Erythrocyte
JF-Expert Member
- Nov 6, 2012
- 128,308
- 245,426
Kyela ni miongoni mwa Wilaya kongwe kabisa za Tanzania , lakini ni Wilaya ya mwisho kabisa kufaidi keki ya nchi hii , kwa miaka yote tangu uhuru imeongozwa na Wabunge wa ccm tu , akiwemo yule mmoja aliyetamba hadharani kwamba ANAMILIKI DIGRII 4 na wala hana njaa yoyote .
Halmashauri ya Wilaya hii haijawahi kuongozwa na chama kingine zaidi ya ccm tangu uhuru wa Tanganyika , huku Mwenyekiti aliyepita wa Halmashauri hiyo akiitwa Hunter Mwakifuna aliyekuwa Diwani wa Ipinda , huyu akishirikiana na DED aliyepita walichukua Soko la Wilaya ambalo ni mali ya wananchi na Chanzo Kikuu cha Mapato na kuipa ccm , yaani soko lililokuwa mali ya Halmashauri sasa hivi ni mali ya ccm (Naapa mbele za Mungu kwamba iko siku nitalirejesha mikononi mwa umma).
Lakini pamoja na Sarakasi zote hizo za watu hawa Wameshindwa kabisa kuwa na UBONGO UTAKAOWAKUMBUSHA UMUHIMU WA KYELA KUWA NA GARI LA ZIMAMOTO , hii ni Aibu kubwa mno na fedheha kwa Watu wa Kyela , Hivi ninavyoandika haya Hospitali ya Binafsi ya Dr Mwaihula , iliyo maeneo ya Mpanda ambako ni karibu na ofisi za Relwe inateketea kwa moto bila msaada wowote , vidumu vya maji vya wananchi havijafua dafu , Mwaka uliopita hospitali ya wilaya ilishika moto na wananchi wakaokoa kwa kutumia njia za kienyeji za kuzima moto , Je siku soko la Kyela lililo katikati ya mji likishika moto (siombei lakini yanatokea) ni nani atasalimika ? kwanini viongozi wa Kyela hawaioni hii hatari , wanataka nini kiteketee ili waone umuhimu wa gari la Zimamoto ?
Nakulilia Kyela , nakuahidi iko siku nitakukomboa .