NHIF Waongeza gharama za Bima ya Afya kwa Watoto, sasa kulipa Tsh. 120,000/= badala ya Tsh. 50,400/=

NHIF Waongeza gharama za Bima ya Afya kwa Watoto, sasa kulipa Tsh. 120,000/= badala ya Tsh. 50,400/=

sajosojo

JF-Expert Member
Joined
Apr 14, 2010
Posts
1,021
Reaction score
636
Ni kilio, baada ya NHIF kufuta kifurushi cha Toto Afya na kulazimisha mzazi kukata bima ya afya pamoja na Watoto wao na gharama kupanda kutoka 50,400 mpaka 120,000 kwa mtoto mmoja.

Screenshot_20230315-002526.png
 
Haya mambo ya NHIF yananikumbusha miaka hiyo Mzee mmoja alikuwa HR wetu.

Wale wazungu kwenye vikao vya management wakajadili njia bora ya wafanyakazi kupata matibabu je wawe wanaleta risiti ya matibabu kuclaim refund au waingie mkataba na hospitali?

Basi yule Mzee HR Mtanzania mwenzetu bila aibu akasema mishahara yetu tayari ina pesa za matibabu, basi wale wazungu wakaona kwakuwa huyu ni Mtanzania mwenzetu basi yupo sahihi.

Kimbembe akaumwa mke wake tikatika Mzee akampeleka Agha Khan si HR wa kampuni ya wazungu bwana, mama alilazwa wiki mbili tu bill million 15, akachukuwa invoice akapeleka ofisini ili wazungu wamlipie, Sasa ninachowapenda wazungu wapo straight wakamuulize Mzee swala la matibabu si lipo kwenye mishahara ya wafanyakazi?

Huu ndio ubinafsi nauona kwa NHIF, wao hawajioni kama ni Watanzania au wana ndugu wanaoathirika na huu upuuzi wao.

Kwa huruma ya wazungu walimpa cheque yulw Mzee akalipe bill lakini atakatwa pesa yote kwenye mshahara wake.

Kwa roho mbaya ya yule Mzee Mungu akamlaani ampaka anakufa anakaa vigorofa vya NHC vya nyumba viliwi na sebule wakati alipaswa awe na mjengo wa maana na compound ya kutosha.
 
Hii issue naona serikali ingekaa na wadau waangalie namna bora ya kuifanikisha, maamuzi mengi wanayochukua peke yao huwa mwishowe yanawaumiza watanzania wa kipato cha chini.

Sioni tena umuhimu wa kuwa na bima ya afya kwenye hii nchi, kinachoenda kutokea ni kujiandaa tu na pesa zako mfukoni.
 
Hakuna kama samia huyu rais wa ndoto zangu haiwezekani mtoto atibiwe kwa hela ndogo kama keeli unampemda mwanao
Hapo nchi kama kenya laki 3 ghana laki 340 kwa mtoto mmoja
Usa wao 1.6m per kid

Ni kuonesha namna gani unampenda mwanao


Twende na samia mpaka 2050

Kaupiga mwingiiiiiiiii
 
Hii issue naona serikali ingekaa na wadau waangalie namna bora ya kuifanikisha, maamuzi mengi wanayochukua peke yao huwa mwishowe yanawaumiza watanzania wa kipato cha chini.

Sioni tena umuhimu wa kuwa na bima ya afya kwenye hii nchi, kinachoenda kutokea ni kujiandaa tu na pesa zako mfukoni.
Halafu kuna siku wakikaa kwenye vikao vyao wanaanza kushangaa na kujiuliza "hivi sisi ndiyo tulipitisha hii?". Ooh Jehova tutetee sisi watanzania.
 
Nchi hii kulipia vitu wana copy Nchi za Ulaya wakati wenzetu wao hawana vyanzo vya kodi zaidi ya watu kuchangia kwa % kubwa huku vyanzo tulivyo navyo utadhani ni vya Waarabu havichangii kitu chochote kumpunguzia Mwananchi maumivu hizo hospital za kanda gharama zake utadhani wanaotibiwa ni Wageni...Roho mbaya, ubinafsi na kutokujali mahitaji muhimu ya Wananchi ndio inapelekea muda wote kuja na gharama za ajabu ajabu....
 
Back
Top Bottom