NHIF huwezi katia bima wategemezi waliopo kisheria mfano mama akibadili jina

NHIF huwezi katia bima wategemezi waliopo kisheria mfano mama akibadili jina

Majina ya mama yako/mama mkwe wako yako tofauti ya yaliyoandikwa kwenye cheti cha kuzaliwa.

Yaani kama mama wakati anakuzaa alikuwa anaitwa Anastazia Tatu Peter (jina la babake au Mme wa zamani) na sasa kwenye cheti chake cha NIDA au cha kura anaitwa Anastazia Tatu Mahendeka.

NHIF hawampi bima kwa maelezo kwamba ni watu wawili tofauti, hence, ni forgery.
Hawatambue hati ya kiapo cha mahakamani/mwanasheria (affidavit) kwamba NHIF hawaitambui kisheria hata kama iko sheria za nchi.

Kama mwenza wako ana ajira na ana bima yake kwenye ajira yake, huwezi kata bima kwa ajili ya wakwe (wazazi wa mwenza wako) kama mke/mme si sehemu ya wanafuaika wa bima yako. NA yeye hawezi nufaika na hiyo bima kama majina yake yanautofauti na yale yaliyo kwenye cheti cha ndoa na kiapo hakitabuliki pia.

My take: NHIF wawaelezee wananchi vizingiti hivi, hasa kutotambua affidavits ambazo zipo kisheria ili tukate bima tukiwa tunajua kuwa kuna kigingi hicho.
Mkuu issue ya majina kutofautiana sio tatizo kwa NHIF pekee, taasisi zote ukienda majina yametofautiana ni LAZIMA uwe na supporting document za kisheria kuonyesha kwama Amina Aly ndio Amina Mkude

Kama amebadilisha jina kwasababu ya Mume basi cheti cha ndoa kinatosha
Kama ni sababu zingine ikiwemo kukosea jina, kubadili jina nk ni lazima kuwe na DEED POOL kuthibitisha kisheria kwamba Juma Komba ndio Juma Kisoda

Hili la utofauti wa majina ni swala la kawaida sana mkuu ni vile tu ulikua HUJUI au hujakutana nalo
Unaleta cheti chako cha kuzaliwa kinasema Baba yako ni Mshindo moko halafu NIDA ya baba yako inasema Jina lake ni Ally Salum Mshindo na unataka ukubalike tu..... HAPANA kuna utaratibu mkuu
 
Back
Top Bottom