Tatizo watanzania wako negative sana. Hawajui hata maana ya insurance. Ukiacha vitu hivi vikawa havina taratibu utaua mfuko. Watu wanalalama kwamba NHIF ni wazeewa makato, ndio, maana wanachokata kwako wewe unayelalama, ndicho kinachowalipia matibabu maelfu ya watu ambao ama wanaumwa wao au wategemezi wao.
Kuna jamaa wanapiga kelele humu, lakini utakuta tegemezi wake ana magonjwa sugu kibao, na anakula pesa za mfuko wa Bima zaidi ya laki 2 kila mwezi, wakati huyo mtoto wa tegemezi anakatwa kila mwezi chini ya elfu 50. Sasa ikiwa tegemezi wake anakula zaidi ya laki 2 kwa mwezi, na yeye na familia yake labda pia anatibiwa hapa na pale, unadhani hizo pesa za juu zinatoka wapi? Zinatoka kwa wanachama wengine ambao wanakatwa pesa ndigo kila mwezi, lakini hawaumwi.
Ukitaka ujue umuhimu wa bima, subiri yakufike.
Kulikuwa na umuhimu kuwa na kipengele cha kujitoa kwenye huu mfuko, ili watu waje wasimulie yakiwapata.
Kumbuka mchango unaotoa NHIF, huwa hautoshi kukupa matibabu.