Mi nadhani umeeleza vizuri sana, isipokuwa kuna watu wanalazimisha kushinda urgument bila kuwa na sababu za msingi.NHIF iharibu kama nani wakati wao wamefuata muongozo uliotengenezwa na wizara ya Afya. Je NHIF ni taasisi yenye miongozo yake kwamba ijitungie sera zake kutofautiana na wizara ambayo inayoiongoza hiyo taasisi? Tumia akili acha uswahili. NHIF akuletee hudima ya kibingwa yeye kama nani wakati yeye simtoa huduma ila ni mlipaji wa huduma kutokana na miongozo iliyowekwa au NHIF ikiuke miongozo yote kesho iwe tofauti na wizara uanze kuilaumu katiba na sheria ya bima ya mwaka 2002. Nani alikwambia kuwa NHIF inahusika na Universal Health care wakati miongozo yake bado inatungwa na msimamizi wake ni TIRA sio NHIF. Acha siasa, use senses utaumbuka vibaya. Mahitaji ya kibingwa yanasogezwa na serikari kupotia wizara ya afya, umesoma sheria ya bima afya ikakuambia kuwa nhif ndio msimamizi wa kusogeza huduma za kibingwa. Unataka maingiliano ya kimajukumu?? Au mpaka sasa huku yaelewa majukumu ya NHIF na ya wizara.
Malpractice ni eneo kubwa kwa mamlaka kulifanyia kazi, tunaona nchi zilizoendelea kuna kampuni nyingi za bima hizi za malpractice. Mimi ningekuuliza wewe Hapa Tanzania kuna aina hii ya bima kwa wanataaluma? Au je tuna wana sheria wa kushughulika na hizi Malpractice yaani specifically medical Malpractice Lawyers?
Labda kunge kuwa na prosecutor wa kushitaki kila medical malpractice ingesaidia watu wabishi kufuata miongozo ya utoaji huduma bila mihemko. Kuwa MD pekee sidhani kama inatosha kufanya procedure zote bila vifaa muhimu kuwepo. Hata specialist anahitaji specified tools and equipments to perform certain procedure, siyo kwa sababu tu ana ujuzi huo basi naweza kufanya procedure popote bila vifaa muhimu kulingana na mahitaji ya hiyo procedure.
Umerudia mara nyingi sana NHIF siyo mtoa huduma ni mlipaji wa huduma, lakini nadhani kuna watu hawataki kuelewa au ndio kutaka kuonekana wanajua basi waendelee kubishana.