Nguvu za giza na mizimu ya ukoo

Nguvu za giza na mizimu ya ukoo

Unachokiongea is real, ni wachache wanaweza kukuelewa.

Iko hivi:
Usithubutu kabisa kufanya hayo matambiko, ukifanya matambiko unayapa nguvu zaidi dhidi yako.

1. Jikabidhi kwa Mwenyezi Mungu kiukweliukweli, siyo unatia mguu kisha unatoka
2. Ishi maisha ya usafi, acha uzinifu, ulevi, na mambo machafu
3. Kuwa conscious na Mwenyezi Mungu , yaani kulitaja jina lake mara kwa mara ukiwa peke yako, kumuomba (Lakini kuwa makini usije kugeuka kama walokole wale wapiga makelele njiani)
4. Kabla hujatoka kwenda kazini, taja jina la Mwenyezi Mungu, Ukirudi nyumbani fanya hivyo hivyo
5. Ukifanya maombi vita ikawa kubwa usiogope, jikaze, yenyewe yataretreat. Yakiretreat haimaanishi yameondoka, yankungoja ukiwa ktk low spirit level yaje tena, kwa hiyo ndiyo maana ni muhimu sana kuishi ktk high spiritual levels all the time.
6. Huwa yana kawaida ya kukuletea mawazo ya kukata tamaa, unaweza kudhani ni wewe ndiye unayedhani hivyo bila influence yoyote, lakini kimsingi yenyewe ndo yanaplant mawazo hayo. Jifunze kuignore mawazo negative na kupromote mawazo chanya.
7 Hiyo ni vita nzito, ukiimanage Mweneyezi Mungu kwa rehema zake atakupa malipo makubwa
TRUE MKUU
 
nilianza na kuumwa homa za ajabu ajabu, mwili kuchoka, dalili za homa ya Presha.



Ulipima damu kubwa mkuu?
 
Sawa mkuu, achabnipite kwenye website yake
Usikate tamaa,

Una kitu kikubwa ndani Yako, ndo sababu unapitia vita kubwa.

Ukishinda vita na kubomoa madhabahu ya Mizimu ya ukoo wenu, utakuwa lango la Ukoo wote kuokoka na kufanikiwa katika Kila nyanja, kielimu, kiimani, kiuchumi, kiuzao nk nk.

Ubarikiwe sana, mwana wa Mungu aliye hai.

Amen
 
Wewe ndio unashida wala hakuna mizimu wala nguvu za giza.

Ukisha uaminisha ubongo wako na Akili yako kwamba kitu fulani ndicho chanzo cha matatizo yako, Basi ubongo wako uta respond hivyo hivyo.
Mkuu jibu ili apa
 
Wachangiaji hapo juu wanaipinga hiyo ibada,sijajua mapungufu ya hiyo ibada.
Kama ni sadaka kote zinahitajika kwa kiwango kisichopishana, masharti yanafanana
Utofauti mizimu inatumia mabavu yani inakulazimisha ufanye wanavyotaka, wanakutesa kama ambavyo jamaa alivyoeleza.
 
Nilipokua mwanzo nahanagika upande wa Giza niliambiwa nasumbuliwa na hizo roho na wazee nyumba waliniambia hivyo hivyo
Hakuna cha wazee. Mtu akifa, kafa.

Unachezewa na watu wabaya kwa kisingizio cha mizimu.

Ikomboe roho yako kabla haijapotea mazima.
 
Fanya uamuzi sasa wa kufuata njia ya Mungu (Yesu Kristo) moja kwa moja bila kupepesa macho utakuwa huru.

Ndio vita itakuwepo lakini mwisho utashinda.

Unachopaswa kufanya ni kujitenga na mizimu ya kwenu pia kupigana vita ya kiroho na wachawi kwani ndio wanaofanya kazi na hizo roho za mizimu.

Hao wachawi sio hata watu wa mbali, ni wanafamilia yenu, mashangazi, wajomba, ndugu, binamu au hata baba na mama yako!

Vita ya kiroho unahitajika kuwa na IMANI kubwa na UJASIRI. Lakini kwasasa fanya vita ukiwa na usaidizi na watumishi wa kweli wa Mungu Aliye Hai. Endelea mpaka ushindi upatikane.

Kwasasa anza kukataa roho za mizimu kwa kutubu ushirikina wowote uliofanya wewe au wazazi kwa niaba yako. Jitakase kwa damu ya Yesu kila wakati.

Ukiwa vizuri kiroho sasa yageukie mapepo na mizimu kwa ujasiri na bila woga wala huruma yafukuze kwa Jina la Yesu na iite Damu ya Yesu.

Fanya sala za nguvu (aggressive prayers) kama vile mtu anayegombana au kupigana; rusha moto wa Yesu kwa mizimu ukiiamuru kukuacha na kutoka maishani mwako. Jitakase kwa Damu ya Yesu kila wakati. Kiitie Jina la Yesu kila wakati na litumie KUHARIBU kila uchawi kwenye maisha yako kila siku.

Pigana vita kweli kweli, rusha moto wa Yesu kwa mizimu, vunja vunja uchawi kwa Damu ya Yesu, nk

Vita hii inataka uwe MKALI kama simba kwenye mawindo huku ukitumia Jina la Yesu, Damu ya Yesu na Moto wa Roho Mtakatifu.

Anza sasa na nipe mrejesho.
Jina la mungu aliyeuliwa ,upuuzi
 
Afu huyu kijana sio tu mizimu sijui nn ... Mara maisha vle mara hiv... Mara makanisa mara sjui nn


Oya kijana kwanza unaonekana hauna Pesa.[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787] Tafuta pesa hta kw jasho pga kaz yyte pga vbarua pata pesa yko ishi toa fikra za kijinga
Ukipata pesa yyte hautoona usumbufu w mizimu wala ktu chchte utaish kwny uhalisia w mahtaj yko huwez kuhis unarogwa au mizmu inaharbu maisha yko

Pesa nazo n changamoto unaweza kla ktu hakiko sawa

Mara vle mara hiv
Huo ni mtazamo wa kwamba wenye pesa hawana shida kama hizi? Nakumbuka niliwahi kusoma na mtoto mmoja wa kiarabu, ilikuwa ikifika saa nne asubuhi baada ya kutoka mapumziko basi lazima aanze fujo atarusha viti, atajibamiza ubaoni yani vurugu tupu hadi anakuja baba ake anamchukua.
Inasemekana katupiwa kitu kibaya na lengo asisome, ukimuona usoni ana makovu kwa ajiri ya kujipigiza ukutani na anaham hama shule kwa ajiri hiyo.
 
Mkuu hilo ndio suluhisho au huduma ya kwanza?
Hilo ndio suluhisho mkuu hakuna zaidi ya hapo.

na pia awe na kumbukumbu kama kuna siku aligombana na wazazi wake na wakamtamkia maneno makali..kwahiyo inabidi pia apate muda wa kutuliza akili.

Kwenye haya maisha kila stori za maisha anayopitia au aliyopitia lazima itakupa huzuni.

Hata hao wenye pesa walipitia wakati mgumu au pengine wanapitia wakati mgumu pia.
 
Habari wana JF, mimi ni new member ningependa mnikaribishe katika Jukwaa letu.

Mimi Ni kijana wa miaka 30’s, kwa mda wa miaka 3 nimekua nikisumbuliwa na Nguvu za giza na Mizimu ya ukoo ambayo imepelekea kuharibu dira ya maisha yangu, nilianza na kuumwa homa za ajabu ajabu, mwili kuchoka, dalili za homa ya Presha.

Nilihangaika sana ikiwemo kwenda kwa waganga wa kienyeji, nikawa napata nafuu lakini baada ya mda hali inarudi palepale, nikajaribu na makanisani ikawa ni vita kali, nako nikawa napata nafuu ila hali inarudi pale pale ikiwa kuhisi mwili unaumwa, kuchoka, macho kuhisi yana kiza na Moyo kuuma sana.

Nilihangaika pia na maombi binafsi ya kujiombea mimi mwenyewe pamoja na watumishi wa Mungu, nikafanikiwa kupunguza hii hali kwa kiasi chake nikapata nafuu.

Kuja kwenu wanaJF ninaomba ushauri kwa sababu nimefungwa upande wa uchumi, akili yangu imefungwa.

Inafika hatua ya kukata tamaa na kuona kila kitu hakiendi na pia kila ninapopata ishu ya kazi au dili lolote hua inafika sehemu mambo yanaharibika, nimekua na roho ya kukataliwa, kila ninapoenda ninadharauliwa na kubezwa, nilishaenda sehemu nikahisiwa mimi ni Mwizi, kiukweli ni kama nina mikosi au gundu.

Siku Moja niliwasiliana na ndugu wa baba ambao wao ni wasukuma, wakaniambia hio kawaida kuna mizimu inabidi kwenda kutambika kwa sababu ukoo wetu tangu enzi ni wa mambo hayo ya kimizimu.

Nipo kwenye dilema nikubaliane na mambo ya kutambika au niendelee huku niliko upande wa Makanisa, japo kiukweli napata vita kubwa kila napopigana na hizi nguvu makanisani.

WanaJF kiukweli nimefika hatua nachanganyikiwa, kila kitu hakiko sawa, nakosa kujiamini kwa kila jambo nalotaka kufanya, ninaomba ushauri wenu na mawazo yenu.

Najua Jukwaa hili lina watu wenye maarifa na maono. Nitashukuru sana

Cc MshanaJR

Kama kijana wa miaka 30 anaenda kwa mganga vipi akifikisha miaka 50 huko?

Nenda hospitalini kwanza acha ilani za kijinga
 
Hilo ndio suluhisho mkuu hakuna zaidi ya hapo.

na pia awe na kumbukumbu kama kuna siku aligombana na wazazi wake na wakamtamkia maneno makali..kwahiyo inabidi pia apate muda wa kutuliza akili.

Kwenye haya maisha kila stori za maisha anayopitia au aliyopitia lazima itakupa huzuni.

Hata hao wenye pesa walipitia wakati mgumu au pengine wanapitia wakati mgumu pia.
Sawa mkuu.
 
Siku Moja niliwasiliana na ndugu wa baba ambao wao ni wasukuma, wakaniambia hio kawaida kuna mizimu inabidi kwenda kutambika kwa sababu ukoo wetu tangu enzi ni wa mambo hayo ya kimizimu.

Nipo kwenye dilema nikubaliane na mambo ya kutambika au niendelee huku niliko upande wa Makanisa, japo kiukweli napata vita kubwa kila napopigana na hizi nguvu makanisani.
mkuu pole sana ila ninachokushauri hayo mambo ya kimila usiyapuuze, NARUDIA TENA USIYAPUUZE ........why? ninapofanya kazi kuna staff alikumbwa na changamoto flani akawa kachanganyikiwa kabisa na zilipofanyika juhudi za maombi ndio hali ikwa worse zaidi. Ilibidi arudishwe kwao kwenye mishe za kimila mambo yakawa sawa na yupo fresh sasa.

NB. Jamaa nae ni msukuma na tatizo lake pia lilichagizwa na mizimu ya huko kwao.... ukipuuza shauri yako ila huu ni ushauri tuu.
 
Back
Top Bottom