NHIF huwezi katia bima wategemezi waliopo kisheria mfano mama akibadili jina

Mkuu issue ya majina kutofautiana sio tatizo kwa NHIF pekee, taasisi zote ukienda majina yametofautiana ni LAZIMA uwe na supporting document za kisheria kuonyesha kwama Amina Aly ndio Amina Mkude

Kama amebadilisha jina kwasababu ya Mume basi cheti cha ndoa kinatosha
Kama ni sababu zingine ikiwemo kukosea jina, kubadili jina nk ni lazima kuwe na DEED POOL kuthibitisha kisheria kwamba Juma Komba ndio Juma Kisoda

Hili la utofauti wa majina ni swala la kawaida sana mkuu ni vile tu ulikua HUJUI au hujakutana nalo
Unaleta cheti chako cha kuzaliwa kinasema Baba yako ni Mshindo moko halafu NIDA ya baba yako inasema Jina lake ni Ally Salum Mshindo na unataka ukubalike tu..... HAPANA kuna utaratibu mkuu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…