako na mawazo uliyotoa kisha kajifungie chumbani peke yako uanze kumlilia Mungu wako.
 
Mawazo yako ni mazuri Ila nilichokiandika rudia tena Kusoma utaelewa tu mkuu
Nimesoma kila neno, na Ndio maana nikaweka Rushwa na uonevu hapo kwani hivi vitu ndivyo vinaumiza watu bila kujali tajiri au masikini, Nchi haindeshwi na mtu bali sheria nzuri,ili Nchi iongozwe kwa mafanikio unahitaji taasisi imara na zinazojitegemea kama Mahakana nk. na hili ndio tatizo kubwa ktk nchi zinazoendelea, viongozi hawataki sheria nzuri, tasisi imara wala hata kufuata sheria walizoziweka wenyewe na ndio chanzo cha matatizo
 
umewaza kipumbavu sana,tathmini umri wako na mawazo uliyotoa kisha kajifungie chumbani peke yako uanze kumlilia Mungu wako.
Hizo hisia zako na ubongo wako unavyokuelekeza aina ya matamshi si tatizo langu ni lako. Mm yangu ni kuwa Utaratibu ufuatwe.

Barabara ni za magari, bajaji, pkpk,baiskeli na watembea kwa miguu.

Machinga wawe na maeneo yao. Kodi nyingi sana imepotea kwa watu kufunga maduka na kuwapa machinga wakajaze vitu barabarani.

TUFUATE UTARATIBU NI MATUMAINI YANGU HILI LITAFANYIWA KAZI.
 
Mtajuta nyinyi parasites mlio endesha maisha yenu kwa miaka yote mitano huku mkimtegemea huyo magufuli kwa kila kitu! Sasa kama sisi watumishi wa umma tutajuta kwa lipi! Si maajabu haya!!
Hii inahusu wanyonge Kaka, sasa watumishi wa hao wapi na wapi
 
Siasa ya ujamaa ni kufuga ujinga tu waacheni watu wapige kazi
Wafanya biashara waachwe wakuze Uchumi wetu tuache ujinga wa kwamba Wafanyabiashara ni maadui wa Muungano kama tulivyokaririshwa
 
Siasa ya ujamaa ni kufuga ujinga tu waacheni watu wapige kazi
Wafanya biashara waachwe wakuze Uchumi wetu tuache ujinga wa kwamba Wafanyabiashara ni maadui wa Muungano kama tulivyokaririshwa
Ujamaa mara nyingi watu ni masikini kiongozi ndo tajiri wa kutupwa kisha anahudumia masikini. Nchi za kijamaa kuwa mjasiriamali mwenye mafanikio ni tatizo.

Katika ujamaa kiongozi ni mungu flani hivi maana ndo ana kila kitu.
 
Well said brother.Umuhimu wa mtu huthibitika baada ya kufa. Waliokuwa wanashinda mitandaoni wakitukana na kudhihaki uongozi wa JPM sasa wataanza kumkumbuka kinafiki.

Uongozi ni kuwawezesha watu kwa kuwawekea miundombinu ili iwasaidie katika shughuli zao,na Magufuli alifanikiwa kwenye hilo.
Pamoja Sana mkuu
 
Hakuna mjadala wamachinga wanatakiwa kytafutiwa maeneo ya kufanyia biashara sio barabara zinazojengwa na walipa kodi fullstop.

...umekuwa mmachinga miaka mi5 hujafanikiwa kubuni kitu hata ukipewa 100 hutaweza,mmachinga gani ana msingi wa milioni 5!!
Hawa watu wameharibu sana huu mji, posta sasa hivi ni chafu sababu ya wamachinga kila eneo na kariakoo nako hakupitiki barabara zote wapo wao tu. Mlipa kodi huna thamani mbele ya mmachinga sasa hivi.
 
or78yhntaij21.png

Nimeona nianze na Mimi kumlilia magufuli
 
Pombe Magufuli hajawai kumtetea mnyonge yeyote bali alitumia wanyonge kujijenga kiaiasa. Kama ni kutetea wanyonge alipaswa kuwafidia wale wananchi wa Kimara- Kibaha aliowavunjia nyumba kupisha barabara.

Angekuwa mtetezi wa wanyonge asingetumia mabilioni kujenga Chato kijijini kwao miundombinu inayostahili kuwa makao makuu ya Mkoa wa Geita. Huku watoto wa Watanzania wanasoma kwenye kwenye miti na wengine hawana madawati. Au kununua madreamliner wakati 80% ya Watanzania hawapati maji safi.

Magufuli ilikuwa ni LAANA, na Mungu ametuepushia, tujenge Tanzania yetu nzuri isiyo na ubaguzi wa kiitikadi, kikabila na kikanda.
Aiseee thread hii imekaa ki February February yani
 
Back
Top Bottom