Nguvu ya matajiri itakapoanza kuchukua nafasi yake, kilio cha wanyonge kumlilia Dkt. Magufuli itazidi kusikika na wa kuwazuia hatakuwepo

Tumshukuru sana Mungu kwa zawadi ya uhai wa John Pombe Joseph Magufuli kwa nchi yetu. Ametutoa pagumu sana, ametuthubitishia yaliyoambiwa hayawezekani yanawezekana kwa vitendo

Ametuachia viongozi makini aliowapika kuwa wazalendo kama yeye mwenyewe na ameacha wananchi wengi walio maskini wakiwa na cha kujivunia kwa nchi yao

Ameiheshimisha Tanzania duniani kote kwa kuondoa uhuru wa bendera na kurudisha misingi ya uhuru halisi

Ametuachia serikali makini chini ya aliyekua msaidizi wake makini Rais Samia Suluhu Hassan na wasaidizi wake wote

Ametuachia jamhuri ya muungano wa Tanzania iliyo imara, bunge imara, mahakama imara na jeshi imara.

Tumuombe Rais wetu Samia Suluhu Hassan aendeleze yale waliyoyaanza pamoja, na Mungu aendelee kumjaza hekma, ampe afya ya mwili, roho na akili katika kulitumikia taifa hili

Rest well our hero President John Pombe Magufuli 💔😭🙏
 
Jana watu wamepiga kontena tatu za futi 20.
Hata mzee baba ajazikwa wapigaji washaanza yao"kudadeki"
Aisee!

Maboda boda huku tayari washaanza kumtaja Mzee wakisema, mnatufanyia hivi Kwa sababu Jembe hayupo??
 
Kama una imani na Mama Samia Suluhu Hassan basi uzi wako hauna maana.
 
Acha siasa ni muda wa maombolezo,au unataka waishi kama mashetani ili furaha yako ipatikane.acha ubinafsi.
 
Acha siasa ni muda wa maombolezo,au unataka waishi kama mashetani ili furaha yako ipatikane.acha ubinafsi.
Kunywa maji kidogo mkuu Ili hasira ishuke kidogo, si Kwa hasira hizo aisee
 
Muda wa kutafuta huruma huu.Ila kuna mambo makubwa sana yalitokea huko nyuma kuna namna tunauasahau.
Wacheni kazi ya Mungu iheshimiwe na kila mwanadamu.

Dumisha upendo popote ulipo hapa dunia..acha tabia za kishirikina na kujigawa gawa ndani ya jamii.
 
Aaah wapi labda wanufaika wa upigaji kama nyie.lkn ni neema tele tu.
Waislamu awajawahi tulaza njaa soma historia
Hili ni tatizo lingine kwa Taifa letu,yupo mwenzako mmoja alitaka kunisababishia BAN jana kwa ujinga huu huu yeye anauliza eti “mbona Tanzania Marais Wakristo hawakai?”,kwamba wasife?wewe unasema Waislam hawatulazi njaa....

Kwa akili zako unaamini ipo siku muislam mwenzako Samia atakuletea mkate mezani kwako?hii mentality mnaitoa wapi nyie na nyie ndo wale hata kiongozi awe mbaya kiasi gani kwa sababu ni dini yako/kabila lako basi mnamuona huyo huyo na mapungufu yake yote anafaa,mbona vichwa vyenu hamvitumii sawasawa ninyi?inakera sana.

Sent from my Redmi Note 5 using JamiiForums mobile app
 
Umeandika madini tupu kiongozi

Na Jambo lingine asilolifahamu ni kwamba, Rais wetu mama Samia ni Raisi wa watanzania na sio Raisi wa waislamu

Kana akili fupi Sana haka kajitu
 
wewe pia ni mnufaika mpaka umekaa hapa kutweet.jibga wewe

Sent using Jamii Forums mobile app
Mimi Ni ndugu wa Eric Kabendera ambaye Dikteta alimuweka rumande kwa sababu alikuwa anamkosoa. Lakini shangazi yetu Mama wa Eric alikuwa anaishi kwa madawa ya Bei ghali. Yule Bibi alimuomba DIKTETA amuachie mwanaye kwa vile hawezi kuishi bila dawa.

Magufuli hakusikia, na hakumruhusu Eric hata kwenda chini ya ulinzi kumuaga mama yake ambaye alifariki kwa kukosa dawa.

Jifanyeni hamuyajui haya kwa vile WATANZANIA kwa unafiki ndiyo kawaida yenu
 
Umeandika madini tupu kiongozi

Na Jambo lingine asilolifahamu ni kwamba, Rais wetu mama Samia ni Raisi wa watanzania na sio Raisi wa waislamu

Kana akili fupi Sana haka kajitu
Nakuona tu unavyo jisogeza kwaheshimiwa Rais Mpya!! Yaani kidogo kidogo roho inaachana na mwili!! 😇

Muda si mrefu mtakuwa mnamponda Jpm na kumwagia sifa Mama! Na hii ndiyo sababu kubwa ya kuwaita nyinyi Mataga 'Misukule!'!
 
Mliwadanganya tu, Hali zao mbaya Kama chokoraa, mlitake advaerntage ya elimu yao ya chini
 
Mkuu, haina haja Sana iwe kufurahi ama vyovyote vile kunapotokea msiba, kwani hakuna mwenye jeuri ya kuchoropoka kwenye kifo,

Au wewe unajua utasepa lini na Kwa kifo kipi??
Mm sijui itakuaje kwa sababu there are millions ways to die.

Lkn linapotokea tatzo sisi tuliobaki tunatakiwa tuligeuze kuwa funzo juu ya namna ya kuish maisha yetu yaliyobaki.

Mahubiri ya msibani huhubiriwa wazima sio marehemu.

Tunalo jukumu kubwa sisi kama binadamu kupitia hili kujifunza na kutengeneza pale palipoharibika for better future.

Even if once Someone die He will be gone forever.

RIP Mr. Prezoo JPM. [emoji22][emoji22][emoji22][emoji22]
 
Nakuona tu unavyo jisogeza kwaheshimiwa Rais Mpya!! Yaani kidogo kidogo roho inaachana na mwili!! 😇

Muda si mrefu mtakuwa mnamponda Jpm na kumwagia sifa Mama! Na hii ndiyo sababu kubwa ya kuwaita nyinyi Mataga 'Misukule!'!
Mkuu kwani na wewe unasapoti udini?
 
Mbona ni kama hamumuamini mama,mnaingiza upepo.

Ambae haamini ni yule asiyekubali kwamba Samia Suluhu Hassan ni rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania kupitia chama cha mapinduzi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…