Nguvu ya matajiri itakapoanza kuchukua nafasi yake, kilio cha wanyonge kumlilia Dkt. Magufuli itazidi kusikika na wa kuwazuia hatakuwepo

Nguvu ya matajiri itakapoanza kuchukua nafasi yake, kilio cha wanyonge kumlilia Dkt. Magufuli itazidi kusikika na wa kuwazuia hatakuwepo

Binadamu sijui ataridhika na nini,huku anasema kazi ya Mungu haina makosa,alafu kwa upande mwingine anamkosoa Mungu kwa kumchukua mja wake aliyempenda zaidi.

Nia ya Mungu haichunguziki kamwe,hatujui ana mpango gani wa kuiponya hii nchi.
 
Pombe Magufuli hajawai kumtetea mnyonge yeyote bali alitumia wanyonge kujijenga kiaiasa. Kama ni kutetea wanyonge alipaswa kuwafidia wale wananchi wa Kimara- Kibaha aliowavunjia nyumba kupisha barabara.

Angekuwa mtetezi wa wanyonge asingetumia mabilioni kujenga Chato kijijini kwao miundombinu inayostahili kuwa makao makuu ya Mkoa wa Geita. Huku watoto wa Watanzania wanasoma kwenye kwenye miti na wengine hawana madawati. Au kununua madreamliner wakati 80% ya Watanzania hawapati maji safi.

Magufuli ilikuwa ni LAANA, na Mungu ametuepushia, tujenge Tanzania yetu nzuri isiyo na ubaguzi wa kiitikadi, kikabila na kikanda.
watu wanaonyosha maelezo hivi mmebaki wachache nchi hii. inabid mlindwe kwa ajiri ya breeding.
 
Hawa watu wameharibu sana huu mji, posta sasa hivi ni chafu sababu ya wamachinga kila eneo na kariakoo nako hakupitiki barabara zote wapo wao tu. Mlipa kodi huna thamani mbele ya mmachinga sasa hivi.
Machinga hawatakiwi onewa huruma hata kidogo
 
RIP my best Tanzanian president of all times..

Go in peace Magufuli.
 
Ndiyo!
Nguvu ya matajiri ikiilemea serikali hii mpya, wanyonge watalitaja Jina la JPM Kwa uchungu mkubwa na hakuna atakayewazuia

Pale rushwa itakapowafanya wanyonge, wamachinga, wamama ntilie, bodaboda, bajaji n.k ambao idadi Yao ni kubwa mno Kwa sasa katika nchi hii kuanza kufukuzwa kwenye maeneo Yao ya kazi aliyokuwa amewaruhusu Jembe Lao JPM R.I.P kufanyia biashara zao,

Ndipo sauti zao na Kwa uchungu mkubwa zitasikika, wakimlilia Kwa upya tena JPM na Jina lake litatawala Kwa upya kwenye vyombo mbalimbali za habari kote Tanzania na hata duniani

Pale majambazi ya kupora muda wowote asubuhi mchana na Wakati wowote yatakapojitokeza, iwapo Serikali hii haitasimama Kiume, sauti za wananchi wengi watakapoanza kumlilia JPM Kwa upya, na watu watasema ni Bora alipokuwepo Jembe haya yalikoma,

Pale matajiri wakubwa watakapoizidi serikali ujanja aidha Kwa rushwa Ili wasilipe Kodi, na Kodi nyingi kuelekezwa Kwa wafanya biashara wadogo wadogo, watu hawa wataanza kumlilia upya Jembe lao, watasema, ni Kwa sababu hayupo JPM ndio Maana wananyanyaswa?

Ingawa Nina Imani kuuubwa Sana na Raisi wetu Madame SHS, kwamba ni jemedali na jasiri asiyeogopa na asiyerudishwa nyuma, Kwa kuwa pia ufanisi wa serikali hii Naamini ni Kwa sababu mama alisimama nyuma yake kuhakikisha tunakuwa hapa tulipo

Mbali na hayo, Sisi ni binadamu tunaweza kujisahau yakarudi hayo na yakawa sababu ya Jina la Jembe kutajwa kila pahala kuwa yeye alikuwa ndiye na kimvuli chake kutawala midomo mwa watu wanyonge

Mh Raisi Madame Samia suluhu Hasan Tunakuombea, kwani tunajua ilivyongumu kuongoza nchi bila ya Mungu Kusimama Mbele yako

Wasalaam
Mtegemee Muumba wewe Achana na ushirikina na Ramli chonganishi kama za kina millionaire Bashite na Dotto
 
Hawa watu wameharibu sana huu mji, posta sasa hivi ni chafu sababu ya wamachinga kila eneo na kariakoo nako hakupitiki barabara zote wapo wao tu. Mlipa kodi huna thamani mbele ya mmachinga sasa hivi.
Wanakera sana mkuu,sio siri, parking zote wamechukua wao
 
Hapo kwenye ujambazi na vibaka daah!!! Raisi Samia Suluhu Hassan naomba asimame imara Sana
 
Asante Rwazi1 kwa kutupa nguvu. Na hii kazi tumeifanya non stop bila kujali MATAGA na wale Lumumba Buk 7 ambao wanatetea kila upuuzi wa Meko
I
Hivi Kirefu cha MATAGA ndio hii

Mataga ni MAKE TANZANIA GREAT AGAIN
 
Badala ya matajiri kuwa watu wanaotisha wakawa watu wa chama.Yale yale tu.
Hao wa unanijua mimi ni nani sasa hivi ndio wako wazi wazi. Siku za nyuma matajiri walitamka hayo hadharani kwasababu walikuwa wanawatumia viongozi kuwafanyizia watu, sasa viongozi waliotumika na matajiri ndio wamejitokeza wazi wazi. Kuanzia kupora chaguzi, kodi kandamizi, kupora mabureua de change, watu kutekwa, na kuuwawa tumeyaona wazi wazi kwenye utawala huu.

Kwa ujumla utawala uliopita ulikuwa wa mtu muovu, hiyo kutetea wanyonge ni hadaa ya mdomoni ili kuficha uharamia uliokuwa unafanyika.
 
Back
Top Bottom