NHIF huwezi katia bima wategemezi waliopo kisheria mfano mama akibadili jina

Sasa mbona unanyanyapaa wenye magonjwa sugu?
 
NHIF ni genge la wahuni, hati ya kiapo ni document ya kisheria, Dawa ya NHIF ni kuwaburuza mahakamani tu ndio wataacha upumbavu wao.
 
Yaani majina uyakoroge mwenyewe then lawama kwa NHIF???

Huyu anaitwa Punda yule Ng'ombe kesho unataka wote waitwe Mbuzi!!!!!

Wabongo tuna akili za hovyo sana
Bahati mbaya sana kilichoandikwa kipo juu ya uwezo wako wa akili kuelewa kimeandikwa nini.

Watanzania wengi wana complication za majina hasa walioolewa wana majina walianza Kwa Wazazi wao na shule wengi walipoolewa walichukuwa ubini wa waume zao, vyeti vyao vya taaluma, cheti cha kuzaliwa na vitambulisho vingine majina hayafanani.

Mfano Salma Kikwete utakuta vyeti vyake vya taaluma ni Salma Malimusi.

Mwigulu Nchemba na Lameck Madelu huyu ni mtu mmoja.

Wewe huna akili.
 
Affidavit haitambiliki huko.. tafuta kitu kinaitwa deed pool umemaliza mchezoo, hyo ndo yenye mamalaka ya kutambua majina yote. Jpo ni gharama zaid
Hata mimi kuna kipindi nilikuwa nafanya mchakato wa kuwaandikisha bima-NHIF familia yangu,pamoja na wazazi pia wakwe.
Sasa mkwe wangu mmoja majina yake ya kwenye cheti za kuzaliwa yalitofautiana na ya kwenye kadi yake ya Nida.
Wakanielekeza nitafute hiyo deed pool,basi nikamfahamisha muhusika akaenda wizara ya ardhi akapewa ndani ya siku moja na gharama yake haikuzidi elfu 20.
Akanitumia nikaipeleka kazi ikawa imeisha,binafsi sikuona usumbufu wowote.
 
Kwamba nikipata hiyo deep poll nitafanikiwa?
naamini inaitwa deed poll.
A deed poll is a signed declaration that binds you to a particular course of action from the date of signing. It is most often used to declare an intention to change your name
 
NHIF intention yao sio kutoa huduma ni kukomoa tu. Imagine kuna dogo mmoja baba yake na mama yake walifariki kitambo akalelewa na kaka yake huko kijijini, kaka amepambana kumsomesha huyo dogo tangu chekechea mpaka leo dogo amemaliza diploma amepata kikazi chake. Kwenye wategemezi wa NHIF si kamuandika kaka yake maana yeye anasema hata baba yake hamkumbuki sababu alilelewa na kaka yake huyo tangu akiwa mdogo.

Eti NHIF wamemkatalia. Ona sasa kwa bahati mbaya ktk harakati za msiha huko kijijini kaka yake kaoata ajali, yani dogo anahangaika huyo hadi anatia huruma. Mbaya zaidi yeye ndio tegemezi kwa kaka yake. Amenipigia simu juzi mpaka analia ananiambia bro kaka anakufa nisaidie, gharama zimekua kubwa na NHIF hawamtambui kama mtegemezi wangu wakati mshahara wangu wanakata kioa mwezi.

Niliwaza nikajisemea hivi hawa ndo wanataka bima ya afya kwa wote?

Hii nchi wapuuzi ni wengi sana
 
 
Serikali iweke option, ikiwa mfanyakazi hataki kujiunga NHIF aweze kujitoa kwa hiari...!! Isiwe lazima kuchangia, iwe willing ya mtumishi kujiunga au kujitoa
Pesa za mifuko ndio zinatakiwa na serikali kufanyixa ufisadi, angalia michango ya wafanyakazi Nssf ilivyokwenda kutupwa Kigamboni Dege.
 
Daahh, limenikuta sasa hili.
Majina ya mama kwenye cheti changu cha kuzaliwa, surname ni tofauti na kwenye ID ya kura(na ndio ID pekee aliyonayo).
 
Daahh, limenikuta sasa hili.
Majina ya mama kwenye cheti changu cha kuzaliwa, surname ni tofauti na kwenye ID ya kura(na ndio ID pekee aliyonayo).
 
Duh poleni sana,mwisho wake ikawaje amepata udhamini wowote mahali
 
Daahh, limenikuta sasa hili.
Majina ya mama kwenye cheti changu cha kuzaliwa, surname ni tofauti na kwenye ID ya kura(na ndio ID pekee aliyonayo).
Ndio uende wizara ya Ardhi Sasa utengeneze hiyo deed poll upeleke NIDA ukarekebishe majina yasome unavyotaka ili update kitambulisho kipya chenye majina sahihi.

Mawakili Mara nyingi wanatoza 30,000/= kukuchapishia hiyo deed poll na wizara ya Ardhi unalipia pesa ya serikali kama 25,000/= sikosei.

Deep poll ikisajiliwa ndio unaipeleka NIDA kujaza fomu kuomba ID mpya Kwa majina sahihi.
 
Pale wizara ya afya palikuwa na Katibu mkuu mshenzi sana, wakati madaktari wana madai yao ya msingi pale Muhimbili aliwadharau na kuwatukana, basi Mungu si Athumani na wala si Mwamedi mama yake akapata maradhi.

Baada ya kuangalia private hospital akaambiwa madaktari bingwa wote wanapatikana Muhimbili, huku private wanakuja part time tu, basi lile jinga likampeleka mama yake Muhimbili wale madaktari wakatonyana jamaa kamleta mama yake, wakasema aje kumtibu mwenyewe Sasa yeye si anatudharau?

Yule mama Alifia Muhimbili, Sasa fundisho Tanzania kuna watu wakipewa Madaraka hawaamini kama kuna siku atahitaji msaada wako.

Haya maisha kila mtu anamuhitaji na kumtegemea mwingine, hata mzoa takataka ni muhimu, nani anaweza kukaa na harufu ya takataka nyumbani? Kwahiyo anayekuja kuziondowa mthamini.
 
NIDA akafanye nini?

Deed poll aipeleke NHIF apate Kadi chap
 
NIDA akafanye nini?

Deed poll aipeleke NHIF apate Kadi chap
Uwezo wako wa kufikiri umeishia NHIF, ungetumia akili zako vizuri ungegunduwa tatizo la msingi lipo NIDA na huwezi kulimaliza Kwa kupata bima tu ya NHIF.
 
Kwa hiyo mtoa mada unataka umukatie Mama Mkwe wako bima,utakuwa umelogwa sio bure
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn moreโ€ฆ