Kuna eneo moja Geita ukiwa unaelekea Msalala, kuna makaburi mengi ya wazungu. Wanasema hilo eneo ndiyo palikuwa pajengwe Chuo Kikuu ambacho kipo Uganda, kikitambulika kwa jina la Makerere. Katika hilo eneo ni pazuri sana pana mvuto.
Ila wenyeji waliwaroga wazungu na kuwauwa, kiasi kwamba walikimbia na kuhamia Uganda ambapo walianzanisha Chuo cha Makelele. Hilo eneo lipo waweza fika Msalala ya Geita na kupata historia. Kuna makaburi mengi sana ya wazungu. Walikuwa wanarogwa na kufa kibao wakakimbia hilo eneo.
Usukumani hawa wanaamini sana mambo ya uchawi ni utamaduni wao. Miaka ya nyuma kule Bulima au Sogesca waliuwawa wazungu wengi kwa uchawi. Maeneo ya Nyashimo kulikuwa na wahindi wengi sana. Huko kulikuwa na misukule kibao.
Kama umesoma historia ya mwanamalundi huyu wajerumani walimuogopa kwa miujiza aliyowafanyia. Alifungwa lakini akawa anavuka bahari kama Musa na kwenda kustarehe kariakoo na sehemu mbalimbali wakati huo. Walitaka kumnyonga wakashindwa. Huyu alikausha miti kwa kuonyoosha kidole, aliacha alama za nyao zake katika miamba mingi sehemu mbalimbali za Tanzania. Mzungu hana ujanja kwa uchawi wa mwafrika. Huyu Mwanamalundi kwao wangemwita Mtakatifu kwa miujiza alofanya.
Namfahamu mama mmoja alikuwa missionari huko kusini jombe, huyu alilogwa tena miaka ya hivi karibuni. Akaenda Ulaya ugonjwa hauonekani, lakini hali mbaya akaambiwa na wenyeji atibiwe kienyeji, alisurrender na kutibiwa kienyeji na kupona. Karejea yuko kwao Ulaya. Hii ni story ya kweli. Make alileta dharau kwa wabena wakamtengeneza. Hivyo si kwamba mwafrika hawezi mloga mzungu.
Siku hizi Ulaya wanaamini katika uchawi wanasafiri kwenda kununua uchawi. Na mzee mmoja mzungu ni rafiki yangu huyu ni mchawi. Alienda Meddetranian kununua uchawi, kauwa watu wengi hasa wachungaji. Alinipa historia kwanini aliamua kuwa mchawi. Na kaanzisha dini ya uchawi anawafuasi kibao ulaya na maeneo mbalimbali duniani. Wazungu wanamuogpa sana huyu mzee. Alinambia Ulaya wanaheshimu na kuogopa uchawi toka Africa, kwa sababu unanguvu na Africa ndo mama wa uchawi. Story yake ni ndefu sana. Pia kuna shemeji yangu ni mzungu, huyu dada utokewa na mizimu ya kwao na mamake, yeye utoa ramli na kuongea na watu walokufa. Huko Romenia uchawi ni mkubwa sana.
Uchawi umeongelewa katika vitabu vitakatifu, upo na unanguvu si jambo geni. Uchawi ni nguvu za kiroho, ila waafrika tunadhani ukisema uchawi haupo, utaonekana weye ni wakisasa. Uchawi upo na hata wazungu wapo wachawi, waafrika wapo wachawi, wahindi wapo wachawi na hata wachina. Kikubwa kama una imani ya Mungu endelea kuamini. Na uhakikishe kama unamshika Mungu mshike kwelikweli.