NHIF yafuta Bima ya Afya kwa watoto "TOTO Afya Kadi". NHIF yadai hawajafuta ila wameboresha

NHIF yafuta Bima ya Afya kwa watoto "TOTO Afya Kadi". NHIF yadai hawajafuta ila wameboresha

benzemah

JF-Expert Member
Joined
Nov 19, 2014
Posts
1,533
Reaction score
3,187
Habari za awali zinadai kwamba Mfuko wa Taifa wa BIma ya Afya umefuta rasmi bidhaa ya "Toto Afya Kadi" iliyokuwa inatolewa na mfuko huo kwa watoto wa chini ya miaka 18 wanaosajiliwa ili kuwawezesha kupata huduma za matibabu katika vituo vilivyosajiliwa na NHIF nchi nzima.

Ikumbukwe kuwa Toto Afya Kadi ilikuwa inatoa nafasi kwa watoto chini ya miaka 18 kutibiwa kwa gharama ya Tsh. 50,400/= kwa mwaka mzima.

Lakini miongozo iliyotoka hivi karibuni inaonesha kuwa mwanachama aliyekuwa akitibiwa kwa bima hii hawezi kufanya malipo mapya pale bima yale inapokwisha muda wa matumizi (hawezi kurenew).

Hivyo ni kama imeondolewa kimyakimya na hata ukitaka kulipia Bima hiyo hivi sasa wanakwambia kuwa huduma haipo.

======

NHIF yatoa ufafanuzi kuwa hawajafuta kifurushi cha Toto Afya ila wameboresha ili na wazazi wao waingie.

IMG_20230313_181053_540.jpg



 
Waharakishe hiyo bima ya afya kwa wote ndio utakuwa mkombozi bila hivyo halmashauri zitenge maeneo mengi kwa ajili ya makaburi, bila Serikali kuweka mkono wake kwenye huduma za afya kwa wananchi wake watu wengi tutakufa kwa kushindwa kumudu gharama za matibabu.
 
Back
Top Bottom