NHIF yasitisha mabadiliko yaliyokuwa yaanze 2/8/2022

NHIF yasitisha mabadiliko yaliyokuwa yaanze 2/8/2022

waongo hawa wameogopa kelele lkn ukienda hospital utakuta utekelezaji unaewndelea. Hii wanaita "wapoze na uwapotezee"
Kuna kila dalili ya ukweli wa hoja yako mkuu, ngoja tuone itakuwaje
 
Nimeona Kwenye social media na breaking news ya ITV kuwa wizara ya Afya imesitisha utaratibu uliokuwa umewekwa na bima ya Afya NHIF na kuanza kutumika tarehe moja August-2022 .Wito wangu serikali iende mbele zaidi isiishie kusitisha tu utaratibu huo bali ichukue hatua kwa wahusika.Haiwezekani mtu anachangia fedha yake ili apate matibabu halfu anakuja mtu anaanza kumpangia anapaswa kuugua mara ngapi kwa mwezi au wiki.Tendo la kuugua sio la hiari bali linakuja kadri mwenyezia Mungu anavyopanga hakuna binadamu anayejipangia kuwa sasa niugue.Ni bahati mbaya sana viongozi wa NHIF makao makuu walijipa mamlaka ya Mungu ya kuamua nani augue na mara ngapi?ndani ya mwezi au wiki.Watanzania wanataka kusikia hatua stahiki kwa hawa waliokuwa wameanza kucheza na afya za watanzania hasa wafanyakazi na wategemezi wao.
 
Bima ya Afya na Wizara ya Afya wote makanjanja tu. Nchi hii imejaa mijitu ya ovyo sana.
 
Kama sababu ilikuwa ni kudhibiti udanganyifu unaofanywa na vituo vya afya, sioni sababu kwanini wakaamua kuwadhibiti wanachama wa huo mfuko wa jamii kufuata huduma wanapopataka, huu ulikuwa uamuzi wa ajabu sana.

Dawa kama hilo tatizo la udanganyifu kweli lipo, walishughulikie kwenye chanzo kwa kuwatafuta wahusika wanaosababisha hilo tatizo, na sio vinginevyo.
 
Wamekurupuka wakayakanyaga, sasa wameyanywa.... Wanazingua hawa BIMA
 
Mifuko iko taabani wazee wamekomba pesa za mifuko na hawarudishi kwa wakati.

Mifuko inalazimishwa kutafuta namna ya kupunguza matumizi regadless outcome.

Yajayo yanasikitisha.
 
Hii mifuko ndy source ya mihela ya Kampeni ya Chama chenu cha Kijani. Mumeamua kubuni kubana matumizi ili 2025 mukwapue tena. Kama kawaida yenu huku wachangiaji wakituishwa Mizgo.
 
Hivi hawa NHIF hawakuwahi kutoa gawio enzi zile za bwana yule?
 
Huyu mtanzania angeshika hatamu enzi za giza (ya ukosefu wa mitandao ya kijamii) tungeamka tukakuta nchi nzima imepigwa mnada!

Sijui ni hujuma ama uhuni dhidi ya utawala wake?
 
Baada ya wananchi kupigia kelele mabadiliko ya mfuko wa bima ya afya, hatimaye NHIF wamesitisha mabadiliko hayo.

Hii ndio nguvu ya mitandao ya kijamii

==============

Pamoja na hivyo kumetolewa taarifa mbili ambazo ni wazi zina onesha wahusika hawakujipanga, taarifa ya kwanza imetolewa na NHIF wenyewe wakionesha kuwa walikuwa na utaratibu mpya, lakini baadaye wameona umeleta utata wameufuta.

Dakika 20 baadaye taarifa ikatolewa na Wizara ya Afya kuwa wamesitisha utaratibu huo mpya, ikumbukwe kuwa awali hakuna taasisi yoyote kati ya hizo mbili iliyojitokeza kuzungumzia kuhusu utaratibu mpya.

Inamaanisha kuwa baada ya presha kuwa

CCM NI MAFII
 
Back
Top Bottom