Ng'wanakapolo mwanamke aliyetetemesha Magu. Misukule yake ya Kihindi na Kizungu iliwashangaza wengi

Ng'wanakapolo mwanamke aliyetetemesha Magu. Misukule yake ya Kihindi na Kizungu iliwashangaza wengi

Masimulizi ya kijinga kama Yale ya kinjekitile ngwale kubadilisha risasi kuwa maji.
Sasa huyo mchawi wa kisukuma ameacha nini Cha kujivunia huko usukumani?
Kuanzia mbogwe,Geita,Kahama mpaka Tabora?zaidi ya umaskini tu,
Uchawi ni uharibifu hauna faida kwa mchawi wala Jamii husika.
Ushirikina unapunguza uwezo wa kufikiri
 
Machimbo ya kwanza ya dhahabu yalianza kuchimbwa Geita(GOLD EXPLONATIONS IN TANGANYIKA) miaka ya 1940s
Na wewe sasa asitufanye Sisi mazombie mpaka utudanganye! Unataka kutuambia asili ya jina la Geita ni ufupisho wa hicho ulichoandika? Wacha mambo yako wewe!
 
Na wewe sasa asitufanye Sisi mazombie mpaka utudanganye! Unataka kutuambia asili ya jina la Geita ni ufupisho wa hicho ulichoandika? Wacha mambo yako wewe!
Pole sana. Lete Tafsiri unayoijua wewe
 
Na wewe sasa asitufanye Sisi mazombie mpaka utudanganye! Unataka kutuambia asili ya jina la Geita ni ufupisho wa hicho ulichoandika? Wacha mambo yako wewe!
Kulikuwa na mlima wa mizimu pale Geita ambao watu walikuwa wakifika eneo hilo wanauawa hivyo Walongo ambao ni wenyeji wa asili wa Geita wakasema ' AKABANGA KENTA ABANTU ' maana yake 'MLIMA UNAUA WATU baadaye wakaanza kuita "KETA" Wazungu walipofika eneo hilo wakatamka GETA.
Walipoanza uchunguzi wa madini ya dhahabu katika milima hiyo wakaweka bango lilisomeka" GOLD EXPLANATIOS IN TANGANYIKA" kwa kifupi GEITA, ndio ukawa mwanzo wa kuita eneo hilo GEITA badala ya GETA.
Tatizo vijana wa Siku hizi mnaleta ubishi bila kuchimbua historia. Mnaokoteleza taarifa tu.
 
Kulikuwa na mlima wa mizimu pale Geita ambao watu walikuwa wakifika eneo hilo wanauawa hivyo Walongo ambao ni wenyeji wa asili wa Geita wakasema ' AKABANGA KENTA ABANTU ' maana yake 'MLIMA UNAUA WATU baadaye wakaanza kuita "KETA" Wazungu walipofika eneo hilo wakatamka GETA.
Hii ndiyo asili ya jina Geita, hayo mengine uliyoweka ni utopolo mtupu! Akabanga Keta Abantu Ndiyo asili sahihi ya hilo jina. Wazungu walipofika wakashindwa kutamka vizuri hiyo Keta ikawa Geita!
 
Hii ndiyo asili ya jina Geita, hayo mengine uliyoweka ni utopolo mtupu! Akabanga Keta Abantu Ndiyo asili sahihi ya hilo jina. Wazungu walipofika wakashindwa kutamka vizuri hiyo Keta ikawa Geita!
Umekariri. Pole sana. Hicho nilichoandika ndio ukweli wenyewe. Tatizo hupendi kuchimbua unarelax sana lakini siyo kosa lako ni utoto ukikua utaacha.
 
Magu imekithiri kwa uchawi, mji umegoma kabisa kuendelea, stendi yao ni ileile tangu miaka ya 70.

Pale Nassa Kuna gambushi matata sana, ukiwa Magu unaendesha gari usiku, ni kawaida kuona bibi anavuka barabara ghafla, ukimkwepa umekwisha
 
Umechanganya sana kuhusu hayo makaburi ya Kabiga katika wilaya ya Nyag'hwale.eneo hilo la Usambilo wamisionari waliuawa na wenyeji kwa kupigiwa mishale yenye sumu siyo kwa kurogwa.nenda kafanye utafiti tena.
MishaLe Yenye sumu ilishinda nguvu za risasi
 
Back
Top Bottom