CHIBURABANU
JF-Expert Member
- Sep 19, 2013
- 2,921
- 3,474
Sawa kabisa mkuuAmbae haamini ni yule asiyekubali kwamba Samia Suluhu Hassan ni rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania kupitia chama cha mapinduzi
watu wanaonyosha maelezo hivi mmebaki wachache nchi hii. inabid mlindwe kwa ajiri ya breeding.Pombe Magufuli hajawai kumtetea mnyonge yeyote bali alitumia wanyonge kujijenga kiaiasa. Kama ni kutetea wanyonge alipaswa kuwafidia wale wananchi wa Kimara- Kibaha aliowavunjia nyumba kupisha barabara.
Angekuwa mtetezi wa wanyonge asingetumia mabilioni kujenga Chato kijijini kwao miundombinu inayostahili kuwa makao makuu ya Mkoa wa Geita. Huku watoto wa Watanzania wanasoma kwenye kwenye miti na wengine hawana madawati. Au kununua madreamliner wakati 80% ya Watanzania hawapati maji safi.
Magufuli ilikuwa ni LAANA, na Mungu ametuepushia, tujenge Tanzania yetu nzuri isiyo na ubaguzi wa kiitikadi, kikabila na kikanda.
Hiyo ni mbaya mkuuNi Bora mana kuna watu walianza kujiona hii ni nchi yao na Wana hati miliki ya kuwa kila sehemu. Kila sekta , na kuwanyima fursa wengine.
Sent using Jamii Forums mobile app
Tanzania hatuna mifumo imaraMfumo ni bora kuliko nguvu ya kiongozi
Machinga hawatakiwi onewa huruma hata kidogoHawa watu wameharibu sana huu mji, posta sasa hivi ni chafu sababu ya wamachinga kila eneo na kariakoo nako hakupitiki barabara zote wapo wao tu. Mlipa kodi huna thamani mbele ya mmachinga sasa hivi.
Unazo sababu za Kwa nini hawatakiwi kuonewa huruma, ama wao si wamoja wetu ktk nji hii mkuuMachinga hawatakiwi onewa huruma hata kidogo
Wawekewe sehemu yao waache barabaraUnazo sababu za Kwa nini hawatakiwi kuonewa huruma, ama wao si wamoja wetu ktk nji hii mkuu
Mtegemee Muumba wewe Achana na ushirikina na Ramli chonganishi kama za kina millionaire Bashite na DottoNdiyo!
Nguvu ya matajiri ikiilemea serikali hii mpya, wanyonge watalitaja Jina la JPM Kwa uchungu mkubwa na hakuna atakayewazuia
Pale rushwa itakapowafanya wanyonge, wamachinga, wamama ntilie, bodaboda, bajaji n.k ambao idadi Yao ni kubwa mno Kwa sasa katika nchi hii kuanza kufukuzwa kwenye maeneo Yao ya kazi aliyokuwa amewaruhusu Jembe Lao JPM R.I.P kufanyia biashara zao,
Ndipo sauti zao na Kwa uchungu mkubwa zitasikika, wakimlilia Kwa upya tena JPM na Jina lake litatawala Kwa upya kwenye vyombo mbalimbali za habari kote Tanzania na hata duniani
Pale majambazi ya kupora muda wowote asubuhi mchana na Wakati wowote yatakapojitokeza, iwapo Serikali hii haitasimama Kiume, sauti za wananchi wengi watakapoanza kumlilia JPM Kwa upya, na watu watasema ni Bora alipokuwepo Jembe haya yalikoma,
Pale matajiri wakubwa watakapoizidi serikali ujanja aidha Kwa rushwa Ili wasilipe Kodi, na Kodi nyingi kuelekezwa Kwa wafanya biashara wadogo wadogo, watu hawa wataanza kumlilia upya Jembe lao, watasema, ni Kwa sababu hayupo JPM ndio Maana wananyanyaswa?
Ingawa Nina Imani kuuubwa Sana na Raisi wetu Madame SHS, kwamba ni jemedali na jasiri asiyeogopa na asiyerudishwa nyuma, Kwa kuwa pia ufanisi wa serikali hii Naamini ni Kwa sababu mama alisimama nyuma yake kuhakikisha tunakuwa hapa tulipo
Mbali na hayo, Sisi ni binadamu tunaweza kujisahau yakarudi hayo na yakawa sababu ya Jina la Jembe kutajwa kila pahala kuwa yeye alikuwa ndiye na kimvuli chake kutawala midomo mwa watu wanyonge
Mh Raisi Madame Samia suluhu Hasan Tunakuombea, kwani tunajua ilivyongumu kuongoza nchi bila ya Mungu Kusimama Mbele yako
Wasalaam
Mkuu, ni angalizo tu!Mtegemee Muumba wewe Achana na ushirikina na Ramli chonganishi kama za kina millionaire Bashite na Dotto
Wanakera sana mkuu,sio siri, parking zote wamechukua waoHawa watu wameharibu sana huu mji, posta sasa hivi ni chafu sababu ya wamachinga kila eneo na kariakoo nako hakupitiki barabara zote wapo wao tu. Mlipa kodi huna thamani mbele ya mmachinga sasa hivi.
Kama wameshindwa mkuu hata ukiwapa miaka 500 hawatabadilikaHao wanyonge siku zote, miaka yote 6 wameshindwa kujiondoa unyonge baada ya kupata mtetezi ???
Ni hivyo kweli. Lakini members ni wale UVCCMI
Hivi Kirefu cha MATAGA ndio hii
Mataga ni MAKE TANZANIA GREAT AGAIN
Hao wa unanijua mimi ni nani sasa hivi ndio wako wazi wazi. Siku za nyuma matajiri walitamka hayo hadharani kwasababu walikuwa wanawatumia viongozi kuwafanyizia watu, sasa viongozi waliotumika na matajiri ndio wamejitokeza wazi wazi. Kuanzia kupora chaguzi, kodi kandamizi, kupora mabureua de change, watu kutekwa, na kuuwawa tumeyaona wazi wazi kwenye utawala huu.
Kwa ujumla utawala uliopita ulikuwa wa mtu muovu, hiyo kutetea wanyonge ni hadaa ya mdomoni ili kuficha uharamia uliokuwa unafanyika.