NHIF Waongeza gharama za Bima ya Afya kwa Watoto, sasa kulipa Tsh. 120,000/= badala ya Tsh. 50,400/=

Hii issue naona serikali ingekaa na wadau waangalie namna bora ya kuifanikisha, maamuzi mengi wanayochukua peke yao huwa mwishowe yanawaumiza watanzania wa kipato cha chini.

Sioni tena umuhimu wa kuwa na bima ya afya kwenye hii nchi, kinachoenda kutokea ni kujiandaa tu na pesa zako mfukoni.
Mission ya Serikali, na mission ya wadau ni tofauti sana na ndio maana hata wakikaa hawapata muafaka.

Serikali imeshakopa sana huo mfuko na haiko tayari kulipa MADENI.

Huo mfuko umeshafanyiwa ufisadi wa kutisha na HAKUNA aliye tayari kuwajibishwa.

Wafanyakazi wa huo mfuko wanajichotea tu pesa na kujikopesha majumba ya milioni 100 na hawako tayari kuacha.

Mfuko Sasa hivi umeelemewa na MADENI kutoka kwa watoa huduma na unaelekea KUFILISIKA.

Mbwembwe zote unazoziona, kupandisha Bei za vifurushi, kuondoa baadhi ya watu wanufaika na Bima ya Afya kwa wote ni JANJA JANJA na Mbinu za kunusuru NHIF.

Kwahiyo, ili uelewane nao labda uwaambie utalipia hivyo vifurushi vyao halafu utaacha kutumia kadi yao ya matibabu ili wasilipe chochote.
 
Ni kilio, baada ya NHIF kufuta kifurushi cha Toto Afya na kulazimisha mzazi kukata bima ya afya pamoja na Watoto wao na gharama kupanda kutoka 50,400 mpaka 120,000 kwa mtoto mmoja.
WaTanzania asili yetu ni watu wa kulalamika lalamika bila hata kutumia akili zetu ku- reason out, hiyo kasumba ililetwa na siasa za ujamaa za kuchonganisha sera za kibepari na raia wake, 120,000 ni sawa na sh 10,000 kwa kila mwenzi kwa ajiri ya afya ya mwanao.

Kwa kweli hiyo sio nyingi, kwa nchi nilizo tembelea bima ni gharama kubwa sana mara 5 au 10 na ya kwetu, tuwe fair some time, mtumishi wa wastani anakatwa 40,000 ya mshahara wake kila mwezi kwa ajiri ya bima hao ndo wanao fidia hiyo pesa tuwe waelewa katika vitu vya msingi kama afya ya wstoto wetu kama huwezi kutenga 10k kwa ajiri ya afya ya mwanai kila kwanini unaendelea kuwapa wanawake mimba?
 
Si kweli kwamba waajiriwa wote wanachangia kiwango kikubwa kuliko watu binafsi.
Nitatoa mfano wa muajiriwa mwenye mshahara wa wa milioni 2. Asilimia 6 yake ni 120,000. Kwa mwaka atalipa 1,440,000. Kiasi hiki kinabeba wanufaika 6. Miongoni mwa wanufaika ni wazazi na wakwe wao. Kila mnufaika mchango wake ni 240,000.
Sasa mchangiaji binafsi wa kundi la umri 35 hadi 59 anachangia 2,220,000 akibeba mwenza wake na wategemezi wanne. Tayari analipa zaidi. Isitoshe atapata huduma pungufu akienda kutibiwa.
Ikumbukwe mshahara wa 2m ni wachache wanaoukaribia.
 
Tatizo nilionalo ni kwa sababu gani waajiriwa wapate huduma nyingi kuliko wanaolipa binafsi. Vifurushi ni ubaguzi.
 
Si kweli kwamba waajiriwa wote wanachangia kiwango kikubwa kuliko watu binafsi.
Nitatoa mfano wa muajiriwa mwenye mshahara wa wa milioni 2. Asilimia 6 yake ni 120,000. Kwa mwaka atalipa 1,440,000. Kiasi hiki kinabeba wanufaika 6. Miongoni mwa wanufaika ni wazazi na wakwe wao. Kila mnufaika mchango wake ni 240,000.
Sasa mchangiaji binafsi wa kundi la umri 35 hadi 59 anachangia 2,220,000 akibeba mwenza wake na wategemezi wanne. Tayari analipa zaidi. Isitoshe atapata huduma pungufu akienda kutibiwa.
Ikumbukwe mshahara wa 2m ni wachache wanaoukaribia.
Mkuu kumbuka wengi hao waajiliwa wako sehemu nyingi za vijijini hawapati hiyo huduma ya afya ya bima kwasbb mawilayani hiyo huduma iko mjini tu tena hopitali moja au mbili, at the end the day sie tuliko Town ndo tunafaika.
 
Ni kweli usemacho kwamba wengi wako vijijini. Binafsi nasikitika kwa ubaguzi. Namlipia binti yangu 516,000 (TIMIZA). Umri wake 23. Anapata huduma pungufu kuliko anaebebwa na mchangiaji wa 120,000 kwa mwaka
 
Mtu Kama Hana ugonjwa wowote wa kurithi au wa Kupata ukubwani

Achana na Bima Mwambie azingatie kula vizuri , mazoezi na kukaa Mbali na ngono . Hiyo bima ni kuwanufaisha wanasiasa tu.
 
Looooh mama kaona hili kweli kuna mbuzi zinaanza kutoa boko hili utawala wake uonekane bure kabisaaaa mama fanya reform hapa NHIF ikiwezekana timua wote jamaa wanamakusudi sana nkumbuka nshawai lipiaga bima yao lakini sikuwaigi itumia mwaka mzimah hadi ikaisha naambiwa hipo rejected mbuzi sana hao watu bureee kabisa nime wa email kutafuta msaada email zangu wanatupiana mpira fulan mjibu mteja nae anapeleka hoja kwa mwngne fulan mjibu wew. Mwezi mzimah nasubiri majibu yao fuko la bima la hovyo kweli hili
 
Back
Top Bottom