Ni aibu kuandaa sherehe za kupokea ndege

Tangu awamu ya Tano tumekuwa na kasumba ya kuandaa sherehe kupokea ndege au kupokea miradi lakini kwa mtizamo wangu mimi mtu wa chini ninaona kama fedheha fulani...
Huyu dikteta mpya anacopy na ku paste mambo ya dikteta wa aliyeenda zake
 
Tusiandae sherehe kuipokea ndege tuliyonunua KATIKATI YA JANGA LA CORONA?!!

Dunia nzima hakuna nchi iliyotoa FEDHA ZAKE kununua NDEGE...ni uthubutu pekee wa Tanzania ...kutokuweka LOCKDOWNS kunatupa nguvu ya KUIPOKEA NDEGE HII/HIZI kwa sherehe ndogo.

#SiempreTanzania
#SiempreCCM
#NchiKwanzaKablaYaNafsiZetu
#KaziIendelee
 
Ndiyo ununuzi wa ndege kinaonekana ni kitu kidogo kwa nchi lakini kina maana kubwa sana miaka ya hivi karibuni hasa baada ya miaka takribani 20 ya kufa kwa kila kitu kilichotambulisha nchi yetu kitaifa na kimataifa...
Yaani wakati mwingine huwa najiuliza,kwa mtindo wetu huu maridadi,wa kwenda kupokea ndege kila zinaponunuliwa, kwa nchi kama SA, Kenya, Ethiopia,Eghypt nk.

Nafikiri marais wao na wananchi wao kila leo wangekuwa busy kwenda kwenye airport zao kupokea ndege mpya....btw kupanga ni kuchagua na kazi iendelee.
 
Tangu awamu ya Tano tumekuwa na kasumba ya kuandaa sherehe kupokea ndege au kupokea miradi lakini kwa mtizamo wangu mimi mtu wa chini ninaona kama fedheha fulani...
Usitegemee mabadiliko ukiwa na ceremonial leaders, wao sikukuu ndiyo fahari, jifunze kwenye vigodoro, mtu anaishi kwenye nyumba mbavu za mbwa lakin siku ya kumtoa mwali au kigodoro, anauza shamba,
  • Anakodi muziki 600,000
  • Analisha wageni siku 3
  • Ananunua sare
  • Anakodo coaster 3
  • Ananunua vinywaji
MWisho wa siku unasikia watoto wamefukuzwa shule hawana michango, wamekosa matibabu hawana fedha ya matibabu
 
Kupanga ni kuchagua, hakuna anayelazimishwa, BTW mazingara vile vile ni tofauti wacha ushamba.
 
Usitegemee mabadiliko ukiwa na ceremonial leaders, wao sikukuu ndiyo fahari, jifunze kwenye vigodoro, mtu anaishi kwenye nyumba mbavu za mbwa lakin siku ya kumtoa mwali au kigodoro, anauza shamba...
Kumbe CHANGAMOTO iko kwenye hulka za watanzania....sasa tutegemee SERIKALI itoke mbinguni?

Chadema watajipotezea muda tu kutaka waungwe mkono katika regime change through endless riots and sit-in🤣🤣

BINAFSI SIUFUKUZI UPEPO

#NchiKwanza
#SiempreJMT
#KaziIendeleee
 
Hii nchi hatuwezi kuendelea maana hata mambo ya muhimu tunakimbilia uchama zaidi. Hata kama unafaidika kuwa mwanaharakati wa hicho chama kwa nini tusiwe na constructive ideas za kusaidia nchi. Kumbuka tuna wajukuu wetu na kama hii nchi ikiharibika hamna cha Chadema wala CCM. Haya machama hayana maana kabisa. Tuwe wote watanzania na tufikirie kuendeleza nchi yetu. Kama watanzania tungekuwa pamoja na kunfikiria mwenzako ni mtanzania tungeweza tukasonga mbele. Haya machama yamefanya wengine wamefungwa, wengine wamekimbia nchi na wengine wameuuawa. Shida tu ni kwamba kwa vile wengi ni wachumia tumbo ndiyo maana mnatetea uchama ili muendelee kula lakini kumbuka kuna leo na kesho. Kwa hapa tulipofika tunahitaji kuiga wachina jinsi ya kuongoza hii nchi otherwise tunakoelekea sioni mwanga kwa sasa.
 
Michango ya kuwachangia kina Lisu imeshaleta jita gani kwa wachangaji na chama kwa ujumla?
LIsu anachangiwa na Kodi? Kama ni wanachama na watu wake mimi inanihusu nini kuhoji ?, Ila kwenye hili ni Kodi zangu pia kwahio lazima nioji
 
Mapokezi ujue pia ni promotion na shirika kutangaza limeongeza ndege. Pia kisiasa hakuna ubaya serikali na chama tawala kuonesha mafanikio yake.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…