WaTanzania asili yetu ni watu wa kulalamika lalamika bila hata kutumia akili zetu ku- reason out, hiyo kasumba ililetwa na siasa za ujamaa za kuchonganisha sera za kibepari na raia wake, 120,000 ni sawa na sh 10,000 kwa kila mwenzi kwa ajiri ya afya ya mwanao.
Kwa kweli hiyo sio nyingi, kwa nchi nilizo tembelea bima ni gharama kubwa sana mara 5 au 10 na ya kwetu, tuwe fair some time, mtumishi wa wastani anakatwa 40,000 ya mshahara wake kila mwezi kwa ajiri ya bima hao ndo wanao fidia hiyo pesa tuwe waelewa katika vitu vya msingi kama afya ya wstoto wetu kama huwezi kutenga 10k kwa ajiri ya afya ya mwanai kila kwanini unaendelea kuwapa wanawake mimba?
Covax, ni kweli tuna kawaida sana ya kulalamika lakini sidhani ni sahihi kudhani tabia hiyo ndio msingi wa malalamiko!! Sio kwa sababu ya kulalamika ndio tunalalamika! Kwa jinsi madawa yanavokuwa hayapatikani au magonjwa kutolipiwa bima, ongezeko lolote lisiloendana na uboreshaji wa huduma - ni wizi!! Ndicho kinacholalamikiwa na wengi hapa japo wengi wameshindwa kukieleza.
Unazungumzia gharama ya juu ya bima za wenzetu - je gharama hizo zinawiana na kiwango cha bima??? Nadhani jibu litakuwa ni NDIYO. Je ukiondoa hili ongezeko, kuna guarantee imetolewa kuhusu uboreshaji au upatikanaji wa huduma???