Nguvu za giza na mizimu ya ukoo

Ila nilichokiona humu kwenye haya matatizo ya kiroho kila mtu anaona hayana ujuzi kwa maana kila mtu anatoa tu maoni yake binafsi kwa mitazamo yake na si kwa uelewa au uzowefu.
 
Utapigwa zaidi hasa ukichanganya Mungu na Mizimu...

Chagua kubaki kwa Mungu...
 
Kwanini unaamini vitu vya kuambiwa na hisia za ajabu? Hapo tatizo ni wewe na wala hayo mambo hayapo mahali popote.fanye setting yako ya mind upya na nenda hospital.
 
Yesu Kristo ndio kiboko ya yote hayo. Tatizo ulienda kanisani kwaajili ya kuponywa na si kunyoosha njia zako baada ya uponyaji. Ukiamua kumtumikia Yesu kikamilifu hakika hayo yote yatakukimbia.
 
Benil Mizimu inatesa mno ingia YouTube tafuta Bishop Elibariki Sumbe my dear masomo yote ya mizimu na utendaj kaz wake utaelewa.. Hutobaki kama ulivyo
Sana kwa ambao hawajapata changamoto hii ni ngumu kuelewa,
 
Kama kijana wa miaka 30 anaenda kwa mganga vipi akifikisha miaka 50 huko?

Nenda hospitalini kwanza acha ilani za kijinga
mkuu unapofikwa na majanga makubwa hasa hasa homa ambayo inakukatisha tamaa. Chochote utakachoambiwa tiba utakubali tu ili mradi ukae sawa, sio kwamba nilivyoanza kuumwa sikwenda hospitali, nilienda na Hakuna homa, ilifikia hatua Daktari ananipa ushauri nikanywe maji mengo zaidi, nifanye mazoezi na kula matunda mana homa haionekani. Mimi binafsi kwa niliyopitia siwezi kurudi tena kwa waganga wa kienyeji
 
Sana kwa ambao hawajapata changamoto hii ni ngumu kuelewa,
kabisaa. Mfatilie huyo mtumishi wa Mungu kila linalokusumbua utapata kuelewa na kufunguliwa
 
Usifanye mazindiko yoyote ya kimila ni hatari zaidi, endelea kuamini kuwa Mungu anaweza yote Mungu ndiyo jibu la uzima wa milele, ukiingia huko kutoka ni ishu zaidi maana utakua umeingia kwenye maagano ya nguvu za giza
 
Hebu nenda kajipatanishe na ndugu zako. Hizi dini tumeletewa tu. Unaacha miongozo ya asili yako unaanza kuhangaika na mungu wa Israel!!!... You are not serious.
 
Hapana HIV sina mkuu nilishapima
Sawa mkuu , ila badilisha mtazamo wako kuhusu hiyo hali , utakua poa tu, hali kma hyo inampata kila mtu tu , chukulia kawaida.
 
Mateso yalikuandama pale ulipooanza sana kuamini uganga kuliko mambo mema ya Mungu, Mungu huwa haziakiwi, nachukuia sana kuona mtu anapambana kweli na mambo ya giza, uganga, uchawi, ushirikina
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…