NHIF Waongeza gharama za Bima ya Afya kwa Watoto, sasa kulipa Tsh. 120,000/= badala ya Tsh. 50,400/=

NHIF Waongeza gharama za Bima ya Afya kwa Watoto, sasa kulipa Tsh. 120,000/= badala ya Tsh. 50,400/=

Ni kilio, baada ya NHIF kufuta kifurushi cha Toto Afya na kulazimisha mzazi kukata bima ya afya pamoja na Watoto wao na gharama kupanda kutoka 50,400 mpaka 120,000 kwa mtoto mmoja.
Naona ni mkakati wa kuwahimiza watu kutozaa sana.. wenye watoto kuanzia watatu gharama ni nzito kweli kweli... watanzania punguzeni kuzaa hovyo..
 
Uzuri wa kukaa kwenye kiyoyozi hujui chochote kuhusu wengine ni kuamua tu ongeza hapa zidisha pale lengo ni hili... yaani ni maamuzi utadhani wanatumi taco kuamua. Ujinga kabisa... kwenye highschool za serikali wazazi wamelipishwa 50400 wakati watoto wanaingia form five lakini mpka leo hakuna kadi na naamini mpaka watamaliza six hakuna card. Hii nchi bi tozo ilishamshinda... kabaki na "mkalitazame na hili"
 
siyo ccm tu hata kije chama gani hali itakuwa hiyo hiyo tu.haya kenya upinzani umechukua dola lkn hali ya maisha imepanda maradufu ya ile ya awali.vyama pinzani au tawal si suluhisho la utatuzi wa maisha ya mwananchi kwani hivyo vyote viko kwa maslahi binafsi.nadhani suluhisho ni kupata katiba nzuri itakayowawajibisha watawala.
 
Ni kilio, baada ya NHIF kufuta kifurushi cha Toto Afya na kulazimisha mzazi kukata bima ya afya pamoja na Watoto wao na gharama kupanda kutoka 50,400 mpaka 120,000 kwa mtoto mmoja.
Serikali ya Ccm imeamua kufanyia afya za watu biashara.
Hii ni kutokana na bunge kuwa la chama kimoja.
Wamekosa mawazo mbadala. Kila kitu kwao ni sawaaaa. Maana wao hutibiwa kwa kodi zetu.
 
Serikali ya Ccm imeamua kufanyia afya za watu biashara.
Hii ni kutokana na bunge kuwa la chama kimoja.
Wamekosa mawazo mbadala. Kila kitu kwao ni sawaaaa. Maana wao hutibiwa kwa kodi zetu.
Kuna haja ya kuhakikisha wateule wanaishi kwa mishahara yao bila posho zozote ili wa feel ile squeeze ya maisha kusudi wawe wanatatua matatizo ya raia badala ya kuwagandamiza.
 
NHIF inaeneshwa na watu wasio jua wanafanya nini.
Hawajui hasara wanayopata inatokea wapi wao suluhisho ni kupandisha vifurushi tuu
Kwa senior citizens miaka 65 kuendelea ndio mlie tuu ni takriban tshs. 1,000,000-kwa mwaka na ndio kundi la wastaafu.
 
Ndugu zangu,
Iko hivi, hii bima ya toto afya na nyinginezo za private wanajiunga baada ya familia husika kupata tatizo la kuuguliwa na mtoto au ndugu. Ukiwa na mfuko wa NHIF ambao wanachama wake wanajiunga wakiwa wanaumwa karibu wote ni hatari Kwa uhai wa mfuko wenyewe.
 
Back
Top Bottom