Ng'wanakapolo mwanamke aliyetetemesha Magu. Misukule yake ya Kihindi na Kizungu iliwashangaza wengi

Ng'wanakapolo mwanamke aliyetetemesha Magu. Misukule yake ya Kihindi na Kizungu iliwashangaza wengi

Aliekwambia uchawi unatumika kuextract madini Nani??[emoji849]
Wasukuma/wanyamwezi na mauchawi yote jamii zenu ni maskini sana,ardhi yenu ina madini kibao,kuanzia Kahama,ushirombo mpaka nyakanazi,kakola,Geita,bulhanhuru,kote huko ni madini lakini watu wake ni maskini sana.
Sasa hayo maujuzi ya uchawi yamewasaidia nini?
 
Pale magu ni balaa, mwaka 2017 nikiwa nafanya project flani na NBS (National Bureau of Statistics) gari yetu ilikula mzinga mmoja hatari sana, yani ilipindikuka tairi zikaangalia juu. Bahati yetu field officers wote pamoja na dereva tulitoka wazima. Na ndio ilikuwa imebaki wilaya hiyo tukamilishe project kwa mkoa wa Mwanza. Ilibidi turudi Mwanza mjini kupumzika badae tulianza kutokea mjini kwenda magu badala ya kulala magu kama ilivyokuwa mwanzo.

Kwa waliobahatika kushiriki agricultural survey ya mwaka 2016/2017 chini ya ofisi ya taifa ya takwimu mtakuwa mnakumbuka hili tukio.
 
Ana bahati hakukutana na watu wa Mungu mwenye nguvu wangemsambaratisha na uchawi wake ungeisha
Njooni muone comment ya qisenger
IMG_20211014_072938.jpg
 
Magu kiboko,kuna mguu wa wilaya mmoja mama mmoja matata sana aliingia kwa mbwembe Magu,siku moja akaamka asubuhi yuko kiwanja cha mpira na nywele za chin wamemnyoa yule alindoka magu siku hiyo hakurudi tena,kutawala mij kama hiyo inatakiwa utumie akili na sio mabavu
 
Upo uchawi wa kufunga ukoo, familia, mtaa,mji,nchi,eneo nk unaitwa malila,kwa kuweka maagano Ili chochote kigeni yakiwemo maendeleo yasiwepo kwenye eneo husika lililofungwa,thus utaona tabia Jamii fulani ya eneo husika huwa na tabia zifananazo mfano uvivu,wizi,hawaoleki,awamalizi shule, ujengi,nk jua eneo hilo limefungwa, zamani vijijini wengi waliogopa kujenga ukijenga tu laana ile inakupata utakufa,fukuzwa kazi au yakuharibikie mambo,nk.
Malila ni uchawi au mikosi inayofungwa na wenyeji Ili kulinda Jamii yao na muingiliano au tamaduni ngeni ni hadi tena wazee waliofunga maagano hayo wayafungue au waruhusu vipya wavitakavyo Ili viingie tena kwenye Jamii yao.
Msikilize aliyekuwa Sauli kabla ajawa Paulo



Nimemaliza clip no.1.
Good at all
 
Ng'wanakapolo tafsiri yake ni mtoto wa Kapolo. Kapolo ni muhogo usio na uchangu, muhogo mtamu.

Miaka ya 1970s hadi 2000 jina hilo lilivuma sana kwenye mji wa Magu uliopo mkoani Mwanza.

Hata kama hukubahatika kumuona kwa macho hakika jina lake ungelisikia tu likivuma maana huyu ndiye aliyewaweka pangoni kwenye vilima vya Nyambitilwa misukule mbalimbali hadi ya kihindi na kizungu.

Miaka ya nyuma alikuwepo bwana mmoja akiitwa Lupondije (Malaki). Aliitwa jina la MALAKI kwa kuwa alikuwa na malaki ya ng'ombe .

Huyu bwana aliamua kujenga jengo la ghorofa kumi pale Magu mjini. Akaanza ujenzi na akiwa anaendelea , Ng'wanakapolo akamfuata akamwambia ghorofa lako liishe hapo, unatuletea mambo ya kigeni (mashikolo mageni) ili iweje? Hapo ujenzi ulikuwa umefika kwenye ghorofa ya nne.

Bwana Malaki hakuwa mkaidi, aliamua aachane na ujenzi ili kuinusuru nafsi yake.

Ng'wanakapolo anatajwa kuhusika na kuwachukua msukule wazungu wawili ambao walikuwa wanajenga barabara ya Mwanza kwenda Musoma.

Wazungu hao walipotea kimiujiza na hawakuonekana tena hadi baada ya miaka kadhaa misukule ya bibi Ng'wanakapolo ilipobainika kwenye milima ya mawe ya Nyambitilwa.

Huko walikamatwa fisi wengi sana wakiwa wamevalishwa hirizi na nguo. Pia ilikutwa misukule mbalimbali wakiwemo wazungu wawili wa Sogesca, muhindi mmoja na Waafrika zaidi ya kumi na tano.

Licha ya Magu kuwa na wafanyabiashara wengi wakubwa wa mifugo na samaki bado wanaogopa kujenga maghorofa kwa kuogopa kulogwa.

Kifo cha Ng'wanakapolo kiliacha gumbo kubwa hapo Magu kwani watu hawakuamini kwamba Ng'wanakapolo anaweza kufa siku moja kutokana na nguvu zake na ubabe wake wa kichawi.
The idiot is now msukule as well. Haya maisha watu wanajitutumua na uchawi wakati hauna msaada wowote
 
Back
Top Bottom