Nguvu ya mfumo humfanya kila mteule (mtu) afanane na aliowakuta

dmkali

JF-Expert Member
Joined
Nov 17, 2014
Posts
12,283
Reaction score
23,443
Nguvu ya mfumo!

Ni aina ya genge la watu au taasisi wanaojielekeza kutekeleza malengo flani!

Miongoni mwa malengo hayo yanaweza kuwa ni ya kisiasa, kiulinzi, kiuharifu au Vinginevyo!!

Sifa moja kuu ya Mfumo (system) ni kurithisha tabia njema au mbaya kizazi hadi kizazi!

Ni binadamu wachache sana waliowahi kufanikiwa kufanya tofauti na mfumo! Lakini waliowengi Humezwa na MFUMO!

Mfumo unafanana na nini?

MFUMO wa kisiasa ni kama vazi maalum ambalo kila anayeingia hulazimika kuvaa! MFUMO Ni kama MVINYO ambapo hata ukiweka kwenye chupa ya maziwa utabaki na ALCOHOLIC ileile!

MFUMO wa kisiasa ni kama control room ambapo kila anaeingia hata kama yupo kinyume atalazimika kubonyeza vitufe vilivyopo!

MFUMO wa kisiasa ni kama chumba chenye AC, ambapo kila anaeingia na jasho hupozwa na kusahau hali ya inje!

Kwasababu hiyo!
  • Ndiyo maana traffic polisi akili zao zinafana kwasababu ya Mfumo!
  • Boda wote akili zao zinafanana!
  • Bamedi wote akili zao zinafanana
  • Majambazi ote akili zao zinafanana.
  • Wana CCM wote akili zao zinafanana etc
Hivyo utawala wa Mama Samia hautakuwa na maajabu kwasababu KAINGIA akijipepea jasho Lakini taratibu Ubaridi wa AC utamkumba!

IKULU HATA RAIS AKIWA NG'OMBE TUTASONGA KWA MFUMO!

Kama mnataka mabadiliko ya kweli FUMUENI MFUMO KWANZA!

  • MFUMO uliopo sasa una mfanya kiongozi aishi kama Malaika!
  • MFUMO uliopo sasa kiongozi hata akiiba mabilioni Ya fedha hakuna cha kumfanya zaidi ya kumuita FISADI basi
  • MFUMO uliopo sasa kiongozi anaweza kudalalia manunuzi ya madege kwa bei kubwa na hakuna wa kumhoji
  • MFUMO uliopo sasa kiongozi hawajibiki kuishi kwa kufuata sheria.
  • MFUMO uliopo sasa pensheni na mafao ya viongozi wanalipana wao mapema kuliko Yale ya wanainchi.
  • MFUMO uliopo sasa kiongozi halazimiki kufuata sheria Bali sheria inamfuata kiongozi!
LILIENI KUBADILI MFUMO KWANZA
 
Taifa letu mifumo ambao viongozi wanachukua sio kabisa, halafu cha kushangaza hata hawapati akili wala hawaamki.

Mfano mzuri;

1) Mfumo wa viongozi kuwateua walimu wa vyuo vikuu (Ma Dr na Prof) kwenda kuwa Mkuu Wa Mkoa au kugombea ubunge au kushika nafasi nyingine serikalini.

Sio akili, ni ujinga, kwasababu una sababisha upungufu wa walimu vyuoni kisa kuonyesha kwamba serikali/bunge fulani ndio inaongoza kuwa na viongozi/wabunge wasomi zaidi kuliko nchi nyingine.

Hawatambui kwamba, mtu anaweza akawa mwalimu mzuri chuo (Lecturer - Dr au Prof) ila practically field akawa hana uwezo kabisa. Na unasababisha uhaba wa walimu vyuoni.

2) Mfumo wa kulipa fadhila kwa kugawana vyeo au nafasi. Hii imetokea sana na inaendelea kutokea. Hawaangalii uwezo wa mtu ila wanaangalia sababu nyingine zao binafsi.

Mara kadhaa tumeona, watu wakipewa zawadi ya kuteuliwa mbunge ili aende akapumzike baada ya kufanya kazi au jukumu fulani.

3) Mfumo wa kuoneana aibu na kuendelea na watu wasio na uwezo.

Tumeona mara kadhaa, mtu ana fukuzwa kazi (Anatumbuliwa kwa lugha ya sasa) kwa ufisadi au kushindwa kuendesha ofisi/wizara kwa misingi ya kisheria au matakwa ya kiongozi, ila akifukuzwa lugha inayotumiwa na mfumo ni kwamba "AMTENGULIWA UTEUZI WAKE NA ATAPANGIWA NAFASI YA KAZI NYINGINE". Really??? Mtu amedhihirisha hana uwezo anaondolewa na kupelekwa sehemu nyingine ili akaharibu??? Ina maana hakuna watanzania wengine wenye uwezo wa kuchukua hizo nafasi???
 
Ni mifumo ya hovyo sana
 
Really??? Mtu amedhihirisha hana uwezo anaondolewa na kupelekwa sehemu nyingine ili akaharibu???
Aliwahi kusema mheshimiwa mmoja, hawa watu wana nguvu, mkiwafunga hawa nchi itatikisika, watu wakamuona yule bwana kuwa ni dhaifu. Lakini kiukweli yeye alikuwa 'maabara' na aliewa kwa undani kuwa hawa watu wana nguvu kiasi gani. Unapowaweka watu dizaini hiyo nje ya mfumo, watatumia nguvu walizo nazo kukuvuruga, so ni better wakae ndani ya mfumo wasikuvuruge even though they will be busy doing nothing.
 
Duh
 
China huwa wananyonga hadharani ndiyo maana waliendelea haraka
 
Sioni tatizo na katiba yetu
 
Sioni tatizo na katiba yetu
Ni kwa sababu upo ndani ya MFUMO! Kiama chenu kipo kwenye ile Rasimu ya Katiba ya Jaji Warioba. Ikipitishwa ile na kuwa Katiba rasmi ya nchi, hakika CCM (wamiliki wa huo MFUMO) mtapoteana.
 
Ni kwa sababu upo ndani ya MFUMO! Kiama chenu kipo kwenye ile Rasimu ya Katiba ya Jaji Warioba. Ikipitishwa ile na kuwa Katiba rasmi ya nchi, hakika CCM (wamiliki wa huo MFUMO) mtapoteana.
Ubinafsi ni kitu kibaya sana! Hizi Mali tukigawana kwa haki zinatosha sana watanzania wote bila lawama
 
UMESIKIA MAMA ALICHOSEMA? YEYE NA MAGUFULI NI KITU KILEKILE
 
Ni kwa sababu upo ndani ya MFUMO! Kiama chenu kipo kwenye ile Rasimu ya Katiba ya Jaji Warioba. Ikipitishwa ile na kuwa Katiba rasmi ya nchi, hakika CCM (wamiliki wa huo MFUMO) mtapoteana.
Hatari sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…