NHIF na hasara ya zaidi ya Bilioni 204 ndani ya mwaka mmoja tu

NHIF na hasara ya zaidi ya Bilioni 204 ndani ya mwaka mmoja tu

TheForgotten Genious

JF-Expert Member
Joined
Jan 18, 2014
Posts
2,087
Reaction score
3,156
Kwa mujibu wa CAG, shirika la bima ya afya ya Taifa limepata hasara ya zaidi ya 204B, kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo kufanya malipo hewa, na marudio ya malipo kwa huduma ile ile kwa mtu yuleyule na kwa wakati ule ule.

Kwa mimi mdau wa afya NHIF wamekosa mfumo maalumu wa kuhakiki taarifa za malipo, pesa nyingi zinapotea kupitia fomu za malipo ya matibabu.

Fomu hizo huwa zinaweza kuwa duplicated tena wahakiki wanaweza kujua lakini dili linapigwa, ni kitu kisichowezekana mfano form 400 zinahakikiwa na watu, unawaamini vipi? Ipi efficiency yao, ni uzembe kama sio mchongo.

MAPENDEKEZO
NHIF isitishe kutumia fomu za karatasi kurekodi huduma alizopewa mgonjwa na kuandika gharama zake pale, waunde mfumo wa kompyuta ama wa uboreshe huo walio nao ambapo utakuwa ukiretrive data moja kwa moja kutoka hospitali husika, na mfumo huo uwe na uwezo wakufilter wenyewe duplication zozote zile ambazo zitajitokeza kwa namna moja ama nyingine, mfumo ndio ufanye hesabu na sio watu, mfumo ndio uhakiki na sio watu.

Ikibidi NHIF waunde mfumo wao maalumu wa huduma za afya ambao watakuwa wakitoa katika kila hospital ambayo wameingia nayo makubaliano kufanya biashara, mfumo huo utakuwa na uwezo wa kuonesha huduma ambazo zipo katika makubaliano tu na hospital husika, mfumo uwe na uwezo wa kupiga hesabu wenyewe, mtu wa billing wa hospital husika atakuwa na uwezo wa kuangalia jumla ya huduma zilizotolewa hatukuwa na uwezo wa kuongeza chochote, utamsaidia yeye kufanya hesabu zake za ndani nakutunza data.

Haya makosa ni ya mchongo

Kama kuna maofisa wa NHIF WAPO huku basi andaeni fungu niwaandalie idea namna muunde mfumo wenu kama mmeshindwa.

Ni hasara za kizembe
 
Sasa hasara ya 204bn kwa shirika, kisa malipo hewa, duplication ya malipo; nani anawajibika? Nani anawajibishwa?

204bn kama hasara ya mwaka mmoja, ni sawa na sh 50,000 ngapi zile za Toto Afya?

Naunga mkono hoja
 
Wizi serikalini hautapungua mpaka hatua kali zichukuliwe.

1) kuuwawa wezi wa mali za serikali.

2) kutaifishwa mali zao zote, wao na washirika wao, wawemo au wasiwemo serikalini.

3) Tuanzie na sehemu ambazo ndiyo wamepewa majukumu ya kuzuwia hayo, kama vile polisi, takukuru, uwt na vyombo vyote vya ulinzi.
 
Wizi serikalini hautapungua mpaka hatua kali zichukuliwe.

1) kuuwawa wezi wa mali za serikali.

2) kutaifishwa mali zao zote, wao na washirika wao, wawemo au wasiwemo serikalini.

3) Tuanzie na sehemu ambazo ndiyo wamepewa majukumu ya kuzuwia hayo, kama vile polisi, takukuru, uwt na vyombo vyote vya ulinzi.
Shida unakuta mkamata MWIZI naye MWIZI.
 
Kwa mujibu wa CAG,shirika la bima ya afya ya Taifa limepata hasara ya zaidi ya 204B,kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo kufanya malipo hewa,na marudio ya malipo kwa huduma ile ile kwa mtu yuleyule na kwa wakati ule ule.

Kwa mimi mdau wa afya NHIF wamekosa mfumo maalumu wa kuhakiki taarifa za malipo,pesa nyingi zinapotea kupitia fomu za malipo ya matibabu.

Fomu hizo huwa zinaweza kuwa duplicated tena wahakiki wanaweza kujua lakini dili linapigwa,ni kitu kisichowezekana mfano form 400 zinahakikiwa na watu ,unawaamini vipi?, ipi efficiency yao,ni uzembe kama sio mchongo .

MAPENDEKEZO.
NHIF isitishe kutumia fomu za karatasi kurekodi huduma alizopewa mgonjwa na kuandika gharama zake pale,waunde mfumo wa kompyuta ama wa uboreshe huo walio nao ambapo utakuwa ukiretrive data moja kwa moja kutoka hospitali husika,na mfumo huo uwe na uwezo wakufilter wenyewe duplication zozote zile ambazo zitajitokeza kwa namna moja ama nyingine,mfumo ndio ufanye hesabu na sio watu,mfumo ndio uhakiki na sio watu.

Ikibidi NHIF waunde mfumo wao maalumu wa huduma za afya ambao watakuwa wakitoa katika kila hospital ambayo wameingia nayo makubaliano kufanya biashara,mfumo huo utakuwa na uwezo wa kuonesha huduma ambazo zipo katika makubaliano tu na hospital husika,mfumo uwe na uwezo wa kupiga hesabu wenyewe,mtu wa billing wa hospital husika atakuwa na uwezo wa kuangalia jumla ya huduma zilizotolewa hatukuwa na uwezo wa kuongeza chochote ,utamsaidia yeye kufanya hesabu zake za ndani nakutunza data.

Haya makosa ni ya mchongo

Kama kuna maofisa wa NHIF WAPO huku basi andaeni fungu niwaandalie idea namna muunde mfumo wenu kama mmeshindwa.

Ni hasara za kizembe
Kwanini mwenyekiti wa bodi ya NHIF Mr. Juma A.M Muhimbi hajajiuzulu hadi leo?
 
Back
Top Bottom