Nguvu ya matajiri itakapoanza kuchukua nafasi yake, kilio cha wanyonge kumlilia Dkt. Magufuli itazidi kusikika na wa kuwazuia hatakuwepo

Hao wanyonge siku zote, miaka yote 6 wameshindwa kujiondoa unyonge baada ya kupata mtetezi ???
 
Ss tunajenga barabara za nn kama wamachinga watazifunga na bidhaa zao? Tufute basi biashara za aina zote tuwe na wamachinga tu. Magari nayo yaondolewe watu wauze vitu kwenye lami.

UTARATIBU NI JAMBO ZURI, HAKUNA CHA MATAJIRI WALA NN NI UTARATIBU.
 
Aaah wapi labda wanufaika wa upigaji kama nyie.lkn ni neema tele tu.
Waislamu awajawahi tulaza njaa soma historia
Kuna wakristo roho mbaya na waislamu roho mbaya wapo, hivi Kwa nini tusitumie kutaja Tu utanzania na sio udini mkuu, anayeongoza Kwa sasa ni mtanzania na sio kiongozi wa waislamu mkuu

Ongeza hekima
 
Na hiyo ndio shida aliyotuachia, alitaka kufanya kila kitu mwenyewe badala ya mfumo ndio maana tunaona bila yeye hakuna kitakachofanyika, akalazimisha tuamini hivyo na wengine mukaamini, sikatai ukali wake kuna sehemu ulisaidia lakini kuna sehemu ulivurunda, tumuombee mama ajenge mfumo mzuri wa kuwajibishana pale kwenye makosa, Nchi iende kama Nchi na sio kwa matakwa ya mtu.
 
Ss tunajenga barabara za nn kama wamachinga watazifunga na bidhaa zao? Tufute basi biashara za aina zote tuwe na wamachinga tu. Magari nayo yaondolewe watu wauze vitu kwenye lami.

UTARATIBU NI JAMBO ZURI, HAKUNA CHA MATAJIRI WALA NN NI UTARATIBU.
umewaza kipumbavu sana,tathmini umri wako na mawazo uliyotoa kisha kajifungie chumbani peke yako uanze kumlilia Mungu wako.
 
Mawazo yako ni mazuri Ila nilichokiandika rudia tena Kusoma utaelewa tu mkuu
Nimesoma kila neno, na Ndio maana nikaweka Rushwa na uonevu hapo kwani hivi vitu ndivyo vinaumiza watu bila kujali tajiri au masikini, Nchi haindeshwi na mtu bali sheria nzuri,ili Nchi iongozwe kwa mafanikio unahitaji taasisi imara na zinazojitegemea kama Mahakana nk. na hili ndio tatizo kubwa ktk nchi zinazoendelea, viongozi hawataki sheria nzuri, tasisi imara wala hata kufuata sheria walizoziweka wenyewe na ndio chanzo cha matatizo
 
umewaza kipumbavu sana,tathmini umri wako na mawazo uliyotoa kisha kajifungie chumbani peke yako uanze kumlilia Mungu wako.
Hizo hisia zako na ubongo wako unavyokuelekeza aina ya matamshi si tatizo langu ni lako. Mm yangu ni kuwa Utaratibu ufuatwe.

Barabara ni za magari, bajaji, pkpk,baiskeli na watembea kwa miguu.

Machinga wawe na maeneo yao. Kodi nyingi sana imepotea kwa watu kufunga maduka na kuwapa machinga wakajaze vitu barabarani.

TUFUATE UTARATIBU NI MATUMAINI YANGU HILI LITAFANYIWA KAZI.
 
Mtajuta nyinyi parasites mlio endesha maisha yenu kwa miaka yote mitano huku mkimtegemea huyo magufuli kwa kila kitu! Sasa kama sisi watumishi wa umma tutajuta kwa lipi! Si maajabu haya!!
Hii inahusu wanyonge Kaka, sasa watumishi wa hao wapi na wapi
 
Siasa ya ujamaa ni kufuga ujinga tu waacheni watu wapige kazi
Wafanya biashara waachwe wakuze Uchumi wetu tuache ujinga wa kwamba Wafanyabiashara ni maadui wa Muungano kama tulivyokaririshwa
 
Siasa ya ujamaa ni kufuga ujinga tu waacheni watu wapige kazi
Wafanya biashara waachwe wakuze Uchumi wetu tuache ujinga wa kwamba Wafanyabiashara ni maadui wa Muungano kama tulivyokaririshwa
Ujamaa mara nyingi watu ni masikini kiongozi ndo tajiri wa kutupwa kisha anahudumia masikini. Nchi za kijamaa kuwa mjasiriamali mwenye mafanikio ni tatizo.

Katika ujamaa kiongozi ni mungu flani hivi maana ndo ana kila kitu.
 
Pamoja Sana mkuu
 
Hakuna mjadala wamachinga wanatakiwa kytafutiwa maeneo ya kufanyia biashara sio barabara zinazojengwa na walipa kodi fullstop.

...umekuwa mmachinga miaka mi5 hujafanikiwa kubuni kitu hata ukipewa 100 hutaweza,mmachinga gani ana msingi wa milioni 5!!
Hawa watu wameharibu sana huu mji, posta sasa hivi ni chafu sababu ya wamachinga kila eneo na kariakoo nako hakupitiki barabara zote wapo wao tu. Mlipa kodi huna thamani mbele ya mmachinga sasa hivi.
 
Aiseee thread hii imekaa ki February February yani
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…