GODSON KITOMARY
Member
- Jun 23, 2020
- 12
- 23
Utawala bora ni mfumo ambao unasimamia sheria,taratibu na kanuni ambazo husimamiwa na serikali au taasisi yoyote ili kuhakikisha kuwa hakuna ukiukwaji wa haki za binadamu,uvunjifu wa sheria pamoja na maadili ya kazi ambayo yameweka ili kumwongoza kila mmoja katika utendaji wake wa kazi ili kuhakikisha kila mtu ananufaika na uongozi ulioko madarakani.
Uwajibikaji ni hali ya mtu kutambua majukumu yake, kuyasimamia na kuyatekeleza ipasavyo kutokana na nafasi aliyopo na muda husika aliopangiwa au kuwa nao kuna aina kadhaa za uwajibikaji ambao ni wa kiutendaji,kifedha,kwa umma na pia uwajibikaji wa kisheria. Yafuatayo ni mambo yanayopelekea utawala bora na uwajibikaji katika kuimarisha maendeleo ya jamii kama ifuatavyo;
Ushirikishwaji wa umma/Wananchi katika dhana nzima ya maamuzi haswa ambayo yanayowausu wao.Serikali au Viongozi hawana budi kuwashirikisha wale ambao wamewapa ridhaa na kuwaweka madarakani kwa niaba ya yao ili waweze kuwaamulia lakini kwa upande mwingine wanapaswa kuangalia baadhi ya maamuzi watakayokwenda kuyachukua na kuwashirikisha wananchi kama walengwa wakuu wa sera, kanuni, sheria au mambo mengine mbalimbali.mfano ndani ya Tanzania tunaona kuwa katiba zote tano zilizowahi kutumika kuanzia mwaka 1961 hadi ile ya mwaka 1977 ambayo ndiyo inatumika mpaka sasa hazikushirikisha wananchi katika uundwaji wake bali chama kiliteua watu 20 ambao walikwenda kutunga hizo katiba ambazo mpaka sasa zinakandamiza baadhi ya haki mfano kutokuwa na haki ya kugombea kama mgombea huru(private Candidate).
Upatikanaji wa taarifa sahihi na kwa wakati pia ni jambo linalochochea uwajibikaji na utawala bora ndani ya jamii kwakuwa wananchi wanapopata taarifa sahihi kwa wakati huwa ni rahisi kufanyia maamuzi,kushauri na kuwakosoa viongozi kabla hawajafanya maamuzi yatakayoigharimu jamiinyao.Pia kutokana na kuwa na taarifa sahihi uuondoa mkanganyiko ndani ya jamii na watu kuwa na uelewa mpana zaidi,Mfano suala la mkataba wa Bandari kati ya Dubai na Tanzania lilileta mkanganyiko mwanzoni kwakuwa serikali hakutolea ufafanuzi mkataba huo na hata utiwaji saini wake bado wananchi hawakuwa na taarifa yake mpaka pale ulipokuja kuibuliwa mwezi huu na wanasiasa mbalimbali na watu maarufu.
Uhuru wa vyombo vya habari ni kiashiria kingine cha utawala bora na uwajibikaji endapo tu vyombo na waandishi wa habari watakuwa huru kuripoti mambo mbalimbali mazuri na mabaya yanayofanywa na serikali yao,pia kuruhusiwa kuandika habariza kiuchunguzi juu ya maswala mbalimbali ambayo yanafwanya na serikali bila yakuwa na kipingamizi chochote wala kukandamizwa.Pia pale vyama vya siasa vinapoweza kutumia vyombo vyote vya habari pasipo ubaguzi wowote na upendeleo wowote.Mfano hapa Tanzania ni nadra sana kuona habari za vyama vya upinzani na viongozi wanaokosoa serikali.pia hata katika swala la bandari tumeona Waziri wa Habari akitishia baadhi ya vymbo vya habari vitakavypendelea na uzungumzaji wa mkataba wa bandari.
Kuweka sheria na taratibu za uwazi ni msingi mwingine wa utawala bora na uwajibikaji ambao utawafanya viongozi kuweka wazi michakato yote ya baadhi ya mambo ambayo wanayafanya kabla ya kuyatolea maamuzi ili wapate ukosoaji utakaowasaidia kufanya maamuzi yenye busara na yenye tija kwa Taifa na jamii yote.Endapo patakuwa na uwazi katika swala zima la ufanyaji maamuzi bhasi kama taifa tutafika mbali. Mfano katika swala la utiaji saini mkataba wa bandari swala hili la mkataba halikuwa wazi na umesainiwa muda mrefu na kuja kujadili ndani ya huu mwaka.
Hivyo bhasi,utawala bora na uwajibikaji ni muhimu sana katika kujenga na kudumisha jamii yenye haki, usawa, na maendeleo endelevu. Ni wajibu wa viongozi wa umma na taasisi za umma kuzingatia misingi hii ili kuhakikisha kuwa wanatumikia wananchi kwa uadilifu na ufanisi. Wananchi pia wana jukumu la kushiriki katika michakato ya kisiasa na kudai uwajibikaji kutoka kwa viongozi wao.

Upvote
0