NHIF na hasara ya zaidi ya Bilioni 204 ndani ya mwaka mmoja tu

Mfano si wapo wameshatajwa na wamejulikana, tuanze na haohao.

Tena iwe hakuna kucheleweshwa, kama uchunguzi umeshafanywa na CAG, iwe kama traffic case tu, adhabu inatekelezwa hapohapo haina haja hata ya kuwafikisha mahakamani.
CCM hawana uwezo huo maana Kuna mgongano wa kimaslahi. Kila unapotaka kumtumbua ni kada au mtoto wa kiongozi mkubwa au mdhamini wa chama tawala Sasa utamuwajibisha vipi?
 
Je nani wakufanya hayo ikiwa mfumo mzima ni mnufaika?
 
shirika la bima ya afya ya Taifa limepata hasara ya zaidi ya 204B, kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo kufanya malipo hewa, na marudio ya malipo kwa huduma ile ile kwa mtu yuleyule na kwa wakati ule ule.
 
shirika la bima ya afya ya Taifa limepata hasara ya zaidi ya 204B, kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo kufanya malipo hewa, na marudio ya malipo kwa huduma ile ile kwa mtu yuleyule na kwa wakati ule ule.
Kaka mkubwa kwema?Nina mazungumzo kidogo nawe nashindwa namna ya kuja Pm yako.
 
Leo umeongea kitu...
 
Hatushangai ongezeko la ghafla la gharama za bima za afya kwa watoto ili kuziba nakisi ya upigaji uliotukuka.

Hivi waziri kazi yake ni kumsifia mama au kutekeleza majukumu yake ikiwemo kuzuia upigaji yakinifu?
 
Nhif hiyo hiyo ukitafuta Mzungu ajae awe CEO utashangaa haipati hasara ...

Wafanyakazi hapo wanafanya fraud
NHIF inapata hasara kwa aina kubwa tatu.
- Frauds ( Wafanyakazi NHIF ) wanakula MICHONGO na Hospitali binafsi, wanaweka claims za kutisha halafu wanapata mgawo.

Nchi hii ni shamba la Bibi.

- Utungaji wa vifurushi uchwara.
( Mfumo wa bima unafanya kazi kea njia ya "pooling together of risks" . Yaani mchangie wengi, wachache watumie.
Sasa unapoweka vifurushi vya mtu mmoja mmoja, hata Kama utamwekea kiwango Cha Milioni 2 kwa mwaka kiuhalisia Bado utakula hasara. Kwasababu, unakuta mtu ana chronic diseases let's say FIGO anafanya dialysis Mara Mbili kwa wiki, na kila dialysis ni ni 400,000!!
Na Sasa hivi nchi hii Ina mzigo mzito sana wa magonjwa yasiyo ya kuambukiza.

- UNAFIKI, UCHAWA, Matumizi makubwa na Nepotism.
Mashirika yote ya umma Wakurugenzi wake hawapatikani kwa meritocracy (uwezo). Ni CCM wanapeana tu. Shirika lipate hasara hata miaka 500 hawawezi kukosa mishahara yao mikubwa na marupurupu , maana wanapewa Ruzuku yote.


Lakini ingekuwa mishahara yao Kama ya TAMISEMI na ukubwa wa mishahara yao unatokana na faida ya shirika labda wangekuwa serious.

Nchi hii imeshashindwa kila kitu, ni watu wanagawana ulaji watulie Basi.


Masikini wasio na sauti Basi.
 
Hayo unayoyaona leo kutoka kwa CAG ni mazao ya Magufuli.
 
Nchi inapigwa wajinga sisi tunashangilia
 
Kwamba CCM mnaweza kumshughulikia Ridhiwani Kikwete, Mchengerwa, Pinda Jr, Nnape Nnauye, January Makamba, Zahra MICHUZI, Lowassa Jr???


Kiuhalisia inafahamika kwanini hao watu wapo kwenye nafasi walizopo.

Hao watu hawakupewa nafasi walizonazo ili walete Ufanisi.

Kwahiyo hata wavuruge vipi huo uwezo wa kuwashughulikia HAUPO.
 
Kuna mwaka waliwahi pata faida?

Hasara nyingi zinasababishwa na uzembe,na wizi na kuajiri watu incompetent.

Mtu kama Makinda eti ni Mkuu wa Bodi ya NHIF,ana kipi kipya anaweza offer?

Shirika hili limeundwa lilete faida lakini hakuna kitu,Kuna malipo ya bil.28 wamelipua Vituo vya Huduma bila kutoa Huduma.

Ikibainika ndivyo ilivyo ni kuvunja Bodi na management yote upya na kuanza recruitment ya staff upya.
 
Tatizo sio mfumo tatizo ni watu.Hata wewe wakija uwaundie mfumo watataka wapandishe bei ili wapige hela.Hata kama mfumo ukiwepo watauzima waseme upo down ili wapate namna ya kupiga.Swali ni Je tunawezaje kudhibiti watu kama hawa?
 
Hizo ni fikra zako, upo huru.
Sio fikra ni FACT, mfano Bonde la Ihefu ripoti ya kina Balile mbele ya Makamu wa Raid ilisema Kuna familia 12 za vigogo wakubwa wa serikali ndio maana ikawa ngumu kuwaondoa. Same to JPM alipopewa ripoti ya wezi wa Mali za CCM akagundua 90% ni vigogo waandamizi wa CCM Sasa utawakamataje?

Conflict of interest au state capture ni tatizo kubwa kwenye uwajibikaji.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…