Haya mambo ya NHIF yananikumbusha miaka hiyo Mzee mmoja alikuwa HR wetu.
Wale wazungu kwenye vikao vya management wakajadili njia bora ya wafanyakazi kupata matibabu je wawe wanaleta risiti ya matibabu kuclaim refund au waingie mkataba na hospitali?
Basi yule Mzee HR Mtanzania mwenzetu bila aibu akasema mishahara yetu tayari ina pesa za matibabu, basi wale wazungu wakaona kwakuwa huyu ni Mtanzania mwenzetu basi yupo sahihi.
Kimbembe akaumwa mke wake tikatika Mzee akampeleka Agha Khan si HR wa kampuni ya wazungu bwana, mama alilazwa wiki mbili tu bill million 15, akachukuwa invoice akapeleka ofisini ili wazungu wamlipie, Sasa ninachowapenda wazungu wapo straight wakamuulize Mzee swala la matibabu si lipo kwenye mishahara ya wafanyakazi?
Huu ndio ubinafsi nauona kwa NHIF, wao hawajioni kama ni Watanzania au wana ndugu wanaoathirika na huu upuuzi wao.
Kwa huruma ya wazungu walimpa cheque yulw Mzee akalipe bill lakini atakatwa pesa yote kwenye mshahara wake.
Kwa roho mbaya ya yule Mzee Mungu akamlaani ampaka anakufa anakaa vigorofa vya NHC vya nyumba viliwi na sebule wakati alipaswa awe na mjengo wa maana na compound ya kutosha.