Ni aibu gani uliipata kwenye Interview yako ya Kwanza? Mimi yangu hii

Interview za benki ya Posta, nikaulizwa "unataka tukilipe kiasi gani"
Hapo hata chuo sijamaliza, nimebakiza kuchomoa sup. Nikawazaa, sijui viwango vya mshahara. Nikataja tuu laki nne.
Hata sikuitwa tena
 
Ilikua kwa kiswahili??
 
Ulikua 2019 niliitwa kwenye usaili wa ualimu. Tulipiga written fresh, ikaja practical nikaingia kupiga pindi. Ile shule ni private na wanafunzi wanaumri mkubwa kidogo na wanavaa sare nyeusi chini juu nyeupe.

Miongoni mwa waliokuwepo darasani kumbe alikuwemo mkuu wa shule sikujua maana umri wake Kama wanafunzi tu. Sasa wakati napigisha pindi na msaili anasimamia nikampoint mkuu ajibu swali.

Wanafunzi wakawa wanashangaa,jamaa akajibu swali wakampigia makofi nikahitimisha pindi. Yaliyojiri sinahaja ya kusimulia wote mnajua.
Ilikuwaje mkuu[emoji23]
 
Mm nilienda interview ya taasisi ya kanisa nilivyoingia sikuona kiti cha kukaa maana kilikuwa nyuma ya mlango sasa kulikuwa na kiti karibu na askofu nikawasalimia nikapitiliza kukaa pale panel nzima walicheka kishenzi mmoja ndo akaniambia kiti chako kile kule
Nilipagawa mpaka kiingereza nilishindwa kuongea [emoji23][emoji23][emoji23]
Wakaanza kunipa ushauri tuu ila kazi walinipa [emoji23][emoji23][emoji23]
 
😂😂😂😂Walikuonea huruma hao
 
Nilijamba ushuzi unaharufu mbaya si unajua lile tumbo la uoga linauma kwa mbali na kaushuzi

Nikaambiwa toka nje kwanza maana hall lilikuwa na madirisha madogo halafu hakuna ac

Sent from my Infinix X650 using JamiiForums mobile app
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]Dah utakua uliwakata stimu kweli..... Ulipata kweli
 
Ulikua 2019 niliitwa kwenye usaili wa ualimu. Tulipiga written fresh, ikaja practical nikaingia kupiga pindi. Ile shule ni private na wanafunzi wanaumri mkubwa kidogo na wanavaa sare nyeusi chini juu nyeupe.

Miongoni mwa waliokuwepo darasani kumbe alikuwemo mkuu wa shule sikujua maana umri wake Kama wanafunzi tu. Sasa wakati napigisha pindi na msaili anasimamia nikampoint mkuu ajibu swali.

Wanafunzi wakawa wanashangaa,jamaa akajibu swali wakampigia makofi nikahitimisha pindi. Yaliyojiri sinahaja ya kusimulia wote mnajua.
Si tutajuae kwani tulikuwepo... Malizia mzee.
 
Mi nikifika nkaona tupo wengi kuliko wastani unaotakiwa ..nkaondoka ... Bro Mmoja alikuwa diwani akaniuliza mbona haukuoneka na nilikuwa nimeongea na kamati ... Nkamwambia haikuwa fair nafasi mbili mnatuita ishirini na tano .... Acha wapate wengine.... Ya pili ya tatu nkapenyamo.
 
Back
Top Bottom